1995: Benjamin Mkapa (61.82%) Augustino Mrema ( 27.77%)
2000: Benjamin Mkapa (71.74%) Ibrahim Lipumba (16.26%)
2005: Jakaya Kikwete (80.28%) Ibrahim Lipumba (11.68%) Freeman Mbowe (5.88%)
2010: Jakaya Kikwete (62.83%) Willibrod Slaa (27.05%)
2015: John Magufuli (58.46%) Edward Lowassa (39.97%)
Mrema alitetemesha 1995 kwa kupata 27.7%. kati ya 1995 -2000 Mrema alipitia misukosuko mingi na alifanya makosa mengi ya kimkakati hali iliyofanya wananchi wapoteze imani na mrema hali iliyosababisha aanguke vibaya 2000. Hata hivyo mkapa alifanya vema kwenye uchumi ambapo aliito nchi kutoka kuwa ya mwisho kwa umasikini duniani hadi kuwa na promising growth na low inflation rate.
Mwaka 2005 timu Rostam/Lowassa ikiwa na maandalizi ya miaka 10 ilijiandaa sana kiasi cha mgombea wake kupata ushindi wa hatari 80%. Lipumba alianguka vibaya kwa sababu waislam waligawanyika (kwa miaka hiyo nchi ilikuwa na siasa za udini sana). CDM ilikuwa na mgombea weak ambaye alikuwa na ushawishi mdogo wa kisiasa na hakufanya vema sana akiwa Bungeni, hivyo mgombea wake alipata kura kiduchu.
2010 CDM waliweka mgombea mwenye ushawishi mkubwa na ambaye alifanya vema alipokuwa Bungeni. aidha, chama tawala kilikuwa na mpasuko wa kujivua gama ambapo timu Rostan/lowassa ilikuwa kwenye mgogoro na mtoto walio mzaa wenyewe. Aidha nchi ilikumbwa na rushwa ya hatari na wanyonge wakapoteza imani na watawala. kumbuka Richmund, Escrow, vijisenti n.k
Baada ya 2010 CDM walisumbua sana Kulikuwa na mgomo wa walimu na wafanyakazi ambao haujawahi tokea tangu uhuru, Mgomo wa Madktari wa kutisha, njaa, mgao wa umeme wa kutisha na uchumi uliyumba sana na rushwa ilishamiri. CDM walinzunguka nchi nzima kuiponda CC na walipata mapokeo makubwa kiasi cha kustaajabisha na kutisha. likatokea zogo la katiba mpya ambalo lilimshinda mkwere na CDM waliendelea ku capitalize. ilipofika 2015 mwanzoni kulikuwa na ishara CDM kukabidhiwa nchi.
2015 ukatokea mpasuko mkubwa chama tawala Lowassa akaamia CDM na kuteuliwa kuwa mgombea Urais. Yote yaliyojengwa na CDM kiitikadi yakayeyuka. CDM badala ya kuwa mshambuliaji ikawa mtu wa kuzuia mashambulilizi kwa kujitetea mwanzo mwisho. Hoja ya Ufisadi ikafa. Mgombea wa chama tawala akaziteka hoja za CDM na kuanza kuzitumia kujijenga na ku win heart and minds za walalahoi. Mgombea wa CDM akapa itilafu za kiafya zilizosababisha ashindwe kujimudu na kunadi sera zake. CDM ikapoteza ngome yake ya Kanda ya Ziwa na kwa kadiri siku za uchaguzi zilivyokuwa zinasogea Lowassa akawa anapata wakati mgumu. Kumbukeni Kampeni zake mkoa wa Tanga na Njombe.
Pamoja na hayo Lowassa alihamia CDM na kundi kumbwa la wana CC hasa kutoka mbeya na kaskzini.
Masuala positive ya Lowassa CDM: aliwasaidia kuwapa mbinu za kuukama mfumo. Katika baadhi ya maeneo CC ndio walikuwa wanaulalamikia mfumo Kaskazini na kisiwani mombassa. Mombassa mfumo ulikamtwa na Ukawa kiasi kwamba katika baadhi ya vitu ukawa ilipata kura nyingi kuliko idadi ya waliojiandikisha. Kuna jimbo Kaskazini Mgombea wa CDM mwenye ushawishi alipata kikwazo cha kijinai kiasi cha kustahili jina lake kutopitishwa lakini kwa sababu mfumo ulikuwa umekamatwa na Lowassa alipita licha ya CC kupinga na hata kukata rufaa.
Athari hasi za Lowassa; aliua idiology ya CDM, aliua hoja za CDM na aliondolea uhalali wa CDM kuwa mtetezi wa wanyonge. Aidha, alisababisha baadhi ya wapenzi wake wapoteze mvuto wa kisiasa hadi leo. Athari hizo bado zinaiandama CDM leo. wanapata tabu kumeza matapishi.
kwa mtazamo wangu finyu: endapo CC wangemsimamisha Mmasai (MMeru) 2015 na CDM wangemsimamisha Mkaratu 2015, CDM wangeshinda, na endapo wangeshindwa na gap la kura lisingezidi 3% wangepata wabunge wengi zaidi na pangechimbika. Mkaratu alikuwa wa moto sana majukwaani na alikuwa na haiba ambayo wamama na baadhi ya CCM walikuwa wnaikubali. Naamini Mkaratu angetumia udhaifu wa MMeru kushindwa kujieleza na kuelemewa na kashfa za ufisadi kushinda uachuguzi huo.
Swali ni nani kwa sasa CDM sasa hivi ana mvuto aliokuwa nao Mkaratu?