Joseph Mbilinyi (Sugu) yupo mahututi hospitalini baada ya kipigo cha Polisi

Joseph Mbilinyi (Sugu) yupo mahututi hospitalini baada ya kipigo cha Polisi

SUGU YUPO MAHUTUTI HOSPITALI,DAR ES SALAAM.


1.Sugu anaongea kwa taabu sana na Sauti ya chini sana, kutoka Hospitali binafsi aliyopelekwa leo asubuhi.

2.Sugu alivamiwa na kupigwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadhi binafsi siyo kwa kutuma askari wa chini,

Kuanzia nje ya ofisi za Kanda ya Nyasa, Mkoani Mbeya kwa kushambuliwa kwa makofi baadae akawa anatumia rungu kabla ya askari wengine kuja kujumuika na Kamishina Awadhi Haji

3.Kamishina Awadhi Haji aliacha Kumpiga Sugu baada ya Askari wengine wengi kuja kuja kumsaidia kumshambulia Sugu sehemu mbalimbali za mwili wake.

4.Kamishina Awadhi Haji alipoacha kumpiga Sugu alihamia katika kumpiga Katibu Mkuu John Mnyika, ambapo alikuwa Mnyika anavutwa kwa nguvu na askari wanamuita mheshimiwa

Kamishina Awadhi ndiyo alikuwa mtu wa kwanza pia kumpiga Katibu Mkuu Mnyika huku akiwafokoea askari wengine kuita Mnyika Mheshimiwa,

"Waheshimiwa wapi hawa, hawa ni wahuni tu, wanataka kuvuruga amani ya nchi. Wanachezea nchi."

5. Katibu Mkuu John Mnyika na Sugu walipandishwa katika Landcruiser hardtop Pickup kwa kuwalaza kifudifudi na juu askari zaidi ya 8 waliokuwa nyuma waliwakanyaga kuanzia Mbeya hadi Makambako

Njiani, Mnyika na Sugu walipokuwa wanajitahidi kutengeneza mazingira ya kuweza vichwa vyao vizuri waweze kupua walipigwa sana marungu ya miguuni na migongoni.

6. Katibu Mkuu Mnyika alishushwa Makambako, kisha Sugu aliendelea na safari akiwa amelazwa pale chini kifudifudi vilevile.

7.Muda wote wa safari, askari waliokuwa wanawasindikiza Mnyika na Sugu walikuwa wamevaa vinyago "mask"

8.Sugu alifikishwa Iringa Juzi majira ya Saa 9 :00 usiku na kuwekwa mahabusu ya pekee yake.

9.Jana majira ya Saa 9 : 00 Jioni walimchukua Sugu kutoka Mahabusu ya Kituo cha Polisi Central, Iringa kwenda Dar es Saalam wakiwa na gari ndogo.

10 Majira ya Saa 5 :00 usiku Polisi walimfikisha Sugu katika kituo cha Polisi Central, Dar es saalam, akiwa anaumwa kiasi cha wao kuogopa kumuweka Mahabusu wala kumpa neno lolote.

11.Polisi Central, Dar es saalam walioona hali mbaya ya sugu tangu ashushwe katika gari kutokea Iringa waligoma kumpa PF (Kibali cha kwenda kutibiwa) na Waligoma wao kumpeleka Hospitali, Walimuitia teksi wakailipa Tsh 7,000/= Dereva atafute sehemu ya kulaza wageni ampeleke Sugu.

12. Kwa sasa Sugu yupo katika Matibabu, baada ya kupata majeraha sehemu za Mgongoni, Mbavuni, Kichwani na Miguuni sehemu ya ugoko.

13.Mwisho, sugu na Mnyika wameibiwa simu zao zote pamoja na fedha kiasi cha Dollar elfu tano na shilingi milioni 3 za Kitanzania.

