TANZIA John Nyerere afariki dunia

TANZIA John Nyerere afariki dunia

Mbowe,Mrema,Lipumba.SEIF shariff hamad,na viongozi wa kibao wa upinzani wanatibiwa nje ya nchi wote nao mafisadi kwa gharama za serikali nao mafisadi? Au hujui kuwa huwa wanaenda nje kutibiwa na kupima afya zao?
dogo umekurupuka , nisome tena , asilimia 95 ya viongozi wa ccm wanaumwa na wengine wanagombea uongozi si kwa ajili ya kuleta maendeleo bali wapate uchochoro wa kutibiwa nje , maana wanaumwa ! inahitaji zaidi ya macho uliyonayo kunielewa .
 
Poleni sana Familia ya Maam Maria Nyerere.
 
R.I.P. mtoto wa Nyerere, hivi hakuna namna nyingine ya kumtambulisha mtu mwenye watoto na wajukuu zaidi ya kuitwa mtoto wa fulani.?

Ni mtazamo tu.

UKo Sahihi Sana Mkuu Na Naungana Na Wewe Kwa 100% Kwa Mfano Mbona Mimi Sipendi Niitwe Mtoto Wa ..............Bali Napenda Tu Niitwe Mr. Gentamycine Mathematician. Mamlaka Ya Baba Yangu Na Cheo Cha Mzee Hakihusiani Na Mimi Na Huwa NAKASIRIKA Mno Hadi KUCHUKIA Mijitu Ikiniita Wewe Mtoto Wa Nanihii Hujambo? Mzee Alifanya Yake Mpaka Akawa Hivi ILA Na Mimi Pia Sasa Nataka Nifanye Mambo Mema Kwa Tanzania Nami Niheshimike Mimi Kama Mimi Na Siyo Kwa MBELEKO Ya Mshua. Mkuu Umenikuna Mno Kwa Post Yako Hii Na Sina Mashaka Na Uwezo Wako Mkubwa Wa Kufikiri Na Nimekukubali Sana.
 
Mtoto wa muasisi wa Taifa anafia Muhimbili wakati walugaluga wengine wasio hata na chembe ya mchango chanya na nchi wanapelekwa nje ya nchi, SHAME KWA WALIOPASWA KUMTIBU NA KUMPATIA TIBA STAHIKI:
 
Pole Kamanda,kipindi cha nyuma kidogo niliwahi kukuuliza kuhusu hili na hukunijubu,lakini naona umeleta jibu wakati huu ambao siyo wakati muhafaka,kwa mtazamo kama Yericko anapenda kujiita jina hilo naona tumpe nafasi afanye hivyo labda analilia kazi alizofanya baba yako,nakushauri usiendelee na mjadala dhaifu kama huu kwani hautusaidii tena hapa tulipofika,hata mimi kesho naweza kujiita Rosemary Nyerere ili tu kukumbuka kazi za baba yako!

Rose umetumia busara na hekima ya hali ya juu sana kumjibu hivyo huyu bwana.Ni kweli mtu anaweza kufurahia kazi, matendo, na hata uongozi wa mwingine hadi kufikia kukubali kuacha kutumia ubini wake na kuutumia wa yule anaempenda na hata kutaka kuongea kama yeye. Hayo ni mapenzi mema ya kumpenda mtu. Pia huweza kum-badili toka tabia mbaya aliyokuwa nayo awali na kuwa na tabia nzuri kama ya yule anaemwamini na hatafanya ovu lolote kwa jamii wala familia ya alieasili jina lake Hapo kuna ubaya gani? Wala hujamsikia Yeriiko akigombea uongozi wowote kwenye familia ya mar. Nyerere wala kudai sehemu ya haki kama mtoto wa marehemu. Familia yote inaelewa pamoja na wana ukoo wote wanaelewa yupo mtu ajulikanae kama Yeriko anatumia jina la ukoo wa Nyerere vizuri na hajawahi kulitumia vibaya tatizo lipo wapi? Wewe ulipokwenda kumhoji mzee Butiku ulitumwa na familia ya mwalimu? Kwa mara nyingine tena heko Rozi na hoja hiyo iishie hapo.
 
Mwana jf mwenzetu Andrew, poleni sana kwa msiba huu mkubwa na nadhani ndio wa kwanza kwa mtoto wa Mwalimu!.

Kusema ukweli baadhi ya wanafamilia wa Baba wa Taifa wako too low profile kiasi licha ya mimi kukulia jirani na Pale Msasani huku tukisoma darasa moja na Milton sikuwahi kusikia lolote kumhusu John zaidi ya kusikia alikuwa na cheo cha Capt. wa JWTZ na alikuwa ni fighter pilot wa Jet.

RIP Capt. John Magige Nyerere.

Pasco

Kumbe Magige ndio John! Nilikuwa sijapata picha.
R.I.P Magige
 
Poleni sana familia ya Nyerere, John alikuwa rafiki wa wote hata watoto wadogo walimpenda John. Binafsi alinifundisha karate katika viwanja vya Ikulu nikiwa kijana mdogo sana. Sina mengi sana ya kusema zaidi ya kukuombea pumziko jema la milele pia nakupa pole Petro rafiki yangu wa utotoni kwa kufiwa na baba yako mzazi
 
Back
Top Bottom