Joseph Kusaga: Tamasha la Fiesta kufanyika Dar es Salaam Disemba, namiliki Redio zote za vijana

Joseph Kusaga: Tamasha la Fiesta kufanyika Dar es Salaam Disemba, namiliki Redio zote za vijana

"...nimezungumza hadi na Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kwamba pengine suala ni venue..."
Maajabu ya Tanganyika na watu wake.
 
Wazo la Endorsement ndilo unalo zungumzia na alisema " Kama Mh Rais unanisikia, Mh Waziri na Mkuu wangu wa Mkoa basi watupe eneo la kujenga Endorsement yenye kuchukua ata watu 20,000 kwa kushirikiana na wadau" lakini Issue ya fiesta alishasema alimeongea na Mh Rais tayari.

Ata Issue ya Endorsement nayo itakuja kuleta malalamiko maana Diamond alishawasilisha mpaka kwa Waziri mkuu kuomba eneo la kujenga Endorsement na Juzi mkubwa Fela nae kamuomba tena Waziri wa habari, Sanaa utamaduni na Michezo kuomba eneo la kujenga Endorsement tena.

Acha kumuonea wivu Joe

Bosi haswa wa Diamond kumbe umekuwa humujui miaka yoteeeee

Ulichoandika wekea watu kideo.. sema kuanzia dk ya ngapi.. na tuambie y unaumua juu ya MD Joe na yake au niseme yao?
 
Kusaga vipi hali ya ruge anaendeleaje maana siku iz naona mnatoa sana #tbt zake kulikoni?
 
Acha kumuonea wivu Joe

Bosi haswa wa Diamond kumbe umekuwa humujui miaka yoteeeee

Ulichoandika wekea watu kideo.. sema kuanzia dk ya ngapi.. na tuambie y unaumua juu ya MD Joe na yake au niseme yao?
Yani we ndiyo zumbukuku kweli! sasa wamtishia nani hapa? Mi nimesikiliza jana na kasema kuwa ameshaongea na Mh Rais sasa nilichosema asije akatumia ukaribu wake vibaya kuzihujumu mamlaka za chini!
We unakuja hapa na mikwara yako eti nianike! Anika chupi yako...!
 
Mi sijamshutumu Mh Rais lakini Kusaga jana amesikika amesema ameshaonea na Mh rais kuhusu hilo Tamasha lifanyike kabla ya mwaka huu kuisha! Sasa unaweza jiuliza inakuwaje akaongee na Mh Rais kisa Fiesta? manaake anatumia uo mwanya ili ashinikize tamasha lifanyike Leaders na si kwengine kama angekubaliana na Manispaa kwanini asipeleke uwanja Uhuru? manaake anataka Mh Rais aingilie kati hilo suala lake afosi ngoma irudi Leaders sasa sijui kama Mh Rais kawakubalia au lah! hapo tusubiri ila nimeandika hili kuonyesha mapema endapo litafanyika Leaders basi Mh Rais kashinikiza.
Sidhani kama Mh Rais atauingia huu mkenge!
Nina imani na Mh Rais.

Jaman tuache roho mbaya, hivi unataka kuniambia ww ungekuwa na access ya kuonana na rais usingetumia hiyo chance kupata mtelemko flan?
 
Jaman tuache roho mbaya, hivi unataka kuniambia ww ungekuwa na access ya kuonana na rais usingetumia hiyo chance kupata mtelemko flan?
Sasa ni roho mbaya au tunaongea tu ili sheria na utaratibu vifuatwe?
 
Sasa ni roho mbaya au tunaongea tu ili sheria na utaratibu vifuatwe?

Hiyo ni roho mbaya, ww ktk maisha yako ujawahi kuomba msaada hata kama ni sehemu ambayo ilitakiwa ufate sheria? Sheria Zote za Tanzania unazifata?
 
Hahaha Kusaga AJENGE UKUMBI iwe ni Leaders au popote akafanye FIESTER hata kila siku, sisi wagonjwa wa moyo hatutaki kelele, akijenga ukumbi asisahau uwe ni sound proof pia,mlio lipia na mlioko ndani tu ndio msikie sisi hatutaki kusikia.
Naomba na waislam wakumbushwe vipaza sauti viwe ndani msikitini tu, sisi ambao hatujaenda msikitini ujumbe hautuhusu!.
 
CEO wa CMG Mr. Joseph Kusaga jana kupitia mahojiano yako katika 360 ulisikika ukisema kuwa Fiesta lazima ifanyike ndani ya mwaka huu, Lakini ulienda mbali sana na kufikia kusema umeshaongea hadi na Mh Rais kwaajili ya tamasha lako la Fiesta.

Kimsingi Afisa Utamaduni wa Manispaa ya kinondoni kwenye barua yake kwenu yenye Kumb No. KMC/UT/KMO/01 ya tarehe 23/11/2018 haikupiga marufuku Tamasha la Fiesta isipokuwa eneo lalamikiwa ambalo linafanyika tamasha lenu lilikuwa na karibu na Hospital na kuwataka tamasha lenu lipelekwe Tanganyika Peakers-kawe, Ata kama musingetaka lifanyike Tanganyika Peakers labda kutokana na miundombinu basi ata Uwanja wa uhuru ungefaa pia.

Kwenda kuongea na Mh Rais kushinikiza Tamasha lenu lifanyike Leaders tena ni kuto tii mamlaka za chini sasa musije kufikia hatua mukawa munamshinikiza Mh Rais avunje utaratibu wa mamlaka zake za chini kisa uswahiba wenu.