Boniface Jacob (Ex Mayor)


=====

UPDATES: 1830HRS

======

View attachment 3068821
JamiiForums, imezungumza na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, anaelezea:

Taarifa za Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) pamoja na Katibu Mkuu John Mnyika ni kati ya walioumizwa wakati Polisi wanawakamata kwenye Ofisi zetu Mbeya, hatua ya sasa wameenda kwenye matibabu.

Bahati mbaya Jeshi la Polisi halikuwapeleka kwenye matibabu hata walipolalamika wana maumivu makali, Mnyika akipelekwa nyumbani kwake Dar, Sugu pia aliletwa Dar licha ya kuwa nyumbani kwake ni Mbeya. Wote hawana simu kwa sasa.

Sugu alipelekwa Hospitalini ndio lakini kama bado yupo amelazwa au ametoka hizo taarifa sina kwa sasa hadi niende nikamuone sababu hana simu.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
Siku Gen Z wakiingia mitaan hawa mabumunda wata jua hii nchi no yetu sote. Kwann kuumizana huu ni ushamba na upumbavu wa hali ya juu
 
Siku Gen Z wakiingia mitaan hawa mabumunda wata jua hii nchi no yetu sote. Kwann kuumizana huu ni ushamba na upumbavu wa hali ya juu
Waingie kwanini?

Purpose matters and surely politics won’t be the reason

Chakadomos have failed big time
 
Niko Mkoa ambao siyo asili yangu na kuna jamaa zangu wengi tu wa kule kwetu wako huku kwa shughuri mbalimbali.

Sasa kuna mmoja ni mfanya biashara mkubwa kiasi,ana kaka yake mkubwa ni mstaafu alikuwaga Askari polisi na ana makazi yake Dar Es Salaam.
Ila huyu mstaafu amechakaa ile mbaya na kibaya zaidi yeye na mkewe wanaishi ndani ya nyumba moja ila kila mmoja anapika kivyake.

Naona aliwekeza muda wake mwingi kuwapiga akina Lipumba virungu vya ugoko kiasi cha kwamba mpaka leo hii ikitokea anahitajika kwenda UJITANI ni lazima ataomba nauli kutoka kwa mdogo wake.

Hili hafanyi kwa kuzuga wala eti kutokana na ukwasi wa mdogo wake bali ni kweli kwamba anakosa namna sahihi ya kupata fedha sasa nami huwa simhurumii hata kidogo kwani mdogo anasema alifikia kwake kutoka UJITANI,wakiishi ndani ya vile vinyumba vya polisi,dogo akafanyiwa figisu na kufukuzwa pale,akatumia hiyo nafasi vizuri akajenga nyumba pale KIBAHA huku kaka yake kazi yake kubwa ikiwa ni kutumia KIWI kukigeuza kiatu kuwa kioo na kupiga watu virungu vya ugoko.
 
Waingie kwanini?

Purpose matters and surely politics won’t be the reason

Chakadomos have failed big time
Unataka ulete siasa wakati sija weka itikadi hapo..? Rudia kusoma. Ndio shida yakuwa chawa yaan unawaza kila saa chadema. Ongea kama mtanzania alie erevuka.
 
duh na ubonge wote ule kapigwa hadi mahututi? kwa maana kumpeleka mtu over weight kama yule chini unahitaji equal and opposite amount of force au zaidi, kweli duniani kuna mambo …
Mkuu inawezekana unaenjoy saivi, ila amini hautoondoka duniani kabla hayajakupata yaliyompata Sugu.

Ukifurahia udhalimu utakutwa na udhalimu. Shetani hajawahi kuwa mwaminifu kwa watu wake.
 
Nikiwa mdogo nilikuwa nasikiliza ngoma ya Sugu "Mikononi mwa polisi".
Sugu hajaanza leo purukushani na polisi. He had also survived dictatorship couple of years ago. Get well Jongwe. 😁
Sugu Moto Chini...
 
Back
Top Bottom