Joseph Mbilinyi (Sugu) yupo mahututi hospitalini baada ya kipigo cha Polisi

Kama ni kweli wapinzani walishangilia kifo cha JPM (naamini ushahidi haupo), na wewe ukaona kuwa ni kitendo kibaya, sawasawa na wewe unavyofurahia mateso wanayoyapata, basi wewe utakuwa ni binadamu wa ajabu anayelipa ubaya kwa ubaya.

Huna la kumfundisha muovu kwa kulipa uovu kwa uovu.

Vikundi vya kumtukana Samia ndiyo vipi hivyo!!??
Vimechukuliwa hatua ya kupelekwa mahakamani!!??
Bosi ukweli tunaelewa kabisa wapinzani wanaonewa ila ilikuwaje wakashangilia kifo cha Dkt Magufuli???? Inakuwaje wanaanzisha vikundi vya kumtukana Dkt Samia. Wakome kabisa. Tunahitaji taifa linalofuata misingi ya kuheshimiana na kuvumiliana.
 
Mkuu inawezekana unaenjoy saivi, ila amini hautoondoka duniani kabla hayajakupata yaliyompata Sugu.

Ukifurahia udhalimu utakutwa na udhalimu. Shetani hajawahi kuwa mwaminifu kwa watu wake.
Kwani wewe umekuwa Mungu?
 
Dola 5000 na 3m wanafanya nazo nini mtaani badala ya kuwa benki? Tukisema walikuwa na nia ovu kutembea na hizo pesa zote tutakosea?
Sheria inaelekeza Mtanzania kutembea na kiasi gani cha fedha mfukoni? Na ni kiasi gani akikutwa nayo inakuwa kosa kisheria?!
 
Mkuu inawezekana unaenjoy saivi, ila amini hautoondoka duniani kabla hayajakupata yaliyompata Sugu.

Ukifurahia udhalimu utakutwa na udhalimu. Shetani hajawahi kuwa mwaminifu kwa watu wake.

nimeuliza tu swali, wamewezaje kumpiga mtu mzito hadi mahututi? i mean, ni lazima walikuwa kundi la askari waliomchamgia mande hadi kumuangusha na kumuumiza mahututi, its not easy, ulishawahi kupambana na mtu mwenye mwili mkubwa? siyo rahisi kihivyo kumtakle na kumpeleka chini …
 
SUGU YUPO MAHUTUTI HOSPITALI,DAR ES SALAAM.

1.Sugu anaongea kwa taabu sana na Sauti ya chini sana, kutoka Hospitali binafsi aliyopelekwa leo asubuhi.

2.Sugu alivamiwa na kupigwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadhi binafsi siyo kwa kutuma askari wa chini,

Kuanzia nje ya ofisi za Kanda ya Nyasa, Mkoani Mbeya kwa kushambuliwa kwa makofi baadae akawa anatumia rungu kabla ya askari wengine kuja kujumuika na Kamishina Awadhi Haji

3.Kamishina Awadhi Haji aliacha Kumpiga Sugu baada ya Askari wengine wengi kuja kuja kumsaidia kumshambulia Sugu sehemu mbalimbali za mwili wake.

4.Kamishina Awadhi Haji alipoacha kumpiga Sugu alihamia katika kumpiga Katibu Mkuu John Mnyika, ambapo alikuwa Mnyika anavutwa kwa nguvu na askari wanamuita mheshimiwa

Kamishina Awadhi ndiyo alikuwa mtu wa kwanza pia kumpiga Katibu Mkuu Mnyika huku akiwafokoea askari wengine kuita Mnyika Mheshimiwa,

"Waheshimiwa wapi hawa, hawa ni wahuni tu, wanataka kuvuruga amani ya nchi. Wanachezea nchi."

5. Katibu Mkuu John Mnyika na Sugu walipandishwa katika Landcruiser hardtop Pickup kwa kuwalaza kifudifudi na juu askari zaidi ya 8 waliokuwa nyuma waliwakanyaga kuanzia Mbeya hadi Makambako

Njiani, Mnyika na Sugu walipokuwa wanajitahidi kutengeneza mazingira ya kuweza vichwa vyao vizuri waweze kupua walipigwa sana marungu ya miguuni na migongoni.

