Joseph Mbilinyi (Sugu) yupo mahututi hospitalini baada ya kipigo cha Polisi

Joseph Mbilinyi (Sugu) yupo mahututi hospitalini baada ya kipigo cha Polisi

Huwa nakuona mtu wa hekima nyingi ilaa.......
Hekima ni kutii bila shuruti.

Ujinga wafanye wao, matamshi ya kuvuja amnai walete wao, masimamishwe ujinga wao wao. Hekima unaitafuta kwangu?

Waulize kwanini walitowa matamko ya uvunjifu wa amani? Waulize walipoambiwa wasikusanyike kwanini waliendelea na hilo zoezi> Hekima yao ilikuwa wapi?

Ushakatazwa kufanya ujinga unaendelea kuufanya halafu unategemea hekima kutoka kwangu?

Punguwani wahed.
 
Nata tamko lao la leo wanaongelea "kujikomboiwa
". Kujikombowa kutoka wapi? Kwani hawajuwi kuwa Tanzania ipo huru?
 
Kama yupo hai ni bahati yake sana, Tanzania tusikubali kupoteza maisha ya wengi kwa ajili ya ujinga wa wachache.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
SUGU YUPO MAHUTUTI HOSPITALI, DAR ES SALAAM.


1.Sugu anaongea kwa taabu sana na Sauti ya chini sana, kutoka Hospitali binafsi aliyopelekwa leo asubuhi.

2.Sugu alivamiwa na kupigwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadhi binafsi siyo kwa kutuma askari wa chini,

Kuanzia nje ya ofisi za Kanda ya Nyasa, Mkoani Mbeya kwa kushambuliwa kwa makofi baadae akawa anatumia rungu kabla ya askari wengine kuja kujumuika na Kamishina Awadhi Haji

3.Kamishina Awadhi Haji aliacha Kumpiga Sugu baada ya Askari wengine wengi kuja kuja kumsaidia kumshambulia Sugu sehemu mbalimbali za mwili wake.

4.Kamishina Awadhi Haji alipoacha kumpiga Sugu alihamia katika kumpiga Katibu Mkuu John Mnyika, ambapo alikuwa Mnyika anavutwa kwa nguvu na askari wanamuita mheshimiwa

Kamishina Awadhi ndiyo alikuwa mtu wa kwanza pia kumpiga Katibu Mkuu Mnyika huku akiwafokoea askari wengine kuita Mnyika Mheshimiwa,

"Waheshimiwa wapi hawa, hawa ni wahuni tu, wanataka kuvuruga amani ya nchi. Wanachezea nchi."

5. Katibu Mkuu John Mnyika na Sugu walipandishwa katika Landcruiser hardtop Pickup kwa kuwalaza kifudifudi na juu askari zaidi ya 8 waliokuwa nyuma waliwakanyaga kuanzia Mbeya hadi Makambako

Njiani, Mnyika na Sugu walipokuwa wanajitahidi kutengeneza mazingira ya kuweza vichwa vyao vizuri waweze kupua walipigwa sana marungu ya miguuni na migongoni.

6. Katibu Mkuu Mnyika alishushwa Makambako, kisha Sugu aliendelea na safari akiwa amelazwa pale chini kifudifudi vilevile.

7.Muda wote wa safari, askari waliokuwa wanawasindikiza Mnyika na Sugu walikuwa wamevaa vinyago "mask"

8.Sugu alifikishwa Iringa Juzi majira ya Saa 9 :00 usiku na kuwekwa mahabusu ya pekee yake.

9.Jana majira ya Saa 9 : 00 Jioni walimchukua Sugu kutoka Mahabusu ya Kituo cha Polisi Central, Iringa kwenda Dar es Saalam wakiwa na gari ndogo.

10 Majira ya Saa 5 :00 usiku Polisi walimfikisha Sugu katika kituo cha Polisi Central, Dar es saalam, akiwa anaumwa kiasi cha wao kuogopa kumuweka Mahabusu wala kumpa neno lolote.

