Jose Mourinho ni kocha mbovu anayebebwa na pesa za usajili

Jose Mourinho ni kocha mbovu anayebebwa na pesa za usajili

MOU kabeba Uefa na Porto, Mara ya mwisho kwa timu ndogo nje ya ligi Tano bora kubeba Uefa ni 1994 Ajax alipobeba, Miaka hii ishirini iliopita mabinhwa wote wa Uefa ni timu Kubwa, Madrid, Barca, Bayern etc.

Porto hawana budget kubwa, hawana wachezaji wazuri, lakini ni mbinu za MOU ziliwapa kombe,

Mara ya mwisho Inter kubeba UCL ni 1965 na MOU pia kawapa na wachezaji wake kina Diego Millito, MOU kawajaza sumu wameperform 200% ya uwezo wao alipoondoka na wao wakarudi kuwa wachezaji wa kawaida.

MOU akipewa authority 100% na kuwa juu ya wachezaji matokeo analeta.
We mwamba mtu akitaka kubishana nawe kwa hoja ktk soka inabidi ajipange haswaaa...maana uko vizuri kuliko maelezo Chifu.

Heshima kwako mkuu.
 
Ni Kocha mzuri sana na ana Roho, mikakati ya ushindi tatizo ni wachezaji na uongozi wa team anazokutana nazo, wachezaji ni wavivu, na wana viburi, hawajitumi, uongozi umejaa siasa na majungu. yeye anachotaka ni Kazi na matokeo mazuri. Akipata team aachiwe awe na uhuru wa kufanya maamuzi, team hio itafankiwa sana.
Upo sahihi. Tatizo la Mournho ni kwamba hataki Kubembeleza mchezaji, anaamini zaidi suala la Nidhamu. Bahati mbaya timu nyingi kwasasa Kocha hana nguvu kwa 100%, Na mchezaji anaweza kusababisha Kocha atimliwa.

Mourinho alifanikiwa sana kipindi cha nyuma kutokana na kuwa na nguvu zaidi ya Wachezaji. Vivyohivyo Ferguson alifanikiwa sana Man utd kwakuwa alikuwa na nguvu sana juu ya hatima ya mchezaji. Tukumbuke issue yake na Berkam na hatimaye Berkam akauzwa. Ingekuwa Leo hii kwa umaarufu wa Berkam ninauhakika angeondoka Kocha na mchezaji angebaki
 
Back
Top Bottom