Josee Chameleon: The Very Best of East Africa

Josee Chameleon: The Very Best of East Africa

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
MILENIA ya tatu ilikuwa inausabahi ulimwengu. Ni mwanzo wa Karne ya 21, hii ni kwa mujibu wa Gregorian Calendar. Mwaka ni 2000, Joseph Kibweteere alishazingua kinoma Uganda, alisababisha vifo vya watu 778. Kipindi hichohicho, Joseph mwingine alikuwa Kenya akitengeneza heshima ya Uganda.

Ndani ya studio za Ogopa Deejays, Nairobi, Joseph alifanya kweli na wimbo “Bageya”, uliochengua vema Uganda na Kenya. The Kenya’s finest, Redson, alitisha kwenye ngoma hiyo. Mwaka 2001, ikawa mwanzo wa utawala wa Joseph East Africa, alipofyatua hit ya eneo lote la Maziwa Makuu, “Mama Mia”.

Joseph huyu hakuwa Kibweteere. Ni Joseph Mayanja. Business moniker ni Chameleone. Tamka, Jose Chameleone, kisha tembea na jina hilo Afrika Mashariki yote, ushuhudie ukuu wake ulivyotamalaki nchi kwa nchi.

Baada ya "Mama Mia" kuhodhi airwaves za Afrika Mashariki, Chameleone aliamua kujiundia tabia ya kuteremsha hit baada ya hit. Kila kazi aliyoachia, iligeuka dude la East Africa. “Njoo Karibu”, “Jamila”, “Sauti ya Dhahabu”, “Mambo Bado”, “Kipepeo”, “Bahati Yangu”, “Shida za Dunia”. Hatujamaliza.

Kabla ya kuendelea kushusha vyuma, tukumbuke songombingo la Joseph wawili, Mayanja na Haule ambaye dunia inamwita Profesa Jay. Mdundo wa ngoma “Nikusaidieje” wa Profesa Jay, Chameleone aliutumia kutoa kitu, “Bomboclaat”. Kisha, Joseph wawili wakaingia studio wakafyatua anthem, “Ndivyo Sivyo”. Amani ikatawala. Mgogoro wa kazi ukasuluhishwa kwa kazi.

Tuendelee sasa; “Bei Kali”, “Mama Rhoda” ft Bushoke, “Dorotia”, “Vumilia”, “Naomba Uniamini”, “Naumia”, “Badilisha”, “Valuvalu”, “Tubonge”. Zote hizi ni East African hits. Ni kwa sababu hiyo, Chameleone akiwa Kenya, kama yupo Uganda, anapokuwa Tanzania, anasahau kama alizaliwa Kampala.

Ukuu wa Chameleone unajengwa na uandishi wake. Kutoka wimbo hadi wimbo, husimulia hadithi yenye mafunzo. Ametengeneza sound ya kipekee. Huwezi kuinakili wala kuiiba. He is the very best of East Africa.

Julai 31, 2026, The Super Dome, Oysterbay, Bongo Flava Honors itamtunuku Chameleone hadhi ya hall of fame. Utapigwa muziki wa viwango vya kuufungua Mlango Bahari wa Hormuz. Sugu the Jongwe atasimamia show.

Ndimi Luqman MALOTO

1784734621839.jpg
 
Huyu jamaa ni mkali sana wa kuimba. Karibia nyimbo zake zote mpaka leo bado ninazikubali, kwa kuwa zimebeba ujumbe usiochuja.

Msanii wetu Bushoke alibakia kuwa pacha namba moja wa huyu mwamba kwenye collabo zake zote alizofanya naye.

Shida kubwa ya huyu mwamba ni ile tu ya kumpenda sana dear gambe.
 
Umimweka chameleon na Kibwetere, namchagua Kibwetere kwa kujua kuawaangamiza walokole.

Ukijifanya ng'ombe unapokelewa kama na treatment utakavyopata ni kama ya ng'ombe.
 
Mayanja alizaliwa Uganda lakini musically alizaliwa Kenya. Bila ule ubunifu wa Wakenya kumpika pale Nairobi, Bageya isingetoboa na pengine angeendelea kusubiri tu Kampala.
 
Anastahili hiyo heshima ya hall of fame, mwamba anajua mnoo na ngoma zake hazichuji. Nuff respect
 
Back
Top Bottom