John Mrema akanusha taarifa za kifo chake zilizoenea mtandaoni

John Mrema akanusha taarifa za kifo chake zilizoenea mtandaoni

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
13,203
Reaction score
23,027
Jamii ikifikia mahali watu wanahasimiana hadi kuombeana vifo na majanga, jee, hiyo jamii ipewe sifa gani? Mimi nitakuwa nimekosea kweli kuiita ni jamii ya watu wenye roho mbaya na unyama unyama?

The Tanzania I used to see and know under Mwalimu (RIP mzee wetu) is totally unrecognizable today!


Mkurugenzi wa mawasiliano chadema John Mrema kupitia mtandao wa Twita amekanusha taarifa zinazoenea katika mitandao mbali mbali zinazodai kuwa amefariki.

Kupitia video fupi John Mrema amesema "Leo nimepata taarifa za kustua zilizozusha kwamba mimi John Mrema nimefariki na nimeanza kupokea salamu za pole, wengine Watanzania wameenda nyumbani kwangu na wengine wakienda kijijini kwetu Moshi.

Nachopenda kuwathibitishia kuwa mimi siumwi, sijasafiri kwenda Afrika Kusini mara ya mwisho kwenda nje ya nchi ilikuwa mwaka jana mwezi wa kumi niko Dar ed Salaam nipo nyumbani kwangu najikinga na Corona."

Aidha, Mrema amesisitiza kuwa "inawezekana taarifa hizo zinazushwa kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazozua taharuki ndani ya nchi.

Hivyo, taifa lina haki ya kupewa taarifa sahihi na sio kuweka propaganda na uzushi kuzushiana vifo inaleta taharuki kwa ndugu jamaa na marafiki."
 
Ufipa hadi inafika 2025 watakuwa wanatafutana kwa tochi
 
Kwani kwazinduka mara ngapi ? Maana reporter wetu anasema ana tabia ya kuzinduka

Mwenyewe natamani niskie kuwa............ tena
 
Tutamzika shetani na kazi zake zote siku si nyingi, kila kitu kitakua sawa, Tanganyika yetu aliotuachia Nyerere itakua salama.
 
MATAGA kwasababu mjomba wenu yuko Nairobi mkaona na nyie mtafute kulipa kisasi, kama hayuko Nairobi mtoeni mliko mficha tumuone.
Subiri maiti kutoka Nairobi, hakuna mtu mle tena.
 
R.I. P Azory!

R.I.P kamanda Mawazo!

R.I. P Akwelina!

R.I.P Saanane!

R.I.P wapigania haki wote !
 
Baada ya watu duni wanaolipwa kusambaza taarifa za uongo za kifo cha Mkurugenzi wa Itifaki wa Chadema Mh John Mrema , Yeye Mwenyewe amejitokeza hadharani na kuthibitisha kwamba yuko hai na wala hana hata kikohozi wala mafua ya vumbi .

IMG_20210310_141952.jpg
 
Baada ya watu duni wanaolipwa kusambaza taarifa za uongo za kifo cha Mkurugenzi wa Itifaki wa Chadema Mh John Mrema , Yeye Mwenyewe amejitokeza hadharani na kuthibitisha kwamba yuko hai na wala hana hata kikohozi wala mafua ya vumbi .

View attachment 1721903
Ni vyema. Na wengine wanaozushiwa wajitokeze ili wazushi waumbuliwe.
 
uvccm wanazushia watu misala ili kupunguza kasi ya taharuki yao.. hakuna kinachodumu milele..mitano tena
 
Back
Top Bottom