TANZIA John Nyerere afariki dunia

TANZIA John Nyerere afariki dunia

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2008
Posts
3,007
Reaction score
2,451
John Nyerere, mtoto wa nne wa Mwalimu Julius Nyerere, amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili.

MAMIA ya wakazi wa Dar es Salaam leo wanatarajia kutoa heshima za mwisho kwa John Nyerere (58), ambaye ni mmoja wa watoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

John alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikokuwa amelazwa.Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto mwingine wa Mwalimu Nyerere, alisema Dar es Salaam jana kuwa mwili wa John utasafirishwa kesho kwenda Mwanza na kisha kupelekwa kijijini kwao Butiama Mkoa wa Mara kwa maziko.

"Misa ya kumuombea John itafanyikahapa Msasani nyumbani kwa Mwalimu na kufuatiwa na utoaji wa heshima za mwisho," alisema Makongoro, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

John alitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na alishiriki Vita vya Kagera vya 1978 na 1979, vilivyolenga kumng'oa nduli Iddi Amin wa Uganda.

Watoto wengine wa Mwalimu ni Andrew, Magige, Madaraka, Anna na Rose.


Chanzo:
Habari Leo
Kapteni John Nyerere atakumbukuwa sana na wana anga wa jeshi kutokana na umahiri wake wa kumudu ndege za kivita wakati wa ujana wake.
========================

UPDATES;

Ratiba ya Mazishi
attachment.php
 

Attachments

  • ratiba.png
    ratiba.png
    146.1 KB · Views: 9,485
Back
Top Bottom