Jokate Mwegelo kubeba mimba bila ndoa katika Utumishi inatoa taswira gani kwa unaowaongoza?

Jokate Mwegelo kubeba mimba bila ndoa katika Utumishi inatoa taswira gani kwa unaowaongoza?

Katika utumishi wa nchi Kiongozi anayeongoza wilaya, mkoa n.k ambaye kikatiba anamwakilisha Rais wa Nchi, kubeba mimba au kuzaa pasipo kuwa na ndoa inatoa taswira hasi kwa wale unaowaongoza...
Nje ya mada:

Twende mbele turudi nyuma hii mimba “imemkubali” sana mh DC. Litakua toto la kiume tu hili ndio hua yanachakaza sura kiasi hiki 🤣
 
Kweli asee.. viongozi wa umma wanapaswa kuwa na maadili kwa kuwa wanaangaliwa sana na jamii wanayoiongoza kama mfano.. basi hata ikitokea wameenda kinyume na maadili basi wafiche mambo yao yasionekane, na hata yakionekana ijulikane kuwa walijitahidi kuficha lakin ikashindikana.. sio kabisa wanatangaza na kujiweka wazi ujinga wao kana kwamba hawakukosea, sio sawa.
 
Nchi hii ina wananchi wajinga na wanafiki sana ,sasa mahusiano yake yanatuhusu nini kama utendaji wake wa kazi haujatetereka ? Ulitaka akatoe ili aendelee na uongozi ? Na ikiwa alifunga ndoa Bomani au kwa mila ulitaka akuletee vyeti nyumbani kwako ? .Hayo Maadili mnaloona ni hilo tu ,tunapigwa mabilioni ya Pesa mmekaa kimya tu ifike mahala watanzania mjielewe na kujitambua .
 
Kwa maadili ya mtumishi wa umma especially kiongozi mwandamizi hakutakiwa kuwa kazini. Maana amevunja miiko ya uongozi wa uma. Na hakutakiwa kupewa wadhifa bila kuwa na cheti cha ndoa.

Ila kwasababu tumeamua kuishi kung'ombe ng'ombe wacha iwe hivi ilivyo, tutakuja kujifunza kwa gharama maana maneno ya hekima au busara huwa hatuyaelewi hata kidogo.
 
Hakuna kumungunya maneno hatuwezi kuendelea kuongozwa na Kiongozi asiye na maadili ya utumishi, anayetarijiwa Kupata mtoto nje ya ndoa, atawashauri nini na kuwafundisha nini mabinti zetu mashuleni, ambao wengi wao wanamchukulia kama role model wao.

Jamii na Watumishi wenzake anaowasimamia watamchukuliaje?, Kiujumla tayari kapoteza sifa za kuendelea kushika wadhifa huo.

Mh. Rais tuletee DC mwingine Temeke mwenye maadili ya utumishi.

#Rais teua DC mwingine Temeke
Naunga mkono hoja.

Wale watetezi wa maadili ya kiafrika hapa utawaona wakikimbia
 
Kweli asee.. viongozi wa umma wanapaswa kuwa na maadili kwa kuwa wanaangaliwa sana na jamii wanayoiongoza kama mfano.. basi hata ikitokea wameenda kinyume na maadili basi wafiche mambo yao yasionekane, na hata yakionekana ijulikane kuwa walijitahidi kuficha lakin ikashindikana.. sio kabisa wanatangaza na kujiweka wazi ujinga wao kana kwamba hawakukosea, sio sawa.
Tujifunze Ulaya na kwingineko. Kiongozi ni mfano kwa mambo yote.
 
Nchi hii ina wananchi wajinga na wanafiki sana ,sasa mahusiano yake yanatuhusu nini kama utendaji wake wa kazi haujatetereka ? Ulitaka akatoe ili aendelee na uongozi ?
Anapaswa kuwa kwenye mstari wa kimaadili ndani na nje ya mamlaka yake.
 
Sioni shida ipo wapi?kwanza bongo hakuna sheria inakataza au ina climinalize ngono!tendo la ndoa nje ya ndoa,uwezi kushitakiwa kwa kukutwa unafanya tendo la ndoa na mtu mzima mwenzio faragha!!sio kosa kabisa!!?
Kuna sheria na maadili ya uongozi wa uma. Miongoni mwa miiko yake ni kuwa na image mbaya. Ndio maana kiongozi mwandamizi hatakiwi kufanya mambo ya hovyo
 
Mwanamke akizaq bila ndoa anajesabika kuwa ni muhuni katika jamii yetu. Ina maanisha anaweza kwenda na mtu yeyote hata mume wa mtu. Sasa haya mambo gani kwa kiongozi ambaye anatakiwa kusimamia maadili
Kabisa hii ni utomvu wa maadili.
 
Nchi hii ina wananchi wajinga na wanafiki sana ,sasa mahusiano yake yanatuhusu nini kama utendaji wake wa kazi haujatetereka ? Ulitaka akatoe ili aendelee na uongozi ?
Afunge ndoa
 
Your life is all about mindset, attitude, perspection, beliefs and you act and react to every scenario or outcomes.those can cause both physical and emotional pains that resulted from your interpretation from your internal environments of your mind and your external
Whatever, the cralility of acting as a lovelel pensica while she is a Distric Councilor is not granted as per our national morality.
 
Katika utumishi wa nchi Kiongozi anayeongoza wilaya, mkoa n.k ambaye kikatiba anamwakilisha Rais wa Nchi, kubeba mimba au kuzaa pasipo kuwa na ndoa inatoa taswira hasi kwa wale unaowaongoza.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Jokate Mwegelo kwa sasa ana mimba na anatarajiwa kupata Mtoto, lakini kitu cha kushangaa haijulikani kama ana mume ao ameolewa jambo ambalo katika maadili ya utumishi linamshusha hadhi.

Mtumishi wa serikali anayetumikia nafasi kama hii kuzaa bila ndoa haileti mantiki kwani wananchi unaowaongoza wanaweza kuzani Kiongozi wao unaruka ruka hovyo na wanaume na hivyo kukushusha hadhi.

Taasisi za dini kama katoliki, mtumishi wao tofauti na watawa ukizaa bila kuolewa tena ndoa unafukuzwa kazi, kwa sababu wanaamini utaleta uzinifu kwenye taasisi yao.

Watumishi wa serikali wenye vyeo vya juu kiutumishi hakikisheni mnafunga ndoa, ili kuleta heshima kwa mnaowaongoza.
Screenshot_20220714-221920_1.jpg
 
Back
Top Bottom