Huyu aligombea ubunge 2010 vunjo kupitia Chadema na kushindwa na hayati Agustino lyatonga Mrema, hivyo Mh.Freeman Mbowe akamwajiri Makao makuu kama Mkurugenzi wa masuala ya bunge maanak alikuwa ndo kamaliza chuo ajira Hana ila Mbowe alimwona ni asset huko mbeleni...! 2015 alikuwa ndio kama kiongozi wa Kampeni akiongozana na Lowassa sehemu mbalimbali za nchi pia alikuwa ndo Mc shughuli za ufunguzi wa Kampeni...! Baadaye akawa ndo Mkurugenzi wa itifaki,mawasiliano na habari...! Mwaka 2020 alishindwa vibaya kwenye kura za maoni Jimbo la segerea ...! Lakini akarudishwa kugombea na Chama lakini kwenye uchaguzi alishindwa vibaya na Bonna Kaluwa...!
Hawa ni vijana wachache akiwemo ezekia wenje, munisi na nk ambao walikuwa karibu na mwenyekiti mstaafu Mh Mbowe, pia wamefaidi sana Ruzuku pale Makao makuu ambapo wanachama wengi wamekuwa wakilalamika ruzuku kuishia Makao makuu, na kashfa nyingi kama kupokea hongo na rushwa ili kuweza kupata nafasi ya ubunge hasa viti maalumu...ambapo yamekuwa malalamiko ya wanachama wengi
Mwenyekiti mpya aliyeingia atakuwa mwiba mchungu kwake maanak Mh Tundu lissu lazima aweke Timu ya ushindi, hapendi rushwa na matumizi mabaya ya Ruzuku...! Na pia ameumia swahiba wake Mh Mbowe na ezekia wenje kuangushwa