PreGE2025 John Mrema: Kampeni yetu ya tone tone mpaka sasa imefikisha shilingi ngapi? Viongozi hawana cha kusema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tonetone ni michango inayoendelea, aseme ya join the chain ilikuwa ngapi?
 
Tunafahamu fika wewe na Mwenyekiti wenu Mbowe mlikuwa wanufaika wakubwa wa pesa za Sa100 kutoka Serikalini na ndiyo maana mnalialia sasa hivi zile pesa chini ya uongozi wa Lisu hazipo tena, inafahamika kuwa wazi kuwa pesa lazima iwe ngumu maana Lisu hayupo tiyari kupokea pesa za hongo.


Tulieni Chama kijijenge upya , mwanzo siku zote mgumu lakini Bora kuwa na Upinzani wa kweli usio kuwa na pesa kuliko kuwa na Chama pinzani kinachojikomba na kuwatengenezea njia Chama tawala miaka nenda Rudi.
 
Piteni hivi mkaanzishe chama chenu,aliondoka slaa na chama kipo hadi leo sembuse nyie.Mngefanya haraka kuondoka msijekosa nafasi kwenye vyama vingine.
 
John Mrema kafuge kuku, nguruwe, kalime hata nyanya fedha za bure wakati wake umepita
 
Hizi ni athari za chama ama kiongozi kukaa madarakani muda mrefu. Siku anatolewa bila kuwa tayari, waliokuwa wanafaidika kupitia madaraka yake, lazima waanzishe tafrani.

Cdm chini ya Lisu wasichukue zaidi ya mwaka kabla hawajafanya mabadiliko ya katiba. Asiwepo yoyote na kwa nafasi yoyote kukaa zaidi ya miaka kumi kwenye nafasi moja ya kuchaguliwa. Hii itasababisha chama kuendeshwa kitaasisi na sio utashi wa mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…