6. Katibu Mkuu Mnyika alishushwa Makambako, kisha Sugu aliendelea na safari akiwa amelazwa pale chini kifudifudi vilevile.

7.Muda wote wa safari, askari waliokuwa wanawasindikiza Mnyika na Sugu walikuwa wamevaa vinyago "mask"

8.Sugu alifikishwa Iringa Juzi majira ya Saa 9 :00 usiku na kuwekwa mahabusu ya pekee yake.

9.Jana majira ya Saa 9 : 00 Jioni walimchukua Sugu kutoka Mahabusu ya Kituo cha Polisi Central, Iringa kwenda Dar es Saalam wakiwa na gari ndogo.

10 Majira ya Saa 5 :00 usiku Polisi walimfikisha Sugu katika kituo cha Polisi Central, Dar es saalam, akiwa anaumwa kiasi cha wao kuogopa kumuweka Mahabusu wala kumpa neno lolote.

11.Polisi Central, Dar es saalam walioona hali mbaya ya sugu tangu ashushwe katika gari kutokea Iringa waligoma kumpa PF (Kibali cha kwenda kutibiwa) na Waligoma wao kumpeleka Hospitali, Walimuitia teksi wakailipa Tsh 7,000/= Dereva atafute sehemu ya kulaza wageni ampeleke Sugu.

12. Kwa sasa Sugu yupo katika Matibabu, baada ya kupata majeraha sehemu za Mgongoni, Mbavuni, Kichwani na Miguuni sehemu ya ugoko.

13.Mwisho, sugu na Mnyika wameibiwa simu zao zote pamoja na fedha kiasi cha Dollar elfu tano na shilingi milioni 3 za Kitanzania.

Boniface Jacob (Ex Mayor)

=====

UPDATES: 1830HRS

======

View attachment 3068821
JamiiForums, imezungumza na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, anaelezea:

Taarifa za Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) pamoja na Katibu Mkuu John Mnyika ni kati ya walioumizwa wakati Polisi wanawakamata kwenye Ofisi zetu Mbeya, hatua ya sasa wameenda kwenye matibabu.

Bahati mbaya Jeshi la Polisi halikuwapeleka kwenye matibabu hata walipolalamika wana maumivu makali, Mnyika akipelekwa nyumbani kwake Dar, Sugu pia aliletwa Dar licha ya kuwa nyumbani kwake ni Mbeya. Wote hawana simu kwa sasa.

Sugu alipelekwa Hospitalini ndio lakini kama bado yupo amelazwa au ametoka hizo taarifa sina kwa sasa hadi niende nikamuone sababu hana simu.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
Mungu amlaani awadhi na hao mbwa wengine polisi this too much 🥹🥹
 
Noma sana.

Waziri wa Mambo ya ndani from South Afrika..

Waziri Tamisemi from South Afrika

Kamanda......from South Afrika.
Lakini wao huko kwao hakuna Mu Ethiopia hata mmoja anaweza kuwa Hata mwenyekiti wa Mtaa...jamaa wamejipanga...

Kweli Uchawi upo ndugu zangu.
Awadhi ni mtanganyika.
 
SUGU YUPO MAHUTUTI HOSPITALI,DAR ES SALAAM.

1.Sugu anaongea kwa taabu sana na Sauti ya chini sana, kutoka Hospitali binafsi aliyopelekwa leo asubuhi.

2.Sugu alivamiwa na kupigwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadhi binafsi siyo kwa kutuma askari wa chini,

Kuanzia nje ya ofisi za Kanda ya Nyasa, Mkoani Mbeya kwa kushambuliwa kwa makofi baadae akawa anatumia rungu kabla ya askari wengine kuja kujumuika na Kamishina Awadhi Haji

3.Kamishina Awadhi Haji aliacha Kumpiga Sugu baada ya Askari wengine wengi kuja kuja kumsaidia kumshambulia Sugu sehemu mbalimbali za mwili wake.

