PreGE2025 John Mrema: CHADEMA 'imeuzwa' ndiyo maana tumeondoka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mkurugenzi wa kurugenzi ya Habari na Taarifa kwa Umma wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), John Mrema amedai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 'kimeuzwa' kwa watu wasiokuwa na mizizi na uchungu wa chama hicho ambacho amekieleza kukosa mwelekeo.

Mrema ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya Jumatano Juni 04, 2025, Mjini Musoma mkoani Mara katika mwendelezo wa Operesheni ya CHAUMMA For Change (C4C).

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Chama chenu leo kimekabidhiwa kwa mtu aliyeishi Ikulu maisha yake yote mpaka alipostaafu, akajiunga nacho 2015, Edward Lowassa akampendekeza awe mbunge, wenzake wawili walisharudi CCM, yeye kumbe alibaki kimkakati, leo kakabidhiwa CHADEMA, ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, halafu mnasema chama hakijauzwa, nendeni mtafakari", ameeleza Mrema.

Chadema sio chama tawala, hili kenge si lisumbuke na ccm!! Au ndio limepata trauma syndrome
 
..dola ndio wanavamia siasa kwa kutumwa na chama tawala.

..hebu niambie ni jambo gani ambalo wanaharakati wa Tanzania wamelipigania unaamini likitekelezwa lina madhara kwa nchi, hivyo kustahili wao kutekwa, kuteswa, na kuuwawa na vyombo vya dola.

..Kwa mfano, Mdude Nyagali alipendekeza jambo gani mbaya kiasi cha kuhalalisha kuuwawa kwake?
Kinachonisikitisha ni kuwa vyama vya upinzani vinaweka juhudi kubwa kuchafuana na kutukanana kuliko wanazoweka katika kuibana serikali kuhusu mambo ya utekaji na mauaji yanayoelekea kukithiri nchini. Suala la Mdude, Mzee Kibao, Soka na wengine kama hao linatakiwa kuwa suala la vyama vyote vya siasa bila kujali itikadi zao. Vyama kama ACT-WAZALENDO, Chadema, Chaumma, CUF vinatakiwa kupaza sauti zaidi ya wanavyofanya sasa hivi. Hata CCM wanapaswa kupiga kelele.

Amandla...
 
..watu wazima wanapaswa kuwakalisha kitako Chadema na Chaumma na kuwanasihi waache kuchafuana.

..John Heche alikosea kumsema vibaya Mama Susan Kiwanga.

..John Mrema alikosea kumsema vibaya Mama Ruth Mollel.
 
Kabisa. Sijui Heche alisema nini lakini sikufurahia John mwenzake alivyomsema Ruth Mollel. Mama Kiwanga na Mama Mollel wanastahili heshima kwa mchango wao kwa taifa letu.

Amandla...
 
John Heche anambeza Suzan Kiwanga kuwa alikuwa mama wa ndani ( sijui alikuwa anamaanisha kuwa house wife au house girl). Kuwa hajasoma. Kuwa alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga.Hana shukrani kwa kupewa ubunge na CDM. Bibi Titi Mohamed hakwenda shule lakini alitoa mchango mkubwa mno katika ukombozi wa nchi hii. Mtu kama Suzan kama ilivyokuwa kwa Bibi Titi anastahili pongezi na sio kubezwa.

Suzan Kiwanga ni mfano wa sehemu kubwa ya wananchi. Kumbeza yeye ni kuwabeza wanawake wengi wa nchi hii. Sehemu kubwa ya wanaojaa katika mikutano ya vyama vya upinzani ni wanawake kama Suzan Kiwanga.
Wakina mama wa nyumbani, hawajaenda shule sana, wana kipato kidogo. Sio busara kuwabeza.

Suzan Kiwanga alishinda uchaguzi hakupewa fadhila. Suzan Kiwanga amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu kutokana na mchango wake kwa chama na sio kwa sababu ya fadhila. Hivyo hivyo Ruth Mollel amechaguliwa kuwa Trustee kutokana na uwezo wake na sio kingine.

Amandla....
 
John Heche anambeza Suzan Kiwanga kuwa alikuwa mama wa ndani ( sijui alikuwa anamaanisha kuwa house wife au house girl). Kuwa hajasoma. Kuwa alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga.Hana shukrani kwa kupewa ubunge na CDM. Bibi Titi Mohamed hakwenda shule lakini alitoa mchango mkubwa mno katika ukombozi wa nchi hii. Mtu kama Suzan kama ilivyokuwa kwa Bibi Titi anastahili pongezi na sio kubezwa.

Suzan Kiwanga ni mfano wa sehemu kubwa ya wananchi. Kumbeza yeye ni kuwabeza wanawake wengi wa nchi hii. Sehemu kubwa ya wanaojaa katika mikutano ya vyama vya upinzani ni wanawake kama Suzan Kiwanga.

