Jose Mourinho ni kocha mbovu anayebebwa na pesa za usajili

Jose Mourinho ni kocha mbovu anayebebwa na pesa za usajili

Najua watu wengi sana macho yao yapo kwa Zidane. Lakini na yeye pia sio kocha mzuri wa kupewa kikosi kibovu akakitengeza. Zidane upande fulani ni kama Mourinho, give hi m the players he wants na sio umwambie aanze kumwagilia maji madogo wa academy. Tofauti ya Zidane na Mou, ni kwamba Z yeye wachezaji wana uhuru wa kucheza watakavyo as long as wanashirikiana na kutafuta ushindani wakati mourinho anataka ucheze anavotaka yeye hata kama ikibidi lukaku akae kipa lazima ukubali. Mou hata kama upo chini ya goli bado kupiga shuti ushinde yeye kama anataka urudishe mpira kwa jones basi uurudishe. ndio maana anakosana na wachezaji.

Tunaweza kwenda kwa pochettino, namuona kuwa ni mtu ambae kama anamwagiwa hela kama alizopewa Mouninho basi ataifikisha timu mbali. Au tunaweza kwenda kwa Simione nae pia ni kocha ambae ana uwezo, tatizo ni resources kwake ni limited kama pochetino.

MU ili panic baada ya Pep kujiunga na MC, ndio maana wakamtimua LVG na kumueka MO.

Sikatai MO anarekodi nzuri, enzi zake Chelsea ukifika Stamford unajitaarisha kuzuia usifungwe mengi, mana pale darajani hata SAF aliteswa sana na MOU, ila huyu wa sasa nawaambia watu kila siku, sio yule wa enzi zile damu inamchemka.
Umeongea vyema hapo atleast diego simeion ndo ataiweza hyo timu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu kibaya kutendea akili, nafsi na roho kama ku judge jambo kwa hisia, tamaa, hulka, silka, chuki na wivu.

Ina maana mnataka kusema kikosi cha Man U ni bora zaidi ya kikosi cha Man City?

Mnataka kusema kikosi cha Man U ni bora zaidi ya kikosi cha Liverpool?

Kikosi cha Man U ni bora zaidi ya kikosi cha Chelsea?

Ina maana mnataka kusema mmekwisha sahau Mou wa Porto? Porto kulikuwa na wachezaji gani?

Mmekwisha sahau Mou wa Chelsea? Aliyeleta Chelsea toka uvunguni hadi kwenye timu ya kuchukua mikoba?

Mmekwisha sahau Mou wa Inter Millan aliyechukua treble huku akiwatoa Barca wakiwa kwenye ubora wao wa karne?

Mmekwisha sahau Mou wa Man U yule aliyekuja msimu wa kwanza kasajili wachezaji watatu tu kachukua Europa, Community Shield, n.k. msimu wa kwanza?

Mmekwisha sahau Mou yule msimu uliopita alipeleka Man U nafasi ya pili ligi kuu, nafasi ambayo Man U haijawahi kufika tangu Sir Alex astaafu?

Mmekwisha sahau kuwa Klop, Pochetino wote walikuwa England muda tu lkn hadi sasa hawana hata bakuli sembuse kombe?

Mmekwisha sahau kwamba msimu uliopita kama sio Man city walio kwenye ubora mkubwa basi kombe la ligi likeenda Man U? Akina Klop, Conte na Pochetino walikuwa wapi?

Ina maana mmekwisha sahau namna Mou alivyokuwa analialia kuhusu kupatiwa walau mchezaji mmoja tu beki?

Ina maana hamuoni namna Man City, Liverpool na Chelsea wanavyofanya manunuzi?

Ina maana mmekwisha sahau kauli ya Ed Woodward kwamba matokeo ya Man U uwanjani hayana athari zozote za kibiashara (na hiki ndicho kilichofanya pasiwepo usajili wa maana msimu huu)

Makosa yanayofanywa na mabeki wa Man U ni ya Mou?

Ok. Tuseme hayo yamepita kwenu hayana maana tena. Sasa, kama mshabiki wa Soka wewe unadhani ukipewa hicho kikosi cha Man U cha sasa utafika nacho wapi????

Kwa waelewa wa soka, mtakubalina nami kuwa Ed Woodward ndio chanzo cha ubovu wa Man U. Lazima alipokuwa Gill David na Sir Alex mambo yalikuwa yanaenda vizuri kabisa.

Na kwa kuona hilo ndio maana wanamtafuta Sporting Director ambaye yeye atakuwa anajihusisha na usajili tu na Ed Woodward kujihusisha na masuala ya commercial ya club maana anashindwa kumudu nafasi zote mbili kwa mpigo.

Na ndio maana fans wa Man U mechi ya juzi waliwa pigia makofi mengi sana wachezaji pamoja na Mou japo game walipoteza. Hii ni kwa sababu wanaelewa wazi wapi tatizo la timu lipo.

Na kwa wafuatiliaji wa soka la ushindani, Man U kumuondoa Mou pale watakuwa na options chache sana za kupata makocha bora.

Mou bado ni kocha bora sana. Man U wanashindwa kukubaliana na wakati, kwamba soka la leo ni pesa. Beki ghali zaidi duniani yupo Liverpool, Golikipa ghali zaidi duniani yupo Liverpool na Chelsea, n.k. n.k

Punguzeni wivu na chuki binafsi.
Ishu ni mfumo mourinho mpe mabeki wagumu ,midifilderz ngumu na foward mmoja hatar ...yaani mourinho anafanya vizur akiwa na wachezaji aina ya maroboti na sio wakina wachezaji wakunyumbulika yaani skilled players.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kante,mahrez shrupp, hao walikuja kuongeza nguvu pia kumbuka hamna mchezaj pale alietoka kwenye academy ya hiyo timu
Walitumia pesa kidogo kulinganisha na timu zilizokua zinachuana top four.

Kwangu ndiyo timu iliyochukua ubingwa bila kutumia pesa.
 
Walitumia pesa kidogo kulinganisha na timu zilizokua zinachuana top four.

Kwangu ndiyo timu iliyochukua ubingwa bila kutumia pesa.
Kuchukua ubingwa bila kutumia pesa ni kuwa na players uliozalisha ktk academy yako umenunua players bado unasema hujatumia pesa nimekupa mfano kante alinunuliwa toka france mahrez toka france uliona michango yao

Ungeniambia walibeba ubingwa kwa kutumia pesa kidogo point yako ingekuwa active.
 
Ishu ni mfumo mourinho mpe mabeki wagumu ,midifilderz ngumu na foward mmoja hatar ...yaani mourinho anafanya vizur akiwa na wachezaji aina ya maroboti na sio wakina wachezaji wakunyumbulika yaani skilled players.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpira unaevolve leo hii mabeki wenye roho mbaya utawapata wapi? Au upaki basi usubiri kuvizia, angalia hata Italia makocha wamebadilika sana wanacheza mpira wa kushambulia zaidi. Lakini Jose anajifanya hataki kuapdate staili aliyoizoea
 
Ya Mourihno leo 29/09/2818 yatamtokea Kocha wa Simba kesho 30/09/2018.

Amebebwa na hela za usajili. Kesho kiama chake.
 
Vipi huko kwenu kuna nafasi__.jpg
 
Hakuna fact hapa ni porojo tuu.. soka la sasa ni pesa.. usiposajili unategemea nini?? alichofanya José .. Guardiola hajafika hata nusu!.. anaebisha leta fact
 
Back
Top Bottom