Jopo la Sheikh Kundecha, na Sheikh Katimba ladai kwamba Mwanasheria Mkuu wakati wa Magufuli, Prof. Kilangi, aliwahi kuwa Padri

Jopo la Sheikh Kundecha, na Sheikh Katimba ladai kwamba Mwanasheria Mkuu wakati wa Magufuli, Prof. Kilangi, aliwahi kuwa Padri

Kusikiliza hawa mashekhe ni kujivunjia heshima

..hawa Mashekhe wana hoja, tatizo ni wanapoelekeza hoja na lawama zao.

..Mashekhe walitakiwa wailalamikie na kuishutumu serikali, sio kanisa Katoliki.

..Kwa mfano, kama wanalalamika kuonewa na kufungwa wanatakiwa wailalamikie serikali, na sio Kanisa Katoliki kwasababu Kanisa Katoliki halimiliki Magereza.

..Kama wanalalamika kunyimwa nafasi za uteuzi wanapaswa kuilalamikia serikali kwasababu wanafanya uteuzi wako serikalini, na CCM.
 
Badala ya kujibu hoja za Kitima, wao wanamshambulia mtoa hoja na dini yake.

Kitima kaweka wazi, yeye anaongea kwa utashi wake; awakilishi taasisi anayoitumikia.

Hawa masheikh wa Samia (maana sio representative wa waumini) wao kazi yao kuleta udini badała ya kujibu hoja.
 
Achaneni nao, hao ndo waharibifu wa nchi hii. Wanahubiri haki msikitini halafu wakitoka wanaongea ujinga. Hao uzee wao hautaisha vizuri. Hao watakuwa wamepewa pesa kuongea upuuzi. Mbona Kikwete na Mwingi hajapingwa kama samia ambaye anahama mahali pa kulala kila siku( dom, dar, kizimkazi). Hawa wazee wamepotoka big time. Ni wazee wanaozeeka kipuuzi. Wengi wao ndo shughuli za uchawa wanazofanya.
 
..sikiliza tamko hapo chini na tuhuma kwamba AG wa kipindi cha Rais Magufuli, Prof.Kilangi, aliwahi kuwa Padri.


View: https://www.youtube.com/watch?v=RhbFPe8Z3yU

Ni mbaya sana kiongozi wa dini unapoibuka bila factual evidences na unakuwa umesema uongo maskini!
Hivi waumini wao wenye exposure hawawaambii ukweli?!
Hii ni hatari sana kwa ustawi wa taifa!
Nimetafuta kila mahali hakuna sehemu Dr.Kilangi amewahi kuwa Padre.Sijui wameitoa wapi hii hawa wazee wetu!
 
Nichezee data kusikiliza wase.nge?....badala ya kufanya maendeleo wamekalia kupiga majungu....
 
imeisha hiyo, siku za mwisho huwa hivyo, miti hutikikisika …
 
..sikiliza tamko hapo chini na tuhuma kwamba AG wa kipindi cha Rais Magufuli, Prof.Kilangi, aliwahi kuwa Padri.


View: https://www.youtube.com/watch?v=RhbFPe8Z3yU

Hivi hawa mburura kwanini huwa hawaendi shule? Most of them ni wale waliosoma shule za uswazi na walikuwa watoro wa kuruka madirishani ndiyo maana hawana akili hata ya kuchanganua mambo. Hivi kwanini hawakumpinga wakati huo au ndiyo ile sifa yao ya ubingwa wa unafiki wanaiendeleza? TEC walipambana na Magu japo naye aliwapelekesha sana huku BAKWATA wakiufyata mkia na kuamua kuwa chawa wa Jiwe, yaani bila kuongelea kilio cha Gen Z cha watu kutekwa, kulawitiwa, kuuawa, uchaguzi haramu na zilipo maiti ambazo mpaka leo hazijaonekana hayo mengine ni ngonjera tu.
 
..hawa Mashekhe wana hoja, tatizo ni wanapoelekeza hoja na lawama zao.

..Mashekhe walitakiwa wailalamikie na kuishutumu serikali, sio kanisa Katoliki.

..Kwa mfano, kama wanalalamika kuonewa na kufungwa wanatakiwa wailalamikie serikali, na sio Kanisa Katoliki kwasababu Kanisa Katoliki halimiliki Magereza.

..Kama wanalalamika kunyimwa nafasi za uteuzi wanapaswa kuilalamikia serikali kwasababu wanafanya uteuzi wako serikalini, na CCM.
Wamelipwa baba, wanatumikia bahasha zao, jana tulikula kuku nyumbani, mzee wetu alitoka, karudi na samia nyumbani, wakati aliondoka na gwajima, pesa baba
 
..sikiliza tamko hapo chini na tuhuma kwamba AG wa kipindi cha Rais Magufuli, Prof.Kilangi, aliwahi kuwa Padri.


View: https://www.youtube.com/watch?v=RhbFPe8Z3yU

These mazafakas are incredibly dumb!

