Nakupa taarifa sahihi na siyo porojo za mitandaoni.
Bonna Kamoli akishinda segerea itakuwa ni moja ya maajabu hapa duniani.
Mrema anafanya kampeni, ila kampeni za sasa hivi kwa ngazi za udiwani na ubunge majukwaani unapoteza muda tu.
Kampeni zinafanyika kwa kuyafikia makundi maalum, vyama vya hiyari, timi za mpira mitaani, vicoba and likes.
Ukimya mnaouna ni ukata wa pesa, wagombea hawana pesa.
Bonna hatopigiwa kura na wanaccm wengi sana, hakubaliki kabisa amini ninachokwambia, kwenye kura za maoni alipita kwa kuhonga mpaka laki tatu kuna wajumbe watata walivuta.
Bonna akipewa tena ubunge kwa njia yoyote ile ni majuto kwa wanasegerea wote, ametumia pesa nyingi sana mpaka dakika hii, mtu wa aina akitangazwa mshindi ndio mmemalizana hamtoonana tena atakuwa bize kurudisha pesa alizotumia kuhonga.
Jimbo la Segerea halihitaji kelele nyingi tayari watu wana maamuzi yao wakiwemo wana ccm wengi tu.