Nani alikuambia wafanyakazi wa serikali ukiacha wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaishi ktk nyumba za serikali bure?. Hata hao wengine tunao wanaishi huku mitaani wamepanga. Walio ktk nyumba za serikali waliobakia hulipa 10%:ya mishahara kulipia kodi. Barua zao zote za ajira hazina kipengele cha kupewa nyumba ya serikali. Wanaobahatika kupewa nyumba ni wale wakuu wa wizra, vitengo ambao ni wachache sana na mara nyingi wanatokea ktk nyumba za kupanga kabla ya UTEUZI.Yaani anmtetea mtu ambae amekaa nyumba ya serikali miaka 30 bure kashindwa kujenga ndani ya muda huo. Watanzania inabidi tujifunze wengine wanavyoishi huko.
Nchi zilizoendelea ukipata benefits zifuatazo bure, kama nyumba, gari full time, mafuta, furnishing, matunzo ya nyumba. Tax man atakwambia hizo ni ‘benefits in kind’.
Nyumba itaangaliwa thamani yake ya kukodisha sokoni utalipa percentage fulani ya market rent value kama kodi, mafuta utapigiwa bei ya mwezi unayogharamiwa utalipa kama kodi, furniture za nyumba zikizidi kiwango kinachoruhusiwa excess utalipa kama kodi.
Hakuna vya bure bure huko na bado mtu anastaafu na nyumba nzuri tu kwa sababu akiwa kwenye benefits za taasisi anaokoa hela nyingi tu. Yaani Tanzania mtu anataka kumuhurumia mtu alieishi miaka 20-30 kwa benefits luluki ambazo free.
Anahitajika mtu wa kuwabadili fikra watanzania.
Hawa huwa hawana uwezo wa kujenga nyumba ktk miaka 30 wanayifanyakazi mpaka wanapostaafu. Vitu muhimu ni kuwa na familia kuikuza kiafya na elimu kwa mishahara midogo wanayopata.
Wanapostaafu ndio hupata pesa ya kujenga kajumba. Ndio sababu wanalalamika kulipwa 33% ya kiinua mgongo halafu ile pesa ya pensheni ya kila mwezi wanapata mwisho miaka 72. Hapo unaachwa ufe. Wakubwa wanaendelea kulipwa mpaka wafe kwa kikotoo cha zamani. UMEELEWA?