Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Jordan imekiona kitisho cha vita baina ya Iran na Israel na imeanza kujiweka mbali na Israel.
Katika kujitetea kwanini walidungua droni za Iran zilizokuwa zikielekea Israel,nchi hiyo ya kifalme imesema haikufanya hivyo kuitetea Israel bali ilikuwa ni kuwalinda raia wake dhidi ya vifaa vilivyopita kwenye anga lake.
Kauli hiyo ya kujitetea imetolewa na waziri wa mahusiano ya nje,Mohammed Swafad na mawaziri wengine wa ufalme huo.
Wakiendelea kufafanua hatua yao hiyo,mawaziri hao wamesema kitendo chao hicho si kwa makombora kutoka Iran tu bali hata kutoka nchi nyengine yoyote ile.
Kwa upande wake mfalme Abdallah wa nchi hiyo katika mazungumzo na raisi Biden wa Marekani,amesema hataki nchi yake iwe ni uwanja wa vita baina ya Iran na Israel.
Ili mashambulio ya Israel dhidi ya Iran yafanikiwe ni lazima ipate ushirikiano kutoka kwa mataifa matatu ya kiarabu inayopakana nayo.
Zaidi ya nusu ya raia wa Jordan wana asili ya Palestina akiwemo mke wa mfalme wa Jordan,bi Rania.
Katika siku za karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la maandamano ya kuiunga mkono Palestina na kutaka kufutwa kwa mkataba wa mapatano baina ya Israel na nchi hiyo uliotiwa saina mwaka 1994.Mkataba ambao tangu mwanzo haujaungwa mkono na raia wa nchi hiyo.