Joseph Mbilinyi (Sugu) yupo mahututi hospitalini baada ya kipigo cha Polisi

Joseph Mbilinyi (Sugu) yupo mahututi hospitalini baada ya kipigo cha Polisi



JamiiForums, imezungumza na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, anaelezea:

Taarifa za Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) pamoja na Katibu Mkuu John Mnyika ni kati ya walioumiza wakati Polisi wanawakamata kwenye Ofisi zetu Mbeya, hatua ya ssa wameenda kwenye matibabu.

Bahati mbaya Jeshi la Polisi halikuwapeleka kwenye matibabu hata walipolalamika wana maumivu makali, Mnyika akipelekwa nyumbani kwake Dar, Sugu pia aliletwa Dar licha ya kuwa nyumbani kwake ni Mbeya. Wote hawana simu kwa sasa.

Sugu alipelekwa Hospitalini ndio lakini kama bado yupo amelazwa au ametoka hizo taarifa sina kwa sasa hadi niende nikamuone.

========================


SUGU YUPO MAHUTUTI HOSPITALI,DAR ES SALAAM.

1.Sugu anaongea kwa taabu sana na Sauti ya chini sana, kutoka Hospitali binafsi aliyopelekwa leo asubuhi.

2.Sugu alivamiwa na kupigwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadhi binafsi siyo kwa kutuma askari wa chini,

Kuanzia nje ya ofisi za Kanda ya Nyasa, Mkoani Mbeya kwa kushambuliwa kwa makofi baadae akawa anatumia rungu kabla ya askari wengine kuja kujumuika na Kamishina Awadhi Haji

3.Kamishina Awadhi Haji aliacha Kumpiga Sugu baada ya Askari wengine wengi kuja kuja kumsaidia kumshambulia Sugu sehemu mbalimbali za mwili wake.

4.Kamishina Awadhi Haji alipoacha kumpiga Sugu alihamia katika kumpiga Katibu Mkuu John Mnyika, ambapo alikuwa Mnyika anavutwa kwa nguvu na askari wanamuita mheshimiwa

Kamishina Awadhi ndiyo alikuwa mtu wa kwanza pia kumpiga Katibu Mkuu Mnyika huku akiwafokoea askari wengine kuita Mnyika Mheshimiwa,

"Waheshimiwa wapi hawa, hawa ni wahuni tu, wanataka kuvuruga amani ya nchi. Wanachezea nchi."

5. Katibu Mkuu John Mnyika na Sugu walipandishwa katika Landcruiser hardtop Pickup kwa kuwalaza kifudifudi na juu askari zaidi ya 8 waliokuwa nyuma waliwakanyaga kuanzia Mbeya hadi Makambako

Njiani, Mnyika na Sugu walipokuwa wanajitahidi kutengeneza mazingira ya kuweza vichwa vyao vizuri waweze kupua walipigwa sana marungu ya miguuni na migongoni.

6. Katibu Mkuu Mnyika alishushwa Makambako, kisha Sugu aliendelea na safari akiwa amelazwa pale chini kifudifudi vilevile.

7.Muda wote wa safari, askari waliokuwa wanawasindikiza Mnyika na Sugu walikuwa wamevaa vinyago "mask"

8.Sugu alifikishwa Iringa Juzi majira ya Saa 9 :00 usiku na kuwekwa mahabusu ya pekee yake.

9.Jana majira ya Saa 9 : 00 Jioni walimchukua Sugu kutoka Mahabusu ya Kituo cha Polisi Central, Iringa kwenda Dar es Saalam wakiwa na gari ndogo.

10 Majira ya Saa 5 :00 usiku Polisi walimfikisha Sugu katika kituo cha Polisi Central, Dar es saalam, akiwa anaumwa kiasi cha wao kuogopa kumuweka Mahabusu wala kumpa neno lolote.

11.Polisi Central, Dar es saalam walioona hali mbaya ya sugu tangu ashushwe katika gari kutokea Iringa waligoma kumpa PF (Kibali cha kwenda kutibiwa) na Waligoma wao kumpeleka Hospitali, Walimuitia teksi wakailipa Tsh 7,000/= Dereva atafute sehemu ya kulaza wageni ampeleke Sugu.

12. Kwa sasa Sugu yupo katika Matibabu, baada ya kupata majeraha sehemu za Mgongoni, Mbavuni, Kichwani na Miguuni sehemu ya ugoko.

13.Mwisho, sugu na Mnyika wameibiwa simu zao zote pamoja na fedha kiasi cha Dollar elfu tano na shilingi milioni 3 za Kitanzania.

Boniface Jacob (Ex Mayor)

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
Tunaelekea wapi nchi hii!
 
Na wale ambao walishingilia wakiwa ccm na wakapewa na madaraka ? Unawaweka katika kundi gani?
Nao pia time is the judge, si unaona walivyo sasa hivi, unajua Dkt Magufuli ktk uhai wake hakuwahi kusimamia jambo akashindwa so his spirit speaks alot about him. Kwa ufupi wapinzani wa Dkt Magufuli walipofuka sana kiasi kwamba kwa tamaduni za binaadamu akishafariki huwa mnasahau tofauti na kuungana kuomboleza ila wao ndiyo wakaanzisha thread za kutukana maiti, wakapiga picha ili kudhalilisha maiti, wakadhani watanzania wataungana nao ila wakabaki peke yao wakishangilia huku watanzania kwa mamilion wakimlilia sana
 
Hao ni certified criminals
Haya mambo Tlaatlaah ndy anapenda kuona

Ova
nafatilia kwa karibu sana jambo hili la kusikitisha kwa mwanadamu ili kujiridhisha na taarafa za pande zote mbili, ndipo sasa naweza kueleza maoni na mtazamo wangu bila mbambamba yoyote...

namtakia ahueni ya mapema huyo muungwana kiongozi muandamizi wa chadema kanda ya Nyasa 🐒
 
Hongera zake Sugu kwa kupata kipigo cha mbwa koko. Nadhani sasa wataelewa maana halisi ya mamlaka ya rais. Alipofariki Dkt Magufuli sugu na genge lake walifanya sherehe za kupongezana na kumsifia sanaaa Dkt Samia. Ila wakasahau kuwa aliyefariki ni mmoja na mfumo wote upo kama ulivyo. Sasa naona watakumbuka na kumkumbuka Dkt Magufuli alivyokuwa anawapenda. Tunamtakia afya njema aje ashuhudie. Na hapo unaweza kuta mbowe ndiyo kaagiza apigwe mpaka afe ili asigombanie nafasi ya uenyekiti
Aisee!
 
Back
Top Bottom