Wakina mama wa nyumbani, hawajaenda shule sana, wana kipato kidogo. Sio busara kuwabeza. Suzan Kiwanga alishinda uchaguzi hakupewa fadhila. Suzan Kiwanga amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu kutokana na mchango wake kwa chama na sio kwa sababu ya fadhila. Hivyo hivyo Ruth Mollel amechaguliwa kuwa Trustee kutokana na uwezo wake na sio kingine.

Amandla....
Ukiwa mpumbavu utasemwa tuu ,bila kujali ulikuwa nani, upumbavu hauwezi kufichwa kwa ajili ya mema , utasemwa kwa upumbavu na utasifiwa kwa mazuri yako
 
Mara nyingi watu wanaopenda kuwaita wenzao wapumbavu wao ni wapumbavu zaidi.

Amandla...
 
..kitendo cha dola kupambana na wanaharakati nje ya mifumo ya kisheria tafsiri yake ni kwamba wenye matatizo ni dola sio wanaharakati.
nyie mnapambana na dola ama ccm? alafu wanaharakati sio watu wa vurugu
 
Ad Hominem attacks.

Ndio silaha kubwa ya CHAAWA wa CHADEMA.

Wamekengemaa kweli na kumchafua John.
 
nyie mnapambana na dola ama ccm? alafu wanaharakati sio watu wa vurugu

..Ccm badala ya kujibu hoja za wanaharakati, au kuzifanyia kazi, inatumia vyombo vya dola, na mahakama, kuwashambulia wanaharakati.
 
Ruth Mollel alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi. Nadhani amewahi kuwa Mkurugenzi au Kamishna wa Utumishi. Ni mbobezi katika masuala ya Utumishi wa Umma. Alistaafu 2011 na kujiunga na Chadema 2015. Sijawahi kusikia scandal zozote juu yake akiwa Mtumishi wa Umma. Ana umri wa miaka 74.

Sasa Mrema anaposema ameuziwa Chadema anamaanisha nini? Kuwa ametoa pesa kwa Chadema ili aongoze ajenda zake? Kusema hivyo ni upuuzi wa hali ya juu. Mrema anapaswa kumuomba msamaha.

Aidha, hivi vyama vya siasa vinatakiwa viwe vinapitia hotuba za viongozi wao kabla hawajizoa jukwaani.

Amandla...
 
Mkurugenzi wa kurugenzi ya Habari na Taarifa kwa Umma wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), John Mrema amedai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 'kimeuzwa' kwa watu wasiokuwa na mizizi na uchungu wa chama hicho ambacho amekieleza kukosa mwelekeo.

Mrema ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya Jumatano Juni 04, 2025, Mjini Musoma mkoani Mara katika mwendelezo wa Operesheni ya CHAUMMA For Change (C4C).

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Chama chenu leo kimekabidhiwa kwa mtu aliyeishi Ikulu maisha yake yote mpaka alipostaafu, akajiunga nacho 2015, Edward Lowassa akampendekeza awe mbunge, wenzake wawili walisharudi CCM, yeye kumbe alibaki kimkakati, leo kakabidhiwa CHADEMA, ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, halafu mnasema chama hakijauzwa, nendeni mtafakari", ameeleza Mrema.

Wajinga jinga Chadema haiko madarakani🤦🏾‍♂️
 
..Ccm badala ya kujibu hoja za wanaharakati, au kuzifanyia kazi, inatumia vyombo vya dola, na mahakama, kuwashambulia wanaharakati.
basi endeeleni kupambana sku mtaelewa tafauti ya harakati na siasa mtuambiie
 
Ruth Mollel alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi. Nadhani amewahi kuwa Mkurugenzi au Kamishna wa Utumishi. Ni mbobezi katika masuala ya Utumishi wa Umma. Alistaafu 2011 na kujiunga na Chadema 2015. Sijawahi kusikia scandal zozote juu yake akiwa Mtumishi wa Umma. Ana umri wa miaka 74.

Sasa Mrema anaposema ameuziwa Chadema anamaanisha nini? Kuwa ametoa pesa kwa Chadema ili aongoze ajenda zake? Kusema hivyo ni upuuzi wa hali ya juu. Mrema anapaswa kumuomba msamaha.

Aidha, hivi vyama vya siasa vinatakiwa viwe vinapitia hotuba za viongozi wao kabla hawajizoa jukwaani.

Amandla...

..hili la HOTUBA ni muhimu sana.

..viongozi wa vyama vya siasa sidhani kama wanafanya maandalizi yoyote kabla ya kutoa hotuba.

..pia sidhani kama wanafanya tathmini yoyote ile baada ya kuzungumza majukwaani.

..Nawashauri Chadema waandae hotuba zao vizuri zaidi, pia wafanye tathmini baada ya hotuba hizo ili kuboresha ujumbe wanaopeleka kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom