John Mrema: Polisi alimwambia Mbowe "This time huchomoi tunakupa kesi ya Ugaidi"

John Mrema: Polisi alimwambia Mbowe "This time huchomoi tunakupa kesi ya Ugaidi"

Wanamkomoa kesi iende miaka mingi upuuzi tu hakuna lingine....mama anaupiga mwingi
 
Huyo Mrema alikuwepo wakati hayo maneno yakisemwa?! Viongozi ni muhimu kujihadhari na maneno yanayoweza chochea chuki za namna yoyote.
Kwani yule aliemwambia kuwa hatashinda ubunge wa Jimbo la Hai alikuwa Polisi wa nchi gani?

Hivi mnafikir hao Polisi wana sifa za kulinda usalama wa raia na mali zao?
 
Kwan boss wa RC Ni Nani? Na mbona mawaziri wanatoa maagizo same time Rais
Lazima ujue maana ya channel of command haiwezekani Rais wa Jamhuri ya Muungano akampigia directly RPC simu na kumpa maagizo. Kuna vyombo vingi vya usalama vinafanya kazi na makamanda wa Polisi. Na hiyo kauli ya Mrema ni propoganda dhidi ya kamanda wa Kinondoni tusubiri mambo yote yatajulikana mahakamani
 
Hata Sabaya aliambiwa na Mbowe safari hii ataozea jela.

Lakini sasa wote watakutana Kisongo
Naona wakikutana zipigwe kwanza tuone nani mwenye ubavu humo kisongo
 
Askofu Benson Lwakalinda Bagonza (PhD) Ameandika:

KABLA YA KATIBA MPYA...

1. Kabla ya Katiba Mpya ya Afrika ya Kusini, Nelson Mandela aliitwa gaidi.

2. Kabla ya "Katiba Mpya" iliyoandikiwa Lancaster, Julius Nyerere alikuwa ni Mchochezi aliyekuwa nje ya gereza kwa kulipa faini.

3. Kabla ya Agano Jipya (Katiba Mpya), Musa alikuwa ni gaidi machoni pa Farao (Firauni).

4. Kabla ya ufufuko (Katiba Mpya) Bwana Yesu Kristo alikuwa na tuhuma za ugaidi na uhaini mbele ya utawala wa Kiyahudi.

5. Kabla ya Muswada ulioleta "Tamko la Haki kwa wote" (Katiba Mpya) huko Marekani, Mwanamke na mtu mweusi kudai kupiga kura ilikuwa ni kitendo cha ugaidi.

6. Kabla ya SUK huko Zanzibar, hayati Maalim Seif alikuwa gaidi, kibaraka wa Usultani na mtuhumiwa wa uhaini.

7. Kabla ya CCM Mpya ("Katiba Mpya"), Waitara, Prof Mkumbo, Mollel, Gekul, Katambi, Silinde, Kafulila, hayati Mgwira nk walikuwa vibaraka wa ubeberu na sasa ni wazalendo.

8.Kabla ya msiba wa kitaifa (Katiba Mpya), Mama SSH alikuwa ni Mshauri wa Rais (Asiyelazimisha ushauri wake), Sasa ni Mshauriwa (Asiyelazimishwa na washauri).

Tunajifunza Nini?

A. Ugaidi ni dhana na silaha ya mtawala dhidi ya mtawaliwa.

B. Muda ndio mwamuzi wa kweli na WA haki.

C. Watawaliwa huteseka; watawala hujuta.

D. Bora mateso kuliko majuto.

E. Katika harakati za kupata madaraka, kila aliyewahi kutawala aliwahi kuonekana ni gaidi mbele ya anaoshindana nao. Hata ndani ya CCM "Magaidi" ni wengi dhidi ya SSH.

Wanaomtuhumu Mbowe kuwa gaidi leo, watakuwa Magaidi wa mfumo wakati ujao.
 
Lazima ujue maana ya channel of command haiwezekani Rais wa Jamhuri ya Muungano akampigia directly RPC simu na kumpa maagizo. Kuna vyombo vingi vya usalama vinafanya kazi na makamanda wa Polisi. Na hiyo kauli ya Mrema ni propoganda dhidi ya kamanda wa Kinondoni tusubiri mambo yote yatajulikana mahakamani
Upo sahihi,

Je,kwann RAIS hutoa maagizo kwa MA RC bila kupitia kwa mawaziri?

Hiyo chain of command unayoisema Ni ipi?
 
Mkurugenzi wa uenezi na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Mbowe kufikishwa Dar kutokea Mwanza, Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, ACP Ramadhani Kingai alimwambia:

"This time huchomoki, tunakupa kesi ya ugaidi"

Mrema ameyasema hayo katika bunge la wananchi linalofanyika kupitia Space!

Ni maneno ya ndugu Jonh Mrema, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa CHADEMA.

Nini maoni yako?
Chadema kwa kutunga uongo na kupotosha hamjambo.
 
Upo sahihi,

Je,kwann RAIS hutoa maagizo kwa MA RC bila kupitia kwa mawaziri?

Hiyo chain of command unayoisema Ni ipi?
Ma RC ni wateuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Makamanda wa Polisi wa Mikoa ni wateule wa IGP. Ndio maana Rais huongea direct na Ma RC
 
Kwani yule aliemwambia kuwa hatashinda ubunge wa Jimbo la Hai alikuwa Polisi wa nchi gani?

Hivi mnafikir hao Polisi wana sifa za kulinda usalama wa raia na mali zao?
Yule tulimwona kwa ushahidi wa video. Na wenye kuitakia mema nchi yetu tulikemea hadharani,humu humu jukwaani.
Sasa huyu Mrema yeye ameyashuhudia hayo yakitamkwa?! Huo ndo msingi wa hoja yangu.
 
Huyo Mrema alikuwepo wakati hayo maneno yakisemwa?! Viongozi ni muhimu kujihadhari na maneno yanayoweza chochea chuki za namna yoyote.
We kenge kumbuka CDM wana mtandao mkali!
Hata waliokuwepo pale (askari) huwa wanaleta hayo maneno 'uraiani'
 
Anyway, hizo ndio sifa za shetani na shetani hajawahi kushinda nguvu za Mungu (wenye haki)
 
Back
Top Bottom