1. Hakuna siku ambayo Father Kitima amewahi kupinga uchunguzi. Anachopinga ni Serikali kujichunguza yenyewe. Anataka wachunguzi huru!
2. Mahakama ya Kadhi na hospitals za Catholic Church zina uhusiano gani na matukio ya raia kuuawa na vyombo vya dola au Serikali kukataa kuendesha chaguzi zinazokidhi viwango vya chaguzi za kidemokrasia?
3. Kama hawa wapumbavu wanataka tuwaelewe, basi wajibu tuhuma dhidi ya Serikali:
🔹Serikali inaua au kupoteza raia wake
🔹Kwa kulazimisha chaguzi kufanyika kabla ya electoral reforms, Serikali imewanyima Watanzania haki ya kuchagua viongozi wanaowataka wao wenyewe
🔹Serikali inatumia raslimali za nchi kunufaishi zaidi kundi dogo la watu
 
Hao ni masheikh wa BAKWATA, kipindi hiki kidato cha nne wanafanya mitihani, matokeo yakitoka tafuteni shule za BAKWATA tuangalie wamefanyaje,hapo hutawalaumu.
Kuna tofauti kubwa kati ya waislamu wa BAKWATA na sisi waislamu wengine.
 
ukitaka kufahamu lugha ya ibilisi ina sifa kuu mbili..
1. vitisho
2. kutia hofu
waislamu wana bahati mbaya kabisa kuwa kwenye kundi la watu wa aina hii na bado wengi hawafahamu!
 
Hao ni masheikh wa BAKWATA, kipindi hiki kidato cha nne wanafanya mitihani, matokeo yakitoka tafuteni shule za BAKWATA tuangalie wamefanyaje,hapo hutawalaumu.
Kuna tofauti kubwa kati ya waislamu wa BAKWATA na sisi waislamu wengine.
BAKWATA ni jumuia ndani ya CCM ambayo jukumu lake ni kuwaghilb Waislamu waiunge mkono CCM hata kwenye mambo ya kupumbavu.
 
sikiliza tamko hapo chini na tuhuma kwamba AG wa kipindi cha Rais Magufuli, Prof. Kilangi, aliwahi kuwa Padri.

Mapito ya sheikh wetu Kundecha :

Sheikh Mussa Kundecha asimulia kashikashi nyingi alizopitia akiwa mwanaharakati Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=rDaa_3GLI2Y

Kiongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu asimulia jinsi alivyopewa kesi ya mauaji baada ya kutoafikiana na Polisi waliolazimisha aongee mbele ya vyombo vya habari kituo cha Polisi awaombe Waislamu waliokuwa na mpango wa kuandamana wasifanye hivyo. ...

Wakati huo Polisi Dar es Salaam mkuu wa upelelezi mkoa ni RCO Abdallah Zombe anaongoza .... nikatupwa selo asubuhi mahakamani nikasomewa kesi ya mauaji ya watu wawili kwa risasi mmoja askari polisi na mwingine raia, kutoka hapo nikapelekwa rumande Segerea miezi 6 ....

Kuhusu siasa Sheikh Mussa Kundecha anasema huwezi tenganisha siasa na dini.

Upande wa elimu anaelezea umuhimu wa suala hilo ... nilisoma Tabora kisha kwenda nje Burundi, Kenya, Saudi Arabia kuongeza elimu nikarudi Tanzania nikafundisha Tabora, Arusha na Dar es Salaam mitaa wa Kiungi Magomeni pia Kinondoni Mkwajuni na msikiti wa Kichangani Magomeni.

Mihadhara ya MwembeChai iliyoshamiri kuanzia mwaka 1994 hadi 1997 jijini Dar es Salaam iliniletea matatizo miaka hiyo ikiongozwa na kina sheikh Mazinge na wengine ...

Pia nilifanya kazi ya kuunganisha waislamu ambao ni wasomi (professionals) wa elimu pana ya kisecular na masheikh wa wanaotoa elimu ya dini, kwani makundi haya mawili yaani professionals wa kiislamu waliona masheikh wao hawana ufahamu wa masomo ya elimu ya secular huku pia masheikh wakiona waislamu wasomi kuwa hawana ufahamu wa dini yao.

Harakati hizi zimeleta mafanikio kuna misikiti zaidi ya 3,000 na huku kuna shule zaidi ya 300 za waislamu kutokana na kuunganisha nguvu za waislamu ....

Mussa Kundecha anaulizwa sheikh ni nani hasa ... pamoja ya kuwa sheikh ni kama inatumika kuonesha kuwa ni mtu mzima isipokuwa katika utaratibu ....

Sheikh Mussa Kundecha akiangalia mbele kuhusu kupata elimu ya dini, anashukuru kuwa mazingira yanazidi kuwa mazuri vitabu vipo vingi tofauti na zamani hapa Tanzania kilikuwapo kitabu kimoja cha Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy .. sasa kuna vingi zaidi ...

Kuhusu BAKWATA - Baraza Kuu La Waislamu Tanzania kutokubaliwa na baadhi ya waislamu, Sheikh Mussa Kundecha anasema kila mmoja ana nafasi yake hivyo ...

Wateja wengi wa Islamic Banking Tanzania ni wale wasio waislamu na wamewapita kwa idadi kubwa huku waislamu wakiwa wachache hivyo ni jambo jema la kijamii kwa wasio waislamu kuwa wengi sana kwa idadi ktk Benki za Kiislamu ...anabainisha Sheikh Kundecha
 
Back
Top Bottom