mpingauonevu
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 621
- 433
ha ha ha! Hapo kuna Kabwe Makanika aka Jitu Kumbuka. Huyu aliwasumbua aana Mafia mob wakiwa na wakubwa wao kina Don Fredrique Gaetano, Lucy Luciano na Giovani Pambieri. Kuporana almasi kule Maganzo Shinyanga na michezo ya mashine ya Magnum 357!
nimeona kijana wa zamani, aya mkuu, hivi sinti bint kasri ilikuwa miaka gani vile? athena nimeicheki, nami pia naisubiria IRIS no 5.
Ulikuwa unajisikiaje unapomuona mwenzako ameshika KUFA NA KUPONA, NJAMA, KIKOSI CHA KISASI, KIKOMO ama SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU?, LAZIMA UFE JORAM, MIKONONI MWA NUNDA, NAJISIKIA KUUA TENA!!!HEBU KUMBUKA ULIPOKUWA UNASUBURI ZAMU YAKO NA WEWE UAZIME!!!
Nimeshangazwa kujua kwamba karibia kila mwandishi bora wa nyakati hizi amefariki. Nataka tuwakumbuke na kuwaombea. Lakini ni lazima nimpongeze mwandishi bora wa nyakati hizi HUSSEIN TUWA. kwa kweli ni mkali sana hebu kwa wale wapenzi wa riwaya tutafute riwaya zake MKIMBIZI, UTATA WA 9/12 NA MDUNGUAJU
Umenikumbusha mbali sana ndugu yangu. Rider Hagard ni mwandishi maarufu sana wa zamani. Alifariki mnamo miaka ya 1920. Hadithi ya Allan Quartermain aliiandika mnamo mwaka 1898. Kabla ya hapo aliandika kitabu cha Mashimo ya Mfalme Sulemani. Ni vitabu vizuri sana... Hakika ungedhani ni habari za kweli, kwani zilihusisha baadhi ya maeneo na matukio ya kweli. Loh, sijui kama vijana wa leo wanaweza kupata vitu kama hivyo.
mkuu simu ya kifo sio faraji katalambula.wapi macarius na ray sibanda kitabu jina limenitoka.Dah! nimekikumbuka lakini mwandishi wake nimemsahau. Kulikuwa na Hammie Rajabu AMA ZAO AMA ZANGU, Nadhani aliandika pia dimbwi la damu na simu ya kifo. kilichonifanya nikumbuke ni uwezo wa kuongeza kujua kusoma na kuandika ulioongezwa na matokeo ya kusoma kitabu kwa haraka kabla hujanyang'anywa. Unajua Tanzania ya sasa watoto hawasomi kabisa na hawana namna ya kujiongezea maarifa kupitia vitabu. Kwa wenzetu watoto wanasoma sana tangu wakiwa wadogo.
a man called god ni noma.jumong anatisha babaakenimeona kijana wa zamani, aya mkuu, hivi sinti bint kasri ilikuwa miaka gani vile? athena nimeicheki, nami pia naisubiria IRIS no 5.
Umenikumbusha mbali sana,uncle wangu nowdays ni shushushu baada yakuvutiwa na kazi
za hao jamaa,nitapata wapi hivyo vitabu?
Waandishi wa siku hizi Hussein Tuwa anajitahidi,pia yupo Beka Mfaume na Innocent Ndayanse.
Naenda kuianza leo jioni, na vitabu vyote alivyotaja hapo juu ninavyo naanza kuvisoma
Hivi waigizaji wetu hawawezi kuekti muvi kwa stori za vitabu vile? nadhani zikiigizwa muvi zitauza na kupendwa sana.Muhanga wa ikulu ni cha BEKA MFAUME na yeye yuko vizuri sana. Edwin Semzaba sikumsoma sana. Mimi alikuwa ni Hammie rajabu na Fred katalambuya (kama sijakosea). Nadhani hawa pia ni marehemu yaaani!!!!
Dah! nimekikumbuka lakini mwandishi wake nimemsahau. Kulikuwa na Hammie Rajabu AMA ZAO AMA ZANGU, Nadhani aliandika pia dimbwi la damu na simu ya kifo. kilichonifanya nikumbuke ni uwezo wa kuongeza kujua kusoma na kuandika ulioongezwa na matokeo ya kusoma kitabu kwa haraka kabla hujanyang'anywa. Unajua Tanzania ya sasa watoto hawasomi kabisa na hawana namna ya kujiongezea maarifa kupitia vitabu. Kwa wenzetu watoto wanasoma sana tangu wakiwa wadogo.
Tuna shida kubwa sana ya professionalism kwenye arts. Ukiwaona hawa wa mtaani wanapenda sana visa vya mapenzi na kwa sababu hakuna ufundi wa scripts basi wewe tafuta msichana mzuri halafu awe anakaa nusu uchi soko umepata. Wale wasomi wa bagamoyo wanakosa uhalisia inakuwa kama wanasoma. Kwa vitabu vya action kama hivi nadhani kwa Afrika bado sana maana hata Nigeria sijaona movie za action labda South Afrika.Hivi waigizaji wetu hawawezi kuekti muvi kwa stori za vitabu vile? nadhani zikiigizwa muvi zitauza na kupendwa sana.
mkuu simu ya kifo sio faraji katalambula.wapi macarius na ray sibanda kitabu jina limenitoka.
Kama Kumbukumbu yangu ni sahihi Simu ya Kifo ni kitabu cha zamani zaidi na kiliandikwa na Hassan Hussein Katalambula kama sikosei na si Hammie Rajab.
Hivi mrembo Zabibu alikuwepo katika simulizi ya kitabu gani...? nadhani ni Njama kama sikosei (nisahihishwe tafadhali). Willy Gamba alipojibarizi naye...alimsifia sana na kumwambia "Yaani, wewe kweli ni mtamu kama zabibu"
daaa nilisoma vtabu hivyo miaka ya 1989 mtwara huko yani acha tu jamani pia enzihzo sani lilikuwa toleo babu kubwa kuna mwandishi amri bawji huyu mtu wa tanga nadhani aliandika lovestory tanga nyika na unguja na kitabu flani cha pumbazo la moyo cjui viko wapi jamani.