Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Fuatilia kinachojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 8, leo Aprili 17, 2024.
Mbunge wa Geita vijijini (CCM) Joseph Musukuma amesema Watanzania wanaliamini Bunge, na kuna vitu vimekuwa vinazungumzwa lakini havichukuliwi kwa uzito wake na kwamba Serikali na Wizara husika zikae chini kutafakari upya suala la kikokotoo kwani linawaumiza watanzania na linatengeneza taifa la wezi.
Amesema Wabunge na Serikali isiweke pamba masikioni kwani imekuwa ni ajenda inayojadiliwa kila siku, na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Nchimbi amesisitiza suala hili lishughulikiwe.
"Nimebakiza miaka 3 na watoto wangu, natakiwa nistaafu nikajitegemee, sina nyumba nipo kwenye nyumba ya Serikali, halafu naenda kupata asilimia 30, lazima niondoke na mzigo liwalo na liwe. Kwahiyo ni vizuri tusijiwekee pamba masikioni, tuone namna ya kuwasikiliza, na kama kuna uwezekano wa kutatua hilo tatizo tulitatue" amesema Musukuma.