Joseph Mwasote: Kutekwa, kuteswa na kumpoteza mwana katika uchaguzi wa 2025

Joseph Mwasote: Kutekwa, kuteswa na kumpoteza mwana katika uchaguzi wa 2025

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252


Kwa takriban miaka 20, Joseph Mwasote amekuwa sehemu ya safari ya kisiasa ya CHADEMA, akipanda kutoka uongozi wa Kata ya Tunduma hadi kuwa mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya na baadaye kugombea ubunge wa Mbeya Vijijini mwaka 2020. Lakini uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, kwa maelezo yake, uligeuza maisha yake kuwa simulizi ya kukamatwa, kuteswa, kutengwa na familia, na hatimaye kupoteza mwanawe katika mazingira anayodai yanahusiana na vurugu za uchaguzi.

Akizimulia matukio yaliyompata na hali anayoishi nayo sasa, Mwasote anaeleza.

Soma pia: Kada wa CHADEMA adaiwa kutekwa

Swali: Ulianza vipi harakati za siasa mpaka ukajikuta kiongozi ndani ya CHADEMA?

Jibu: Mimi nimefanya kazi takriban miaka 20 ndani ya CHADEMA kwa sababu nimejiunga 2006. Tangu nimeingia tu nimekuwa mwenyekiti wa Kata ya Tunduma. Nilianza na umakamu nikaja mwenyekiti, nikashika nafasi mbalimbali nimekuwa mwezi nimekuwa mwenyekiti wa jimbo.

Mwisho kabisa nimeondoka 2014 nikawa mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, kabla ya Songwe haijagawanyika. Na walivyokuja kugawanya nimekuja nikamaliza nikaongoza hii mikoa yote miwili kwa mwaka miwili, nikabaki Mbeya wakati najiandaa kugombea jimbo la Mbeya vijijini Nikafanya miaka mitano tena kwa hiyo nimefanya miaka 10. Na nikagombea ubunge Mbeya Vijijini2020. Lakini pia nimekuwa makamu mwenyekiti wa kanda ya Nyasa, mwenyekiti wangu alikuwa Mchungaji Peter Msigwa.

Swali: Naomba utueleze yaliyokupata wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Jibu: Ninachoweza kusema ni kwamba mazingira niliyochukuliwa yana utata kusema nilikamatwa japo walionichukua ni polisi. Lakini mimi nilichukuliwa katika mazingira ambayo kisheria ningekuwa nimekamatwa kama kawaida, kwa muda wa saa 8 kufika saa 11 ningekuwa nimeshahojiwa, nimepekuliwa.

Sasa mimi haikuwa hivyo, mimi nimechukuliwa, nimepelekwa, wananiambia eleza... unataka kuchoma nyumba... kwa nini ulitaka kumuua mheshimiwa naibu waziri (anamtaja)?

Swali: Ulichukuliwa tarehe ngapi na ulikuwa wapi?

Jibu: Nilichukuliwa Mpemba (Tunduma) ambako nilikuwa nimeenda kuchukua gari yangu (Toyota land Cruiser) maana nilikuwa nimepata ajali, hivyo nilikuwa natafuta fundi. Nilikuwa nimetoka Mbeya nikawa niko pale.

Ilikuwa Oktoba 25, 2025 muda ya saa 8 mchana. Kwa hiyo nikapelekwa kituo cha polisi nilikuwa nimefungwa macho, kwa kutumia t-shirt yangu mwenyewe ikaizungushwa juu, lakini nikawa nimepigwa sana usoni.



Swali: Ulipelekwa kituo gani cha polisi?

Jibu: Kituo cha Polisi Tunduma. Baadaye nikaondolewa, nikapelekwa kusikojulikana kwa sababu nilikuta tu niko kwenye jumba ambalo liko wazi, juu, ni kama linamaliziwa ndani.

Nikakutana na watu wana mapanga, marungu,wakaanza kunipiga sana chini miguu. Nikatupwa kwenye kituo kidogo cha Mpemba nikiwa sijapata fahamu vizuri. Usiku nikaamka kujaribu kujivuta nikakuta siwezi kutembea siwezi kufanya kitu chochote.

Lakini bahati kesho yake Jumapili... kuamkia Oktoba 26 nikabebwa na polisi, ikaja gari kutoka Mbeya, ya polisi, kutoka ofisi ya RCO (Ofisa Upelelezi wa Jinai) nikapelekwa Mbeya ambako nako nilipitia nikapelekwa kwenye mateso.

Walikuwa wakinipiga huku wakiniuliza kwamba nina vijana wa hamasa? Kwamba mimi ni kiongozi wa hamasa. Nikajaribu kukataa wakasema bosi wako amesema... wewe ni mtu mbaya.

Swali: Huyo bosi wako ni nani?

Jibu: Alikuwa (anamtaja aliyekuwa kada wa chama hicho kabla hajahamia CCM).

Ni kweli kwamba mimi baada ya kustaafu uongozi wa chama kufuatia uchaguzi wa mwaka 2024 Nilikaa miezi mitatu nikiwa kwenye ile idara ya hamasa, kuhamasisha chama. Niliombwa niwatengeneze kikosi cha hamasa kwa ajili ya kuhamasisha chama, baadaye wananiondoa.

Kumbe wananiondoa yeye akahamia CCM Oktoba 28, 2025 jijini Mwanza, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi.

Wakati polisi wakiendelea kunitesa, walisema, bosi wako anasema hivi na hivi na hivi wewe unakataa nini? Leta vijana ulikuwa nao... Kwa hiyo nikapigwa sana. Kwa kipigo nilichopitia ndugu yangu, ndio maana nasema hawa watu wana roho mbaya sana.

Kwa hiyo nikatolewa hapo (Tunduma), nikakaa Ilomba, baadaye nikapelekwa Ruanda Nzovwe pale, nikatoka Oktoba 28, 2025 nikapelekwa Tukuyu, nikafichwa huko. Baadaye nikarudishwa Central (Mbeya) Novemba 6, 2025 nikatolewa tena usiku nikapelekwa Vwawa.

Mpaka nakuja kuhojiwa ilikuwa Novemba 24 nikiwa Mpemba. Siku zote nilikuwa sijasaini mahala, nafungiwa kwenye chumba peke yangu. Kwa hiyo hiyo siku... ndio nikawa nahojiwa, ndio naona sasa niko salama. Sasa kwa mazingira ya namna hiyo, ndugu yangu, utasema nilikamatwa? Nilitekwa.

Swali: Walipokuhoji walikwambai una kosa gani?

Jibu: Walisema nimetaka kuchoma nyumba ya askari huko Ileje. Baadaye ilionekana huyo mtu ni kama alikuwa mtu wa kutembea na wake za watu ilikuwa ni visasi. Lakini ilendio ilisababisha watoke na ghadhabu wakanipiga sana. Walinipiga bro mpaka wanamwangalia askari 'huyu jamani hata kama mnatumwa, mbona mna hasira ya kwenu tu, nimewakosea nini mimi sijafanya chochote'. wakasema mimi nataka kuua askari.

Swali: Umewahi kuwasiliana na Silinde baada ya hapo?

Jibu: Leo ukimuuliza umewahi kumpa kumpa hata pole? Hakuna. Sasa kaka... wanasema tusizungumze chochote... Unakuwa mnyonge, mtoto wako ameuawa. Wewe mwenyewe umepata vilema. Halafu leo ukitaka useme, upumue ungalau uzungumze, mtu anasema... anakutengenezea kesi na ndio maana uliona juzi nimeamua kuzungumza wazi kwamba 'Hapana, mimi najua natafutwa.

Swali: Kwa hiyo walikuachia lini baada ya kukukamata hivyo na kukutesa?

Jibu: Mimi tumeachiwa Novemba 28 na tulipelekwa mahakamani, tukatoka chini ya uangalizi, tukawa tunaripoti kwa... kwa mkuu wa upelelezi wa wilaya. Mimi nilikuwa naripoti mara mbili. Tulikuwa kama watu 10 hivi.

Swali: Mlipelekwa mahakamani mkishitakiwa kwa kosa gani?

Jibu: Hatukushitakiwa wanaita binding over, walituachia kwa maana ya tulikuwa chini ya upelelezi ya uangalizi kwa hiyo jalada letu lilikuwa linachunguzwa kwenye zile tuhuma tulizouulizwa.

Kwa hiyo tukawa hatutakiwi kufanya kosa, lakini pia kama tutabainika, tuna makosa kwenye yale, tunaweza kufunguliwa kesi. Kwa hiyo tukawa chini ya uchunguzi... Kwa hiyo jalada langu lilifungwa rasmi Mei.

Kwa hiyo mimi nilimaliza miezi mitano miezi sita hiyo nusu mwaka, tukawa tunaripoti kwa wiki kwa mwezi mara mbili. Na hatukuweza kusafiri tulimaliza hiyo adhabu.

Swali: Na vile vitu vyenu mlirudishiwa?

Jibu: Hapana. Hatujarudishiwa, na hii ndio labda nataka tu nini nini nilikuwa nataka nayo pia kama, kama kweli hawa majaji waliotoka nje, wanaweza wakashauri vizuri. Kwa sababu tume (Tume ya Jaji Mohamed Othman Chande) iliyoundwa ya kwanza... ilikutana na baadhi ya watu. Sisi hatukubahatika kukutana nayo, japo ni waathirika, lakini hatukukutana nayo.

Sasa kwa nini walibaki na hizo simu na kwa nini wako nazo? Kwa hiyo ninaamini hii tume inayoundwa saa (Tume ya Jaji Shaaban Lila) hizi itatumia chombo kile kile, kilichokuwa kinapiga, kinaumiza watu, watu wanasema uongo...

Swali: Walichukua kama shilingi ngapi?

Mhojiwa: Simu zote walichukua (simu mbili) kila kitu, hela mfukoni kila kitu... Yaani ulikuwa ujambazi. Saa yangu ikang'olewa. ilikuwa kama 500,000, simu, saa, viatu nilivyoenda navyo Mpemba baada ya kupigwa sana mguu mmoja nimeondoka hapo sina kiatu.

Nimeondoka na suruali mbili nzuri nilikuwa na koti kwenye gari, walivyozichana zote ni damu tupu wakanipa koti nikawa nimeenda nalo Mbeya.

Swali: Baada ya kuachiliwa, umekuwa ukipata vitisho vingine?

Jibu:
Ndio. Julai 7, 2026 nilipigiwa simu na RCO k wa Songwe akisema anayo taarifa kwamba mimi najipanga niko kwenye nyumba ya jamaa tunafanya vikao vya kutaka kuchoma nyumba.

Nikamwambia 'Hapana, mimi sipo'. Lakini nilimwona wakati tunajaribu kujibizana hivi kwenye message ni mtu ambaye hakutaka kuniamini.

Swali: Umesema mtoto wako aliuawa, ilikuwaje?


Jibu: Aliuawa mimi nikiwa ndani Oktoba 29 na mimi niko hoi. Kwa hiyo pale nyumbani kulikuwa vilio viwili... kilio cha kwangu na kilio cha mtoto wangu.

Swali: Na yeye walimfuata nyumbani?

Jibu:
Kwanza Oktoba 28 mtoto wangu huyo alivyo toka Mbeya inaonekana kuna watu walikuwa wakimfuatilia wakamkosa. Akarudi na kaka yake nyumbani. Walivyorudi yeye akasema Oktoba 29 mimi sitoki nje... anafua nguo.

Kuna watu walimfuata nyumbani. Wakamchukua wakasema 'baba yuko kule twende tukampiganie'... kumbe wanamuuza. Basi mtoto wangu amefukuzwa nao, watu wamefanikiwa... wakamuua.

Swali: Ikawaje baada ya hapo?

Jibu: Mtoto wangu alipigwa risasi akiwa dada yake yuko hapo ni nesi. Walipoua tu, waliwatuma wakafuta zile namba walizokuwa wanawasiliana naye, wakamwambia mtoto yule aliyemuita kwenda nyumbani... wakampeleka simu wakamwambia mama yake 'mama eeh, wamemuua Stefano'.

Kwa hiyo mama akatoka pale na dada yake na walimkuta Stephano amepigwa... kwenye paji la uso hapa pametoboka, damu zinatokea hapa kwenye mshipa. Inamwagika damu, lakini wamemvua nguo wamelala pembeni. Kwa hiyo mtoto wangu alichosema tu, anasema 'Mama, nakupenda sana, lakini nakufa leo.' Akawa amekata pumzi ya kuongea.

