Ili uelewe vizuri, tafuta salary scale za watumishi! huyo mwenye degree uliza ana staafu akiwa na level gani ya mshahara hapo ndio utajua kuwa watumishi wa umma wanapitia magumu.I get it kuna struggle in the beginning but then salary inapanda over the years. Unapostaafu bado una faida pension ina-calculate mshahara wako wa mwisho sio mwanzo.
So automatic unafaidika maana michango ya mwanzo ni kidogo na ndio miaka mingi, wakati calculations za malipo zinaangalia miaka ya mwisho hiyo hela pension fund lazima wajue wanaitoa wapi.
Halafu kwenye jamii walau watumishi wana-pension, si ajabu wote mke na mume ya uzeeni.
Huku kuna watanzania wengi sana with degree qualifications hawana ajira, zikitangazwa kuna wakati walijaribu kufanya usaili uwanja wa Mkapa nusu ulijaa vijana.
Ili watumishi wapate hiyo pension yao serikali inatumia resources nyingi sana, bado kuna changamoto za pension investments to how they work hadi ulipwe average ya miaka ya mwisho na changamoto zao za ‘cash-flow’.
Sasa sudhani kama serikali ime set hiyo withdrawal ya 33% kwa intentions za kuonea watu ni kwa sababu ya uhalisia wa cash-flow za mfuko na available liquidity ya kila mwaka ili waweze kukidhi kulipa (story ni ndefu to how they increase their assets).
Jaribu kufikiria kwa mwaka kama kuna wastaafu laki moja tu huo mzigo wa malipo sio mdogo na kila mtu analipwa kwa average ya mshahara wake wa mwisho. Kila mtu akichukua 50% ya lump-sum withdrawal sidhani kama watabaki na kitu. Na uwekezaji wao mara nyingi pension funds ni kwenye bonds za miaka mingi hizi taasisi kawaida hazina liquid assets banks wana value tu za bonds na interest earned.
Ni hivi kuna changamoto na CAG anazielezea mara kwa mara kwenye report yake, serikali imekuja na utaratibu ambao wanadhani wanaweza mudu watu hawataki kuelewa, halafu anatokea huyo msukuma anataka mpaka mijitu iliyokuwa na uwezo wa kujenga katika muda wao (wale ambao wameishi nyumba za serikali waibe kama serikali aiwezi wapa 50%).
Binafsi naona watumishi ni ungrateful
Naamini hapo utakuwa katika position nzuri sana ya ku argue basing on reality!
Haya unayoyasema ni mtazamo tu, kama motivation speakers wanavyo motivate watu without regarding reality ya kipato cha mtanzania au watumishi wa umma.
Sio rahisi mtumishi aache kulipia ada watoto, au kuhudumia familia, aanzishe project itakayo mcost lot of money wakati cash in-flow ni kiduchu, atafungwa au kufilisiwa hata hicho kidogo alichinacho.
Waulize waajiri kuhusu madeni waliyonayo, watumishi wao, ndio utajua uhalisia wa hichi tunacho jadili hapa.