Nakutaka Kusaga kuheshimu mamlaka kwani manispaa ya Kinondoni ishapiga marufuku kwa shughuli zozote za matamasha kufanyika hapo Leaders na usitumie mwanya wa uswahiba wako na Mh Rais kushinikiza yale unayoyataka ilimradi sheria na taratibu zivunjwe.

CEO fuata utaratibu.
Kwani itakiwa mara ya kwanza kuvunja sheria, acha wivu watu tule burudani
 
Kwani itakiwa mara ya kwanza kuvunja sheria, acha wivu watu tule burudani
Sio Wivu mi sijapenda kumshirikisha Mh Rais ilimradi avunje utaratibu na hili litamuharibia Mh Rais na ndiyo maana katika Post nimeandika kabisa ata uwanja wa Uhuru si fresh tu! Kwanini amtumie Mh Rais alimradi aipate Leaders? hii haijakaa sawa itaonekana Mh Rais ameweka Uswahiba mbele itamchafua kisiasa.
 
Hiyo ni roho mbaya, ww ktk maisha yako ujawahi kuomba msaada hata kama ni sehemu ambayo ilitakiwa ufate sheria? Sheria Zote za Tanzania unazifata?
Unajua mi sijaongea kwa ubaya, Lengo langu hii issue asimusishe Mh Rais! Leo ikionekana Fiesta imeenda Leaders unajua nani atatukanwa? Unajua nani atadhalilishwa? Unajua nani atafedheheswa? Ni Mh Rais hii itakaa mbaya kisiasa! itaonekana anawabeba marafiki ilimradi wavunje utaratibu! kama tamasha ata akifanyia Uwanja wa Uhuru mbona fureshi tu! ila asing'ang'ania Leaders na kibaya zaidi kamtaja mpaka Mh Rais kana kwamba kaenda kumlalamikia ilimradi apapate Leaders na hii itakuwa turufu kwa vyama vya upinzani kumchafua Mh Rais.
 
Sio Wivu mi sijapenda kumshirikisha Mh Rais ilimradi avunje utaratibu na hili litamuharibia Mh Rais na ndiyo maana katika Post nimeandika kabisa ata uwanja wa Uhuru si fresh tu! Kwanini amtumie Mh Rais alimradi aipate Leaders? hii haijakaa sawa itaonekana Mh Rais ameweka Uswahiba mbele itamchafua kisiasa.
Hivi unakumbuka baada ya Fiesta kustishwa kwa kisingizio cha hospitali Gazet la Mwananchi walienda hadi kwenye hyo hosptali na kufanya mahojiano na Mganga mkuu na kusema hakuna aliyelalamikia mziki wa fiesta, hueni kuwa fiesta ilistishwa kwa hila za mtu flani na njia sahihi ilikuwa ni kuongea na Rais ili atoe ruksa yake fiesta.
 
Unajua mi sijaongea kwa ubaya, Lengo langu hii issue asimusishe Mh Rais! Leo ikionekana Fiesta imeenda Leaders unajua nani atatukanwa? Unajua nani atadhalilishwa? Unajua nani atafedheheswa? Ni Mh Rais hii itakaa mbaya kisiasa! itaonekana anawabeba marafiki ilimradi wavunje utaratibu! kama tamasha ata akifanyia Uwanja wa Uhuru mbona fureshi tu! ila asing'ang'ania Leaders na kibaya zaidi kamtaja mpaka Mh Rais kana kwamba kaenda kumlalamikia ilimradi apapate Leaders na hii itakuwa turufu kwa vyama vya upinzani kumchafua Mh Rais.

Kwani pale leaders hizo hosp zimejengwa mwaka huu? Si maika yote zipo?
Fiesta ngapi zimefanyika, bonanza ngapi zimefanyika Mbona hakuna watu wamekuja?
Mpaka wameenda kwa mkuu means wameona Kuna figisu
 
Kwani pale leaders hizo hosp zimejengwa mwaka huu? Si maika yote zipo?
Fiesta ngapi zimefanyika, bonanza ngapi zimefanyika Mbona hakuna watu wamekuja?
Mpaka wameenda kwa mkuu means wameona Kuna figisu
Barua ilijieleza "Kutokana na malalamiko" sasa sidhani kama utakuwa sawa malalamiko mbona hayakuwa toka mwaka juzi! na Juzi manispaa imepiga marufuku kabisa tamasha lolote kufanyika pale hasa ya muziki, sijui dini ambayo sauti inakuwa kubwa kiasi kama kile
 
Hivi unakumbuka baada ya Fiesta kustishwa kwa kisingizio cha hospitali Gazet la Mwananchi walienda hadi kwenye hyo hosptali na kufanya mahojiano na Mganga mkuu na kusema hakuna aliyelalamikia mziki wa fiesta, hueni kuwa fiesta ilistishwa kwa hila za mtu flani na njia sahihi ilikuwa ni kuongea na Rais ili atoe ruksa yake fiesta.
Mwenye ile Hospital ndiye aliandika barua kwenda manispaa kuomba ile shughuli inawabughudhi pale! embu fikiria mwenyewe sound kama ile alafu mita 150-200 kuna hospital! just be serious jomba! ukiwa Hospital tu huruhusi kupiga honi alafu mtu anafunga sound moja ambalo hatari! Inshort taarifa za serikali ni siri ningekuwekea.
 
Barua ilijieleza "Kutokana na malalamiko" sasa sidhani kama utakuwa sawa malalamiko mbona hayakuwa toka mwaka juzi! na Juzi manispaa imepiga marufuku kabisa tamasha lolote kufanyika pale hasa ya muziki, sijui dini ambayo sauti inakuwa kubwa kiasi kama kile

Sasa fiesta inaenda kufanyika pale pale hahahaha
 
Back
Top Bottom