Dada mtu kwa sababu ana usoefu au nesi akaomba pikipiki. Akakimbia naye kwenda wakamweba wakaenda kwenye zahanati. Kufika pale dispensary wale kwa sababu walikatazwa wasichukue waliouawa kwenye vurugu zile, wakagoma.

Mtoto wangu amefia pale. Dada yake akafanya kila linavyowezekana akabeba ule mwili kwenye pikipiki wakaondoka naye... wakaenda naye mortuary serikalini pale.

Swali: Baada ya hapo mlipata fursa ya kumzika?

Jibu: Hatukuupata mwili. Bahati nzuri mwanangu yule wa kike alipofika pale zahanati alimkuta aliyekuwa pale walisoma wote. Akamhudumia haraka, akaihifadhi maiti ilikuwa ya nane. Akamweka na alama. Akarudi nyumbani.

Kesho yake wanaenda, wakakuta... hamna mwili pale. Lakini mbaya zaidi yule dada aliyekuwa pale walivyomwondoa, anasema kuna watu walikuja usiku, mwili walikuwa wanautaka hawasemi mwili wa mtoto wa China, mwili wa China.

Kwa hiyo moja ya kwanza walivunja ile CCTV ya pale ili wasijulikane. Lakini Mungu ni mwema, wapo walioona walijua walioutoa. Kwa hiyo, walitoa ule mwili usiku. Mwili ulipatikana, na kuhakiki kwamba amekufa, na mimi nilikuwa naamini kwamba, mtoto wangu atakuwa amefariki.

Swali: Swali: Kwani wewe una watoto wangapi?

Jibu: Mimi nina watoto 12 na huyo mmoja ndio amefariki sasa hivi.

Swali: Kama unaendelea kutishiwa kwa nini usitafute mahali salama labda ukakimbia nje ya nchi ili kuendelea kujilinda. Kwa nini unaendelea kubaki?

Jibu: Mimi bwana... kwanza nina maisha yangu ni magumu. Kwa sababu ya mazingira ya siasa ambayo nimeisimamia kwa muda mrefu sana. Kwa hiyo niliathirika kutafuta uchumi... sasa, uwezo wangu wa kukimbia labda nikimbilie hapo tu na... Niko wazi, niko Tunduma , kwa sababu sina uwezo, sasa nifanye nini?

Lakini, sitanyamaza, nitaendelea kusema. Kwa sababu kinaniuma. Na simkosei mtu kwa sababu sina mpango wowote mbaya, na taarifa ninazozipata ni kwamba wanaendelea kuniwinda. Kwa hiyo nipo, sina uwezo wa kwenda mbali kwa sababu ya mazingira ya kiuchumi. Lakini pia na nani, naenda wapi? Yaani hiyo ndio njia tu ya kujua unaweza ukawa mahala fulani na ukawa salama.

Swali: Kwa hiyo familia umeacha Tanzania iko Tunduma na wanaendelea tu na biashara walizokuwa wanazifanya?

Jibu: Familia iko Tunduma na watoto wangu wapo wanasoma, wengine wa msingi, wako wa sekondari... mama yupo, shughuli zangu ndogondogo wanaendelea nazo. Ndio maana unakuta hata kuzungumza ninalazimika, lakini nilitamani nikae kimya, kwa sababu hata nikikaa kimya bado naona kama ndio wananiwinda zaidi. Bora watu wajue kwamba wananiwinda. Yawezekana ikawa ni... ikawa salama kuliko kukaa kimya.

Swali: Kuna watu wamewahi kujitokeza kukusaidia?

Jibu: Kusema ukweli sina mtu yeyote. Nilipata tu jamaa, marafiki walionitumia 50,000 walionipa pole kunishika mkono kama kawaida. Lakini juu ya namna gani nitaweza niko salama, kwa kweli sina.
 
Aiseee siasa imekuwa uhasama, ndio wabunge wengi wamekuwa kama akili hawana kila jambo wanaitikia tu wanaenda kupingia chooni kwasababu ukipinga waziwazi unaenda kupimwa mkojo
 
Back
Top Bottom