Uchaguzi 2020 Joshua Nassari amuomba radhi Rais Magufuli kwa mabaya yote aliyomtendea akiwa CHADEMA!

Mbunge mstaafu wa Chadema Dkt. Joshua Nassari ameomba radhi rasmi kwa Rais Magufuli kufuatia mambo maovu aliyomfanyia kabla hajahamia CCM.

Nassari ambaye alikuwa akiongea kimasai amewaomba radhi wanaccm na wana Arusha wote kwa machukizo aliyowasababishia akiwa CHADEMA.

Nassari amewataka malaigwanan na wamasai wote na wananchi kwa ujumla kumpigia kura Dkt. Magufuli.

"Ninamshukuru sana kijana Nassari ni kijana anayejitambua, ebu mpe 'Mic' asalimu hapa na aombe kura kwa ajili ya wabunge wengine, huyu anajitambua alijua alikuwa amekosea na mimi Nassari nakuambia nitakupa kazi, ebu omba kura kwa ajili ya waheshimiwa hawa", amesema Dkt Magufuli.

Kwa upande wake Joshua Nassari akatumia nafasi hiyo kumuomba msamaha Dkt Magufuli, "Mh. Rais mtu anayeomba radhi ni anayefahamu tendo la ujasiri na mimi naomba leo niuvae ujasiri nije mbele yako na wana Meru kama kuna mahali nimewahi kukosea ninakuomba unisamehe, ninaomba radhi kwa niaba ya watu wa Meru, mwaka 2015 katika uwanja huu niliwaomba watu hawa wapeleke kura mahali pengine".

Maendeleo hayana vyama!

====

Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari ameomba kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuwa upinzani

Nassari alihamia CCM akitokea CHADEMA mwezi Julai 2020, miezi kadhaa baada ya kuvuliwa ubunge kutokana na kutohudhuria vikao vitatu vya bunge

Nassari amesema mambo mengi waliyokuwa wakiyasema alipokuwa upinzani yametekelezwa na Dkt. Magufuli katika muhula wa kwanza wa uongozi wake.
Wewe yohana mbatizaji umeamua kupotosha au? Mbona maelezo yako yanaonesha kuwa ameomba radhi kama aliwahi kuwakosea, hajathibitisha mojakwamoja kuwa aliwakosea
 
Cdm wao ni 28.10.2020 mapema sana wamesha wafukuza wahamiaji
Wanaowaahidi kuwapigia kura tarehe 28 ndio waliogoma kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura
28 muda kama huu tumeshamaliza jambo letu
29 mapema tunaanza celebration
 
Ndoto za wakimbizi
 
Nassari ni mmeru sio mmasai anawasemea wamasai yeye kama nani, kujua lugha sio ndo kuwa mhusika
Yale yale tu,Mnyambo kusema sio muhaya,lakini kihaya anakiongea,au Msukuma kusema mnyamwezi sio mwenzangu wakati lugha zote zinafanana,
 
Achana na kitu madaraka,hizo ndio siasa,unaangalia maslahi,
Lowasa,sumaye,Slaa,Kafulila,Dr kabolou,wote walihama sembuse Nassari.
Acha kitu njaa,
Vijana wengi humu,mkiitwa mbele Waziri,ukaambiwa umkane Mzazi wako upewe kazi ya UDC,wengi. Fasta watakamata fulsa,sembuse kusimama mbele ya Raisi.sio kwa vijana wa kizazi hiki.
Waliweza kuwa na misimamo dhabiti ni PM Salim Ahmed Salim,alikuwa balozi akiwa kidato Cha sita tu,
 
Mbunge mstaafu wa Chadema Dkt. Joshua Nassari ameomba radhi rasmi kwa Rais Magufuli kufuatia mambo maovu aliyomfanyia kabla hajahamia CCM.

Nassari ambaye alikuwa akiongea kimasai amewaomba radhi wanaccm na wana Arusha wote kwa machukizo aliyowasababishia akiwa CHADEMA.

Nassari amewataka malaigwanan na wamasai wote na wananchi kwa ujumla kumpigia kura Dkt. Magufuli.

"Ninamshukuru sana kijana Nassari ni kijana anayejitambua, ebu mpe 'Mic' asalimu hapa na aombe kura kwa ajili ya wabunge wengine, huyu anajitambua alijua alikuwa amekosea na mimi Nassari nakuambia nitakupa kazi, ebu omba kura kwa ajili ya waheshimiwa hawa", amesema Dkt Magufuli.

Kwa upande wake Joshua Nassari akatumia nafasi hiyo kumuomba msamaha Dkt Magufuli, "Mh. Rais mtu anayeomba radhi ni anayefahamu tendo la ujasiri na mimi naomba leo niuvae ujasiri nije mbele yako na wana Meru kama kuna mahali nimewahi kukosea ninakuomba unisamehe, ninaomba radhi kwa niaba ya watu wa Meru, mwaka 2015 katika uwanja huu niliwaomba watu hawa wapeleke kura mahali pengine".

Maendeleo hayana vyama!

====

Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari ameomba kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuwa upinzani

Nassari alihamia CCM akitokea CHADEMA mwezi Julai 2020, miezi kadhaa baada ya kuvuliwa ubunge kutokana na kutohudhuria vikao vitatu vya bunge

Nassari amesema mambo mengi waliyokuwa wakiyasema alipokuwa upinzani yametekelezwa na Dkt. Magufuli katika muhula wa kwanza wa uongozi wake.
Asubirie uteuzi sasa
 
Back
Top Bottom