4.Kamishina Awadhi Haji alipoacha kumpiga Sugu alihamia katika kumpiga Katibu Mkuu John Mnyika, ambapo alikuwa Mnyika anavutwa kwa nguvu na askari wanamuita mheshimiwa

Kamishina Awadhi ndiyo alikuwa mtu wa kwanza pia kumpiga Katibu Mkuu Mnyika huku akiwafokoea askari wengine kuita Mnyika Mheshimiwa,

"Waheshimiwa wapi hawa, hawa ni wahuni tu, wanataka kuvuruga amani ya nchi. Wanachezea nchi."

5. Katibu Mkuu John Mnyika na Sugu walipandishwa katika Landcruiser hardtop Pickup kwa kuwalaza kifudifudi na juu askari zaidi ya 8 waliokuwa nyuma waliwakanyaga kuanzia Mbeya hadi Makambako

Njiani, Mnyika na Sugu walipokuwa wanajitahidi kutengeneza mazingira ya kuweza vichwa vyao vizuri waweze kupua walipigwa sana marungu ya miguuni na migongoni.

6. Katibu Mkuu Mnyika alishushwa Makambako, kisha Sugu aliendelea na safari akiwa amelazwa pale chini kifudifudi vilevile.

7.Muda wote wa safari, askari waliokuwa wanawasindikiza Mnyika na Sugu walikuwa wamevaa vinyago "mask"

8.Sugu alifikishwa Iringa Juzi majira ya Saa 9 :00 usiku na kuwekwa mahabusu ya pekee yake.

9.Jana majira ya Saa 9 : 00 Jioni walimchukua Sugu kutoka Mahabusu ya Kituo cha Polisi Central, Iringa kwenda Dar es Saalam wakiwa na gari ndogo.

10 Majira ya Saa 5 :00 usiku Polisi walimfikisha Sugu katika kituo cha Polisi Central, Dar es saalam, akiwa anaumwa kiasi cha wao kuogopa kumuweka Mahabusu wala kumpa neno lolote.

11.Polisi Central, Dar es saalam walioona hali mbaya ya sugu tangu ashushwe katika gari kutokea Iringa waligoma kumpa PF (Kibali cha kwenda kutibiwa) na Waligoma wao kumpeleka Hospitali, Walimuitia teksi wakailipa Tsh 7,000/= Dereva atafute sehemu ya kulaza wageni ampeleke Sugu.

12. Kwa sasa Sugu yupo katika Matibabu, baada ya kupata majeraha sehemu za Mgongoni, Mbavuni, Kichwani na Miguuni sehemu ya ugoko.

13.Mwisho, sugu na Mnyika wameibiwa simu zao zote pamoja na fedha kiasi cha Dollar elfu tano na shilingi milioni 3 za Kitanzania.

Boniface Jacob (Ex Mayor)

=====

UPDATES: 1830HRS

======

View attachment 3068821
JamiiForums, imezungumza na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, anaelezea:

Taarifa za Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) pamoja na Katibu Mkuu John Mnyika ni kati ya walioumizwa wakati Polisi wanawakamata kwenye Ofisi zetu Mbeya, hatua ya sasa wameenda kwenye matibabu.

Bahati mbaya Jeshi la Polisi halikuwapeleka kwenye matibabu hata walipolalamika wana maumivu makali, Mnyika akipelekwa nyumbani kwake Dar, Sugu pia aliletwa Dar licha ya kuwa nyumbani kwake ni Mbeya. Wote hawana simu kwa sasa.

Sugu alipelekwa Hospitalini ndio lakini kama bado yupo amelazwa au ametoka hizo taarifa sina kwa sasa hadi niende nikamuone sababu hana simu.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
But why jmn?
 
Hizo dola elfu tano wamechomekea tu hapo kutengeneza msingi wa madai.
 
Nijuavyo "sugu" haidhuriki kwa kipigo.

Habari imekaa kishabiki sana hii. Labda alimletea kamishna jeuri. Maana huyo mtu ni mjinga mjinga.
 
Back
Top Bottom