11.Polisi Central, Dar es saalam walioona hali mbaya ya sugu tangu ashushwe katika gari kutokea Iringa waligoma kumpa PF (Kibali cha kwenda kutibiwa) na Waligoma wao kumpeleka Hospitali, Walimuitia teksi wakailipa Tsh 7,000/= Dereva atafute sehemu ya kulaza wageni ampeleke Sugu.

12. Kwa sasa Sugu yupo katika Matibabu, baada ya kupata majeraha sehemu za Mgongoni, Mbavuni, Kichwani na Miguuni sehemu ya ugoko.

13.Mwisho, sugu na Mnyika wameibiwa simu zao zote pamoja na fedha kiasi cha Dollar elfu tano na shilingi milioni 3 za Kitanzania.

Boniface Jacob (Ex Mayor)


=====

UPDATES: 1830HRS

======

JamiiForums, imezungumza na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, anaelezea:

Taarifa za Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) pamoja na Katibu Mkuu John Mnyika ni kati ya walioumizwa wakati Polisi wanawakamata kwenye Ofisi zetu Mbeya, hatua ya sasa wameenda kwenye matibabu.

Bahati mbaya Jeshi la Polisi halikuwapeleka kwenye matibabu hata walipolalamika wana maumivu makali, Mnyika akipelekwa nyumbani kwake Dar, Sugu pia aliletwa Dar licha ya kuwa nyumbani kwake ni Mbeya. Wote hawana simu kwa sasa.

Sugu alipelekwa Hospitalini ndio lakini kama bado yupo amelazwa au ametoka hizo taarifa sina kwa sasa hadi niende nikamuone sababu hana simu.

===
AGOSTI 14 (5:30 Asubuhi)
Sugu ameandika kwenye Mtandao wa X.

Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi mkuu, TUMEFIKAJE hapa tena???!!!!


PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
Inasikitisha kwa kweli,Mungu wa Mbinguni atamlinda Mheshimiwa na atapona lakini Police tumieni nafasi zenu vizuri maisha ni haya haya kuna siku mtastaafu je jamii itawachukuliaje??Na nyie ni sehemu ya jamii,zingatieni utu msitumike vibaya,vyeo huisha lakini ubinadamu hubaki pale pale.
 
Au Mnatafuta mazingira yakupiga hela maana nyie jamaa tunawajua Ni matapeli tapeli Sana
 
Umeona Sugu akiwa ICU ameandika kuukiza,"Mama Samia,amiri jeshi Mkuu,tumefikaje hapa?"
Nadhani Sugu anawaza Ile sys ya BibliaGenesis 41:44,ambapo Pharaoh anamwambia Joseph, Nwananchi asiinue mkono au mguu bila ruhusa ya kiongozi."
Kwa hiyo aliyekuwa anaambiwa alikuwa Joseph na Sugu pia ni Joseph; kwamba mwananchi asiinue mkono au mguu bila ruhusa ya kiongozi. Pia asidise bila ruhusa ya kiongozi. Unafikiria tunaweza kumpata kiongozi kama huyo?
 
Sugu nae aache mambo kama ya Suarez kwenye mpira, maana hata akiguswa kidogo tu, anajifanya kavunjwa mguu wote..!! Aache kutafuta public sympathy
Ni kwa kiasi gani umepata maheraha Dr ndo anaweza kujua!
 
Inasikitisha kwa kweli,Mungu wa Mbinguni atamlinda Mheshimiwa na atapona lakini Police tumieni nafasi zenu vizuri maisha ni haya haya kuna siku mtastaafu je jamii itawachukuliaje??Na nyie ni sehemu ya jamii,zingatieni utu msitumike vibaya,vyeo huisha lakini ubinadamu hubaki pale pale.
Sugu ana post hauwezi kuwa mahututi upost hizo no drama
 
Back
Top Bottom