Joseverest is Back!! (Hatimaye nimerudi tena)

Joseverest is Back!! (Hatimaye nimerudi tena)

Woyooooo...piga keleeeeeeee[emoji108][emoji108][emoji108][emoji108]

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Iliwahi kunitokea 2007, nilizushiwa na baadhi ya ndg wakapewa taarifa. Ilileta usumbufu mkubwa sana, aliyezusha hadi leo hana amani, nami nilimsamehe nikamwambia awe na amani kwani mimi nitaishi miaka yote niliyepangiwa na Muumba. Najua umeumia sana pole sana. Watu wajifunze kutosema wasiyo na uhakika nayo
Pole sana mkuu nami nimepoa pia, Hata mimi sina sababu ya kuwauliza kwa nini wamenizushia kifo, nawasamehe kiroho safi na maisha mengine yaendelee.. Ndio binadamu tulivyo
 
Wasalaam wakuu,

Hatimaye nimerudi tena baada ya kimya cha mwezi mzima. Natumai mnaendelea vyema na shughuli zenu hapa jamvini na hata za nje ya jukwaa. Katika mwezi huo mmoja niliokaa kimya kumeibuka 'Sintofahamu' nyingi juu yangu kwa wale ndugu, jamaa na rafiki zangu wa humu Jukwaani

Lengo la kuandika uzi huu ni 'KUWEKA MAMBO SAWA' na SIO 'SIFA' au sijui wengine mnaita 'KIKI' kwani baada ya kuingia kwenye account yangu nimekuta 'taarifa tata' zinazonihusu mimi kutoka kwa members wa hili jukwaa.. Hadi thread nimeanzishiwa kuhusu uwepo wangu, nimeona si vibaya kuweka mambo sawa yakae kwenye mstari ili kuondoa 'utata' kwa maana haiwezekani nizushiwe mambo 'AMBAYO SIO SAWA' nikae kimya tu

{ Najua zimesemwa taarifa nyingi tu ila hapa najaribu kuainisha chache tu }


Miongoni mwa taarifa hizo nilizoziona na ambazo nimezushiwa ni;
1. Nimebadili ID na avatar

2. Nimetekwa na watu wa usalama na kufichwa kusipojulikana

3. Nilienda Zimbabwe wengine wakasema Kenya kwenye uchaguzi

4. Nimemaliza kazi niliyotumwa na 'watu wa system'

5. Nipo chuo Tandabui

6. Mke wangu kanizuia kuingia JF

7. Simu yangu imeharibika au kudondokea kwenye maji

8. Nimetongoza mwanamke wa mojawapo ya mods ndio maana nimezuiwa kupost

9. Nipo Kibiti napimwa mkojo kwa ajili ya uchochezi au nipo magereza

10. Nipo nchini China/Canada kikazi/kimasomo ambapo baadhi ya mitandao ya kijamii imefungiwa (kupigwa BAN)

11. Wengine walidiriki kwenda mbali na kusema Nimefariki katika ajali ya pikipiki (iliyotokea ubungo riverside ikimuhusisha ndugu yetu Johanes [RIP])


Sasa, napenda KUKANUSHA TAARIFA HIZO KAMA IFUATAVYO kwa maana sio za kweli

1. Sihusiki na hizo ID mpya kama mbili/tatu hivi ( ya kike na ya kiume) nimeziona zinazotumia Avatar kama hii ya kwangu..Ya kwangu ni hii tu (Joseverest) hamna nyingine kwa maana siwezi kumiliki ID zaidi ya moja na sioni faida yake.

