PreGE2025 John Mrema: Kuzuia uchaguzi ni kufanya Jinai, njia ya No Election si sahihi

PreGE2025 John Mrema: Kuzuia uchaguzi ni kufanya Jinai, njia ya No Election si sahihi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA John Mrema amesema iwapo chama hicho kitatekeleza mpango wake wa kuzuia uchaguzi bila kushirikia itakuwa ni sawa na kufanya jinai.

Mrema amesema hayo leo April 06, 2025 akizungumza na wanahabari juu ya waraka ulioandikwa na kundi la G-55 ambalo ni wagombea ubunge 2020 na watiania wa ubunge wa chama hicho kwa mwaka 2025 ulioandikwa kwenda kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika.

“kwenye no election njia ambayo chama imetumia tunaona sio sahihi…tunaona hatuwezi kuzuia uchaguzi kwa kuwa nje ya uchaguzi, kujaribu kuzuia uchaguzi huku ukiwa nje itakuwa ni sawa na kufanya jinai”

Mrema amefafanua njia pekee inayoaminiwa na kundi hilo ya kuzuia uchaguzi ni kushiriki kwenye uchaguzi ili wawatumie wagombea kushawishi wananchi kuzuia uchaguzi katika vituo vya uchaguzi.

View attachment 3294783
Hii simbilisi toka ipigwe chini pale Chadema HQ imepauka kweli kweli
 
Aisee huyu jamaa anajisikia anachokiongea?? Yaani anaongelea kuhusu kupiga kura huku akimaanisha ndio uchaguzi!! Ilikuwaje kuwaje akaweza kuwa Mkurugenzi kabisa kama uelewa wake kuhusu uchaguzi ndio upo hivyo?😀
 
Mentality ya John Mrema na wenzake ni kutaka kugombea ubunge ili Tume ya CCM labda iwaonee huruma na kuwarushia viti vichache vya Ubunge na maisha yasonge!

Magufuli alishaonesha ubovu wa mfumo wetu wa uchaguzi na bila aibu akapora viti vyote kasoro kimoja tu kule Nkasi. Mama Samia naye kafanya hivyohivyo juzi kati hapa baada ya kujua Watanzania wengi sana ni wajinga, na hatutamfanya kitu!

Ni ujuha, upumbavu na ubabaishaji kung’ang’ania kuingia kwenye uchaguzi katika mazingira yaleyale huku ukitegemea matokeo tofauti. Na hii ndio definition halisi ya madness!
 
John Mrema G55 ni kiongozi makini sana, mwenye uwezo wa kujenga hoja. hoja zake zinalenga kukijenga chama. Mwenyekiti anataka kukiuwa chama. Chadema asilia wameshtuka.
 
huyi jamaa mkewe si ni kati ya wale covid-19, naona anatikisa mboga
 
Tatizo TAL anaongea lakini field haonekani ,akiambiwa anataka akamatwe anakimbia nchi....inatakiwa apambane afungwe kama mbowe ndiyo tutaona kweli ana dhamira.
 
Acha uongo, Mbowe alipigwa kwenye uchaguzi hadharani na akakubali. Kwa maana nyingine Mbowe alistaafishwa siasa na Lissu. Kwa hivyo hakuna Cha CHADEMA ya Mbowe.
Hakuna asiyejua hilo,ila wote waliomuunga mikono ndiyo wanaonekana waasi.......kama huo ufa huoni kama ni Lissu vs Mbowe utakuwa na mtindio wa ubongo
 
Back
Top Bottom