Umenikumbusha mbali, ukimtaja Savimbi, usisahau jina kama Augustino Neto, ilikuwa radio Tanzania , utasikia majina kama Daniel Ortega, wa Nicaragua wapinzani Sandinista na contras,Samora na frelimo Dhlakama na Renamo,utasikia ,Belifast bomu lalipuka, hao ni sinn fain wa N. Ireland, mtu kama Gerry Adam atatajwa,utasikia , huko mashariki ya kati majina kama Abu Nidali,Arafat,George Habash na Shimon Peres,Yitzhak Shamir, watu kama Goukini Ouedeye, Hisen Habre, huko Chad moto uliwaka,Polisario wa Sahara magharibi kukaliwa ki mabavu na Morocco, chifu Mangusuto wa afrika kusini, baadae john Garang sudani kusini, pia Thomas Samkara na Samwel Doe,kwa wahabesh Mengistu Haile-Mariam, na wengi wababe waliokuwa serikalini au upinzani(msituni-vitani) ambao tulikuwa tukiwasikiliza kwenye redio enzi hizo,bila kumsahau jenerali wa naijeria alierudi kivingine kwa kura, pia hapa kwetu majina kama Salum A.salum na brg.gnrl Hashim Mbita(pbah) walitajika sana miaka hiyo wakiwa vijana,Angola ya swapo ilikuwa nyingine,