2. Sijatekwa na mtu yeyote wala kutishiwa maisha kwa namna yoyote ile ndani ya huu mwezi mmoja niliokuwa kimya

3. Sikwenda Zimbabwe wala Kenya, taarifa za uchaguzi wa Kenya nilizipata hapahapa Tanzania kupitia vyombo vya habari

4. Sina kazi maalumu niliyotumwa na hao watu wa system, mimi ni kijana najitegemea na maisha yangu binafsi na Sihusiki kwa namna moja au nyingine na hao watu mnaowaita ni wa System

5. Sisomi chuoni Tandabui, mambo ya kusoma yaliisha kitambo ila hapo mbeleni nitajiendeleza kielimu kwa neema za Mungu akijaalia

6. Sina mke au mpenzi ambae ananizuia kulog in (kuingia JF)

7. Simu yangu ipo sawa haijaharibika wala kudondokea kwenye maji

8. Sijihusishi kimapenzi na mwanamke yeyote wa mods kwa maana siwajui na haitakaa itokee

9. Sipo Kibiti kwa ajili ya kupimwa haja ndogo kwa maana sikuhusika kwa namna yoyote kwenye masuala ya uchochezi katika mojawapo ya machapisho yangu humu jukwaani, Pia sipo/sikuwepo gerezani kwa maana mimi sio mhalifu

10. Sipo nchini China wala Canada kikazi/kimasomo nipo hapahapa Nchini Tanzania


11. SIJAFA wala SIJAPATA ajali ya aina yoyote iliyotokea hivi karibuni mahala popote(Japokuwa sipingi kifo, najua kila nafsi itaonja mauti)...hadi muda huu ninavyoandika uzi huu ( Nipo Physically and Mentally Fit, nikimaanisha niko sawa kimwili na kiakili[timamu] )

Mwisho kabisa napenda kutoa RAI kwa baadhi ya watu kuwa, mtafute TAARIFA SAHIHI na sio ' Uzushi au taarifa mbaya zenye lengo la kumdhalilisha/kumchafua mtu aonekane mbaya/muongo/mfitini miongoni mwa wanajamii wanaomzunguka.

-Tuendelee kutumia JF kama sehemu muhimu na maalum ya kujifunza, kuelimika, kupata habari na hata kuburudika..
Samahani kama nimewakwaza kwa thread hii ndefu( nimejaribu kufupisha kadiri niwezavyo)

Original Joseverest ✓
167955498d25090555d3e1ce9a77eedb.jpg


Sent using Tapatalk
Swali langu moja tu kwako Jose,

Dar umepaonaje mkuu?[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Maana hiyo tarehe moja ndio ilikuwa siku yako ya kuwasili dar na kwa bahati mbaya zaidi ukapotea mazima humu jukwani.[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4]
 
Hahaha ina maana Comrade huamini kama nimerudi [emoji56][emoji56][emoji56]???
Kwanza nikupe pole na hongera kwa mihangaiko ya kutafuta ugali wa kila siku.
Na moja ya mada zilizo niletea ubishani mkubwa hadi kwa shemeji zako (anae julikana na 2 wasio julikana), ni hasa hii habari iliovuma kwamba wewe ndie yule kijana aliefariki kwa ajali ya pikipiki.
Nimefurahia ujio wako comrade.
Hii mada na I'D yako, ileta sinto faham hapa jamvini na kupelekea threads kadhaa kuanzishwa.
Karibu tena Amigo.....[emoji144]
 
Swali langu moja tu kwako Jose,

Dar umepaonaje mkuu?[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Maana hiyo tarehe moja ndio ilikuwa siku yako ya kuwasili dar na kwa bahati mbaya zaidi ukapotea mazima humu jukwani.[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4]
Dar kuzuri mkuu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwanza nikupe pole na hongera kwa mihangaiko ya kutafuta ugali wa kila siku.
Na moja ya mada zilizo niletea ubishani mkubwa hadi kwa shemeji zako (anae julikana na 2 wasio julikana), ni hasa hii habari iliovuma kwamba wewe ndie yule kijana aliefariki kwa ajali ya pikipiki.
Nimefurahia ujio wako comrade.
Hii mada na I'D yako, ileta sinto faham hapa jamvini na kupelekea threads kadhaa kuanzishwa.
Karibu tena Amigo.....[emoji144]
Nashukuru sana amigo aisee, nimeona huo uzi watu wanasema ni mimi, sio kweli wamenizushia.. Mungu amlaze mahala pema ndugu Johanes
 
Back
Top Bottom