Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,403
- 12,775
Nakumbuka enzi za utoto nilikua napenda kujiitta majina ya watu hatari hatari kama Savimbi, Hitler, Mussolin, Bocassa, Osama kweli siku zinaenda R.I.P SAVIMBI.
Kwa kuwa tokea ukiwa mtoto umependa kujiita majina ya watu waliokuwa against na jamii adilifu na kwa kuwa wote uliowapenda wamekwisha kufa,ama kuuawa basi ndugu nikutakie tu Pumziko la milele huko jehanam ikiwa utakufa bila sisi kupata taarifa.
Mungu wangu
Aisee unajua perception creates reality....!!! Naona hata username yako ina reflect hivyo...!!! PUBLIC ENERMY
aliacha chombo cha maana kumbe....
Alikufa kizembe sana, baada ya Dos santos kukubaliana na matakwa ya West hasa Marekani, Savimbi aliitwa na USA na kuambiwa vita sasa basi akagoma, na siku ya kufa kwake maraisi wote wa SADC waliitwa na USA na kuambiwa Angola vita inaisha na Savimbi anaenda kufa, savimbi aliitwa na USA polini wanakokutaniana na akaenda bila kuwa na jeshi lolote zaidi ya walinzi Wake wachache na akauliwa hapo huku vyombo ya propaganda vya West CCN, BBC, SKY nk wakishuhudia na kuchukua picha
Angola hapa, SADC kULE
Sijakuelewa Mkuu
Scenario ya hiki kifo, ni kama SADC ndio waliomuua!
Soma tena unielewe, Angola iko ndani ya SADC, na Savimbi aliuliwa na wamarekani wenyewe waliomtengeneza, lakini kabla ya kifo chake viongozi wote wa SADC walikuwa wanajua kitakachomtokea Savimbi kwani walishafaamishwa na Wamarekani
mara zote nchi zinazokuwa kwenye jumuiya fulani huwa zinakuwa updated kwa kitu chochote kikubwa cha kijeshi kitakacho tokea au kinachotarajiwa kufanyika, na hiyo huwa hivyo kuzi alert nchi zote zinazobenefit na migogoro fulani kubadirika na kukubaliana na maamuzi
DRC Iko SADC na SADC walipoamua kuwatoa waasi wa M23 member wote walifaamisha na Tanzania, Malawi na RSA ndio waliopewa kazi hiyo wakiwa pia wana baraka za UN, Wakati majeshi ya SADC/UN yataka kuingia nchi zote zilizo karibu na DRC Rwanda, Burundi na Uganda zilialifiwa kitakacho tokea na kama zina maslahi basi zibadirike na zikubaliane na kitachotokea
Miaka hiyo kila mtu mwenye madevu basi alikuwa anaitwa Savimbi
kwa waliosoma Tambaza miaka hiyo, kulikuwa na mwalimu aliyekuwa na jina lisilo rasmi la Savimbi kutokana na Midevu aliyokuwa nayo
Umenikumbusha mbali, ukimtaja Savimbi, usisahau jina kama Augustino Neto, ilikuwa radio Tanzania , utasikia majina kama Daniel Ortega, wa Nicaragua wapinzani Sandinista na contras,Samora na frelimo Dhlakama na Renamo,utasikia ,Belifast bomu lalipuka, hao ni sinn fain wa N. Ireland, mtu kama Gerry Adam atatajwa,utasikia , huko mashariki ya kati majina kama Abu Nidali,Arafat,George Habash na Shimon Peres,Yitzhak Shamir, watu kama Goukini Ouedeye, Hisen Habre, huko Chad moto uliwaka,Polisario wa Sahara magharibi kukaliwa ki mabavu na Morocco, chifu Mangusuto wa afrika kusini, baadae john Garang sudani kusini, pia Thomas Samkara na Samwel Doe,kwa wahabesh Mengistu Haile-Mariam, na wengi wababe waliokuwa serikalini au upinzani(msituni-vitani) ambao tulikuwa tukiwasikiliza kwenye redio enzi hizo,bila kumsahau jenerali wa naijeria alierudi kivingine kwa kura, pia hapa kwetu majina kama Salum A.salum na brg.gnrl Hashim Mbita(pbah) walitajika sana miaka hiyo wakiwa vijana,Angola ya swapo ilikuwa nyingine,
Hii historia murua kizazi cha leo hawaijui kabisa..! Pathetic!!!!
Mungu wangu