Joseph Kusaga: Tamasha la Fiesta kufanyika Dar es Salaam Disemba, namiliki Redio zote za vijana

Joseph Kusaga: Tamasha la Fiesta kufanyika Dar es Salaam Disemba, namiliki Redio zote za vijana

MD wa clouds media Joseph Kusaga tamasha la fiesta halina faida yoyote kifedha kwa upande wa clouds tofauti na watu wanvyosema na kudhani inawanyonya wasanii, Kusaga anasema wanaendelea kufanya Fiesta kwasababu wanaamini katika kuwapa wasanii platform na kukuza mziki wa bongo fleva
Kusaga aliongeza ukiangalia gharama za maandalizi na vile watu wanapoona watu wamejazana viwanjani Basi wanajua clouds wanakusanya mamilioni lakini ukweli ni kwamba gharama za kuendesha Fiesta ni kubwa kuliko kill kinachopatikana.
Ameongeza Fiesta Dar es Salaam itafanyika kabla mwaka kuisha.
Huwezi kuendesha kitu kisicho na faida kwa manufaa ya wengine ilihali wewe ni mfanyabiashara.

BIG NO! Anatafunga kamba huyu jamaa, duniani hakuna mwenye harakati za mshumaa. Aungue mwanga wapate wengine
 
Yes CMG wanamazuri mengi kuliko mabaya. Kama unaakili utajifunza na hasa wajisiliamali wanapaswa kujifunza namna CMG inavyo handle wafanyakazi na kuwatumia kwa faida ya pande zote.
Kweli kuna mengi ya kujifunza kutoka kwao ni kuamua kuchagua kujifunza au kuchagua kusikiliza tu makosa yao na kusbiri wapi wanapokosea.
You only see what your eyes want you to see.
 
Huwezi sema hadharani naingiza mabilion ya pesa kupitia huu mradi kwa hapa bongo!

Wengi wa Wabongo kuanzia viongoz mpaka RAIA wa kawaida huwa wamejaa roho za wivu na kwanini!
Ukitamka tu naingiza kiasi flani tayari hujuma zinaanza!

Ndio maana ukiwa na mradi wako bongo hata ukipiga vimilioni kadhaaa we lalamika umepata faida kidogo sana!!
 
Siri yoyote ya biashara ni kutokuonesha kuwa umeianzisha kwaajili ya kupata faida.

Siku zote wafanyabiashara huwa wanajaribu kuonesha UMMA kuwa FOCUS YAO KUBWA SIYO PESA WALA FAIDA, ila lengo lao ni KUSAIDIA WATU au kutatua MATATIZO YA WATU.

Hivyo alichokizungumza yuko sahihi ndio ilivyo kwa mfanyabiashara yoyote.

Lakini ukweli halisi ni kuwa WANAPIGA FAIDA ZA AJABU !
umesomeka saana mkuu
 
Huwezi kuendesha kitu kisicho na faida kwa manufaa ya wengine ilihali wewe ni mfanyabiashara.

BIG NO! Anatafunga kamba huyu jamaa, duniani hakuna mwenye harakati za mshumaa. Aungue mwanga wapate wengine
Kwenye mstari wako wa mwisho hiyo inaitwa "huruma ya mshumaa, yaani mshumaa hutoa mwanga lakini huku unateketea".
 
CLOUDS FM ILIANZA MWAKA 1999 BONGO FLEVA ILIANZA 1981 NADHANI BOSI KUSAGA AMEANZA KUCHANGANYA MAFAILI .

IVI HAJUI KABLA YA CLOUDS STESHENI NYINGI ZILIKUWA ZINAPIGA BONGO FLEVA
Nitajie mwanamuziki wa bongo fleva 1981 kwa kumbu kumbu zangu miaka hiyo ni break dance ,robot ,rhumba ,chacha , regae tena ya bob marley na burning spear, highlife style kutoka nigeria ,blues na pop
Naomba ushuhuda
 
Yes CMG wanamazuri mengi kuliko mabaya. Kama unaakili utajifunza na hasa wajisiliamali wanapaswa kujifunza namna CMG inavyo handle wafanyakazi na kuwatumia kwa faida ya pande zote.
Amemshukuru sana Charles Kimei kwa kuwaamini na kuwapa mkopo wa millioni 40 miaka 20 plus iliyopita.

Joseph Kusaga wanaotaka kumsifu shime tumpe sifa na shukrani zake sasa hivi msisubili mpaka Mungu ampende ndio muanze unafki wenu wa sifa za marehemu.
 
Ongezea wadhamini wanatoa shillingi ngapi? Ndio yale yale ya kampuni za madini kila siku wanakuambia hawapati faida, lkn madini yanaisha na wenzetu ambao wana madini kama yale Wanafaidika.

Alafu kama Fiesta ingekuwa haina faida, sasa kwa nini wanawabania wasanii wasiotaka kushiriki tamasha la Fiesta.
hawawabanii ila kuna wasanii wengine wanaringa eti ukimuita kwenye show anataka mill 100 kiruuu c bora upige mziki tu watu wacheze
 
hawawabanii ila kuna wasanii wengine wanaringa eti ukimuita kwenye show anataka mill 100 kiruuu c bora upige mziki tu watu wacheze
Sio kwamba anaringa bali anajitambua na anatambua thamani yake. Hivi Ruby naye alivyobaniwa alikuwa anataka milion 100.
 
Anajaribu kuwafanya watu " Matomaso " yaani mfanya biashara afanye biashara isiyo na faida " kwa kipindi cha muda wa Miaka 10s .... kusaga aache kuvuta bangi
 
MD wa clouds media Joseph Kusaga tamasha la fiesta halina faida yoyote kifedha kwa upande wa clouds tofauti na watu wanvyosema na kudhani inawanyonya wasanii, Kusaga anasema wanaendelea kufanya Fiesta kwasababu wanaamini katika kuwapa wasanii platform na kukuza mziki wa bongo fleva
Kusaga aliongeza ukiangalia gharama za maandalizi na vile watu wanapoona watu wamejazana viwanjani Basi wanajua clouds wanakusanya mamilioni lakini ukweli ni kwamba gharama za kuendesha Fiesta ni kubwa kuliko kill kinachopatikana.
Ameongeza Fiesta Dar es Salaam itafanyika kabla mwaka kuisha.
[emoji445][emoji445][emoji444][emoji443][emoji441][emoji441] mafanikio ni kama chupi.... Hakikisha hawajui Rangi..[emoji445][emoji445][emoji441][emoji441]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Mfanyabiashara kwenye ubora wake
 
Hakuna mtu wa kufanya biashara kichaa ya bila faida ...kusaga asione watu ni watoto wadogo
 
Back
Top Bottom