Tetesi: John Mrema aliahidiwa "kutangazwa" mshindi Jimbo la Segerea

Ninachokataa mimi ni kile mtu/watu wakipingana na Mwenyekiti au na msimamo flani wa chama basi anaonekana msaliti ndani ya chama.
Naona hii dhana, mnaiendeleza hata Mbowe aliitumia sana.

Sio muda utasikia wamefukuzwa uanachama. 😁
Hao wanaliwa vichwa mapema tuu
 
Mtu akitofautiana mtazamo/msimamo na Mwenyekiti suluhisho ni kumfukuza?

Kuna kanuni gani wamevunja G55?
Vp yule mzee aliyefukuzwa ccm kuhoji maazimio ya 19 Jan DODOMA?
Huwez kupingana na maamuz uliyoshiriki kuyatengeneza mwenyewe
Unaona wenzako popoma kama wewe halafu wakuchekee tuu??
 
Ni kweli, watafukuzwa uanachama. Lakini hoja zao hazitajibiwa.
Kwa nn umjibu mtu aliye asisi kauli mbiu halafu anakuja kugeuka anataka apewe ufafanuz wakat yeye mwenyewe ndiyo alitengeneza

Dawa ni kuliwa kichwa tuu aende vyama vingine vipo vingi tuu aende nccr akaungane na yule popoma mwenzake shilling thelathini
 
Ninachokataa mimi ni kile mtu/watu wakipingana na Mwenyekiti au na msimamo flani wa chama basi anaonekana msaliti ndani ya chama.
Naona hii dhana, mnaiendeleza hata Mbowe aliitumia sana.

Sio muda utasikia wamefukuzwa uanachama. 😁
Hata ccm kupo hivyo. Ni kudhibiti wasaliti. Kama hukuweka hoja kikaoni kaa kimya ama kaa pembeni.
 
Shida ununuzi na ufadhili unatoka chama jirani,huku akitaka aendelee kukihudumia chama chake huku akikihujumu.
 
Mrema weeeee katika ubora wako
 
Sio kwa povu lile. Huyu Mheshimiwa atakua ameahidiwa kutangazwa mshindi kwenye matokeo ya uchafuzi hapo Oktoba 2025. Alindwe kwa gharama zote
 
Hiyo ndio demokrasia anayohibiri Lissu na genge lake la wahuni!
 
Vipi kuhusu CCM, Kuna mwanachama alienda mahakamani kupinga uteuzi wa wagombea nafasi ya Urais na Makamu wa Rais wa chama chake kuwa haukufuata katiba ya CCM. Una habari kashafukuzwa uanachama? Ukiwa unaleta hoja kuwa na references na usiwe biased.
 
Hata sisi CCM mtu akipinga agenda tunamfukuza sisi ni wakubwa kuliko chadema
 
Yule mzee aliyehoji maazimio ya Dodoma ilikuwaje?.
Usijitoe ufahamu kiasi hiki.
Huyu Chivundu ni tapeli, Mzee Godfrey Malisa kahoji kilichotokea Kamati ya CCM Januari Mwaka huu Dodoma alifukuzwa mara moja. Enzi za Magu walioimba 'tunaimani na Lowasa' wote wapata misukosuko ya hatari. Au CCM ni chama kidogo Cha siasa?
 
Njaa mbaya sana Mrema ulikua unakula kiulaini kiujanja ujanja saiv umeondolewa kwenye nafasi unapiga mayoee sana tulia tafuta kazi uishi kama unaona hutaki msimamo wa viongozi wenu hama njoo ccm uone kama utaropoka dhidi hata ya mkiti wa wilaya tunakufukuza haraka sana.
 
Mtu akitofautiana mtazamo/msimamo na Mwenyekiti suluhisho ni kumfukuza?

Kuna kanuni gani wamevunja G55?
Kanuni ya collective responsibility unaijua au huwa Unaisikiaga tu? Ukitaka kupinga maamuzi ya balaza ni Sharti kwanza ujiuzuru kabla ya chochote.
Tena si kufukuzwa, wamejifukuzisha wenyewe Kwa kanuni hiyo ya collective responsibility.
Muwe munaelewa mambo Kwa upana wake basi…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…