Team Bashite! Pilipili usiyoila inakuwashia Nini? Hayo yaliyoandikwa kwenye hiyo barua yalijulikana masaa machache kabla ya Tamasha? Alietoa kibali hakujuwa uwepo wa hizo sababu? Kawe hamna Hospitali? Hamna Wagonjwa wa BP?CEO wa CMG Mr. Joseph Kusaga jana kupitia mahojiano yako katika 360 ulisikika ukisema kuwa Fiesta lazima ifanyike ndani ya mwaka huu, Lakini ulienda mbali sana na kufikia kusema umeshaongea hadi na Mh Rais kwaajili ya tamasha lako la Fiesta.
Kimsingi Afisa Utamaduni wa Manispaa ya kinondoni kwenye barua yake kwenu yenye Kumb No. KMC/UT/KMO/01 ya tarehe 23/11/2018 haikupiga marufuku Tamasha la Fiesta isipokuwa eneo lalamikiwa ambalo linafanyika tamasha lenu lilikuwa na karibu na Hospital na kuwataka tamasha lenu lipelekwe Tanganyika Peakers-kawe, Ata kama musingetaka lifanyike Tanganyika Peakers labda kutokana na miundombinu basi ata Uwanja wa uhuru ungefaa pia.
Kwenda kuongea na Mh Rais kushinikiza Tamasha lenu lifanyike Leaders tena ni kuto tii mamlaka za chini sasa musije kufikia hatua mukawa munamshinikiza Mh Rais avunje utaratibu wa mamlaka zake za chini kisa uswahiba wenu.
Nakutaka Kusaga kuheshimu mamlaka kwani manispaa ya Kinondoni ishapiga marufuku kwa shughuli zozote za matamasha kufanyika hapo Leaders na usitumie mwanya wa uswahiba wako na Mh Rais kushinikiza yale unayoyataka ilimradi sheria na taratibu zivunjwe.
CEO fuata utaratibu.
Tanzania ina wajinga wengi Sana, kibaya zaidi, asilimia kubwa Ni Vijana, mmojawapo Ni wewe!