kekule benzene
JF-Expert Member
- Sep 28, 2016
- 1,444
- 3,576
Hizi ndio shida za kuwapa dhamana watu wasiojua wanaowaongoza. Eti unasave laki 5 Hadi 7 kwa mwezi. Unajua mshahara wa daktari, nesi, mfamasia, walimu?Kiongozi embu tuwe wa kweli
Mtu anaishi nyumba ya serikali rent mtaani nyumba anayoishi tena sio prime area labda laki 5-7 kwa mwezi. Ndani ya mwaka anaokoa million sita mpaka nane. Mafuta gari ya kazini kwa mwezi labda matumizi yake binafsi ni łąki mbili mpaka tatu, anaokoa millioni mbili mpaka tatu ukijumlisha ndani ya mwaka, mshahara million tatu plus kwa mwezi.
Kwa mwaka anaokoa kama 8-10 million kwenye mshahara wake. Halafu unakuta mtu private na mshahara wa millioni nne au tano kabla ya 40 years ana nyumba yake bila hizo ‘benefits-in-kind’ za watumishi na wenyewe wana ndugu hao hao wakuwasaidia na kusomesha.
Ifike wakati watu waambizane ukweli, uwezi kufanya kazi zaidi ya miaka 20 serikalini huku ukipokea benefits zote hizo usiwe na nyumba hata kama hukua mpiga deal.
Nyumba ya laki 6 wakati wengine hawapati hata take home ya laki 6.