PreGE2025 John Mrema: CHADEMA 'imeuzwa' ndiyo maana tumeondoka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni sahihi kabisa
 
CHADEMA imepoteza muelekeo
 
Na wao watolewe Chaumma maana walikuwa CHADEMA...Yawezekana wanatumika kuiua CHAUMMA.
 
..harakati ndizo hutueleza wapi panapovuja, ili tupazibe. Wanaharakati ni watu wenye uzalendo.
sasa chadema ni chama cha harakati ama chama cha siasa, unajua tafaut ya siasa na harakati
 
sasa chadema ni chama cha harakati ama chama cha siasa, unajua tafaut ya siasa na harakati

..chama cha siasa kisipokuwa na wanaharakati kinageuka genge la kutafuta, au kung'ang'ania madaraka, kwa njia za kihalifu.

..wanaharakati ndio wanaokipa chama cha siasa DIRA YA KIMAADILI katika kufanya siasa na kuwatumikia wananchi.
 
Naomba kusaidiwa anamsemea nani huyo kuwa maisha yake kaishi ikulu na Lowasa alimpendekeza.
 
..sikubaliani naye.

..ukifuata anachosema chama kitaishia kumiliki magenge ya kuteka, kutesa, na kuua, ili kubaki kwenye madaraka.
tatizo umevamia siasa, unapofanya siasa kuna misingi na taratibu ndo maaana wanaharakati wanapokumbana mkono wa serikali mnalia
 
tatizo umevamia siasa, unapofanya siasa kuna misingi na taratibu ndo maaana wanaharakati wanapokumbana mkono wa serikali mnalia

..dola ndio wanavamia siasa kwa kutumwa na chama tawala.

..hebu niambie ni jambo gani ambalo wanaharakati wa Tanzania wamelipigania unaamini likitekelezwa lina madhara kwa nchi, hivyo kustahili wao kutekwa, kuteswa, na kuuwawa na vyombo vya dola.

..Kwa mfano, Mdude Nyagali alipendekeza jambo gani mbaya kiasi cha kuhalalisha kuuwawa kwake?
 
ndo maaana nmekuuliza unajua tafauti ya mwana harakati na mwanasiasa, ukasema hapana! kwahio maaana yake wewe ni mmoja wa mamluki, chama cha siasa lengo lake kuu ni KUSHIKA UONGOZI everything else mnafanya nje ya lengo hili ni kuvunja sheria, na mnakiangamiza chama mkidhan mnafanya kitu ambacho ni sahihi, sikiliza hio video vizuri tafakari alafu fanya kinachotakiwa kufanyika, unasajili chama cha siasa alafu ndan mnafanya harakati alafu mnaona mpo sahihi
 

..kitendo cha dola kupambana na wanaharakati nje ya mifumo ya kisheria tafsiri yake ni kwamba wenye matatizo ni dola sio wanaharakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…