John Samwel Malecela alitoka kwenye Uwaziri Mkuu akawa Mbunge wa kawaida

John Samwel Malecela alitoka kwenye Uwaziri Mkuu akawa Mbunge wa kawaida

Kugombea ni haki yake na hakuna cha ajabu.

Achana na John Samwel Malecela.

Hata John Quincy Adams rais wa Marekani alipostaafu alirudi kuwa Congressman.

Lakini pia kuna maswali mengi kama vile, hawa watu wengine hawatosheki na uongozi? Hawachoki? Hawawaandai watu wengine kuongoza?

Is this really about getting the best leadership or their own egos?

Kuna uzi umewekwa hapa Salma Kikwete kasema kaambiwa na wananchi ubunge ni wake mpaka achoke mwenyewe.

Hawana hata aibu?

Hawajui kufurahia maisha ya kustaafu na kucheza na wajukuu?

Huu si utumwa wa aina fulani huu? Uraibu wa vyeo na power?
Mtu kama Salma inafikirisha sana kwanini aendelee kutaka Ubunge very interesting Mkuu

Yule kwasasa ilipaswa awe na ka NGO tu kakina mama uko na Kufanya Community activities za hapa na Pale kuliko izo heka heka za Ubunge

Kwanza Mume wake Tayari ni Rais mstaafu na bado ana influence na Mambo mengi nchi hii sasa inashangaza kweli former first lady Kulilia ubunge bado

Lakini all in all ndio mambo ya diversity hayo we should embrace it
 
Naona umesahau Bro. Malecela alikuwa Balozi wetu London akaitwa na Rais Mwinyi awe Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais. Hii ilikuwa kujaza nafasi ya Joseph Sinde Warioba aliyefukuzwa na Boss wake Rais Mwinyi kwa kosa la kutowajibika na kuwa legelega. Nchi ni kweli kabisa ilikosa mwelekeo ubadhirifu na magendo yakashimiri huku Waziri Mkuu akiyumbayumba tu. Malecela alienda hadi akamaliza awamu yake. Nashangaa CHADEMA kumshabikia mtu ambaye Rais Mwinyi alimfukuza kwa fagio la chuma.
 
Kuna kitu kinaitwa "status anxiety". Watu wana anxiwty na status, kuipata, kui maintain, kutoipoteza.

Yani wanakuwa focused na hiyo anxiety, mpaka wanakuwa hawajui kuwa mtu akishakaa Ikulu kama First Lady kurudi kwenye ubunge ni kushuka daraja.

Yani mtu kapenyapenya mpaka kawa Rais wa nchi. Cheo kikubwa sana ambacho nchini kwetu ni watu sita tu wamewahi kukipata.

Halafu bado mtu anaona cheo hicho hakitoshi anaenda kukonbeleza PhD za heshima na kutaka na yeye aitwe Dr., as if urais si distibction ya kutosha.

Famikia moja baba kawa rais, mama mbunge, mtoto waziri.

Huko kwingine nasikia John Samwel Malecela anamrithisha dogo Samwel John Malecela ubunge, tumekataa uchifu na vyeo vya kurithishana halafu tunakubali ujinga huu.

Kina Magifuli nao wanajiandaa ubunge, kwa kuwa baba yao alikuwa rais tu.

Zanzibar imekuwa na marais wawili wa kurithishana.

Nepotism all over the place.
 
Tujikumbushe wakuu…

John Samwel Malecela aliwahi kuwa Waziri Mkuu kisha baadae alipoukosa u-PM akawa Mbunge wa kawaida mpaka pale alipostaafu na kumuachia Kibajaj jimbo la Mtera.

Kwahiyo hakuna jipya wala msishangae mkimuona PM wa sasa anasema atagombea tena Ubunge.

Lolote linaweza kutokea…
Siyo huyo huyo aliyebwagwa na Kibajaji Lusinde; mmoja wa wabunge wa hovyo kabisa kutokea ndani ya taifa hili tokea uhuru?
 
Waziri mkuu pekee anayeheshimiwa sana na wana CCM nchi nzima na watanzania ni Mizengo Pinda tu peke yake
Ndio waziri mkuu mstaafu pekee Tanzania anayejua maana ya kustaafu uwaziri mkuu
Hata anapoona nchi innajisiwa, yeye hana dogo la kusema? Huyo ni kama marehemu, hayupo tena kwenye nchi aliyoitumikia.
Mtu pekee anayebeba heshima hiyo ni Joseph Sinde Warioba kwa sasa hivi. Hakuna mwingine.
 
John Samwel Malecela aliwahi kuwa Waziri Mkuu kisha baadae alipoukosa u-PM akawa Mbunge wa kawaida mpaka pale alipostaafu na kumuachia Kibajaj jimbo la Mter
Unakumbusha jambo usilo lifahamu, au unapotosha maksudi? John Malicela alibwagwa na Kibajaji Lusinde.
Hakuna kitu cha kujivunjia heshima kinachofanana na jambo hilo!
 
Acha uongo Malecela hajastaafu jimbo la mtera,bali aliangushwa kura za maoni na huyo " kibajaji"
Jitafunze kutafiti kabla ya kuongea
Huo ni mchezo tu, janja.

Tafuta uhusiano uliopo kati ya Malecela na Kibajaj
 
Naona umesahau Bro. Malecela alikuwa Balozi wetu London akaitwa na Rais Mwinyi awe Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais. Hii ilikuwa kujaza nafasi ya Joseph Sinde Warioba aliyefukuzwa na Boss wake Rais Mwinyi kwa kosa la kutowajibika na kuwa legelega. Nchi ni kweli kabisa ilikosa mwelekeo ubadhirifu na magendo yakashimiri huku Waziri Mkuu akiyumbayumba tu. Malecela alienda hadi akamaliza awamu yake. Nashangaa CHADEMA kumshabikia mtu ambaye Rais Mwinyi alimfukuza kwa fagio la chuma.
Janja wewe ndio umesahau!

Malecela hakumaliza kipindi chake aliliwa kichwa na Msuya akapewa tena U-PM mwaka 1994 mpaka 1995
 
Naona umesahau Bro. Malecela alikuwa Balozi wetu London akaitwa na Rais Mwinyi awe Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais. Hii ilikuwa kujaza nafasi ya Joseph Sinde Warioba aliyefukuzwa na Boss wake Rais Mwinyi kwa kosa la kutowajibika na kuwa legelega. Nchi ni kweli kabisa ilikosa mwelekeo ubadhirifu na magendo yakashimiri huku Waziri Mkuu akiyumbayumba tu. Malecela alienda hadi akamaliza awamu yake. Nashangaa CHADEMA kumshabikia mtu ambaye Rais Mwinyi alimfukuza kwa fagio la chuma.
Malicela aliondolewa akachukua Msuya mpka uchaguzi mkuu 1995
 
Back
Top Bottom