José Mourinho kusaini mkataba wa miaka miwili na Real Madrid

Narudi kuwa Shabiki wa Madrid tena baada ya Mironho kurudi. Alipo Morinho Nipo, akiondoka kwa kufukuzwa timu hiyo na uongozi wake naichukia. Paul Pogba alimletea ujinga pale man U huyu jamaa mpaka leo Man U inajitafuta kubebea walau Carabao
 
Masupastaa wajipange. Mwamba huwa hadekezi wauza sura. Ukifanya kazi atakukubali. Ukimletea ujuaji na kuuza sura kwingi, anakutupa kwenye hii kitu 🚮

Mwamba aliwapa bench Sergio Ramos na Iker Casillas na alikuwa anachukua points kwenye kila game. Mourinho doesn't give a shit about your status. Ingekuwa Dunia ya sasa wangesema ni AI.
 
Laana inaendelea kuwatafuna Madrid kwa walichomfanyia Carlo. wataendelea kubadilisha makocha tu

Kwa wanaoijua Real Madrid watakwambia Don Carlo alibahatika kuikuta Real Madrid iliyotengenezwa ba Jose Mourinho. Bernabeu kulikuwa na majina makubwa kama Raul Gonzalez, Figo, R9, David Beckham, Roberto Carlos na wengineo lakini bado walistrugle. Miaka ile mimi nilikuwa naishi Ciudad de Madrid. Lakini fiesta zilianza tena Bernabeu baada ya Mourinho kutoka Italy kuja pale.
Alibadilisha mfumo mzima wa mpira pale na Real Madrid ikawa moto. Ndoo zote walizobeba Don Carlo na Zidane, Jose Mourinho apewe maua yake. Aliamua kuondoka kwa kiburi chake tu lakini alitawa akae kuenjoy matunda ya kazi yake. Madridista wote tuko happy anarudi
 
Mourinho ni muasisi wa kupack bus kama akiona timu pinzani ni kali kuliko yake! Real madrid aliwaliza akiwa na kitimu kidogo cha benfica! Almanusura wasiingie hatua ya mtoano champions league!
Ana uwezo wa kukupa matokeo hata kama timu yake si kali kivile! Wakati akiwa Inter Milan, alliteration sana Barcelona iliyokuwa moto wa kuotea mbali na akabeba ndoo!!
 
The Special one! Mourinho huwapiga mkwala mastar kwa kuwaambia yeye ndio star pekee kwenye timu!! Ukileta nyodo unaozea bench!
 

TAKATAKA

watu wazima tuseleteane mambo ya kitoto.
 

unamaanisha nini ukisema muasisi? watu wanapaki basi tuko black and white mkuu, unatwambiaje Mourinho ndio muasisi?
 
Jose aliletwa Madrid kuja kubeba makombe au kutengenezea watu njia?

Ndio maana nikasema unakuwaga na umama sana. Toa maoni yako, elezea tujue upeo wako kuhusu football sio unakuja hapa ueleweki unataka nini
 
Ukiona Real Madrid wamemgeukia Mourinho ujue ukame wa vikombe umewachosha!

Personally I'm not a big fan of Jose Mourinho lakini bado namuheshimu sana kama manager wa modern football. He's cocky person with different attitudes lakini bado ni competitive na ana uwezo wa kumiliki rocke room.
For the last 3 seasons pamoja na kuchukua la liga na UCL lakini Real Madrid bado iko kwenye transition. Full of talents in the squad lakini timu bado inaonekana mediocre kwasababu hajapatikana mtu sahihi mwenye creative ideas kwa ajili ya project mpya.
Na wachezaji hawahawa na Mourinho utashangaa kuona different games.
 
bayern wanakwenda patupu na Kampany
Patupu kivipi!? Maana kama ni nyumbani juzi tu wametia kibindoni ndoo zote mbili za nyumbani kama ambavyo imekuwa kawaida yao kwa miaka mingi.

Kama ni Ulaya hata Madrid hana chake Ulaya na sio Ulaya peke yake hata nyumbani hana chake, kwani mahasimu wake Barcelona ndio watawala sasa. Tena sio mara moja.

Haya sasa elezea hiyo patupu yako ni ipi!?
 

hata wewe unaweza beba kombe la Bundesliga na Bayern, kipimo cha kocha Buyern kipo kwenye champion league
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…