Joti hana mpinzani kwenye tasnia ya uchekeshaji

Joti hana mpinzani kwenye tasnia ya uchekeshaji

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
10,589
Reaction score
35,268
Wadau Leo nakuja kivingine , huyu jamaa nilikuwa bado sijampata vyema , Joti ni legendary anayeishi upande wa comedy , mwamba anaweza Igiza angle yoyote unayotaka wewe. Hata script za professional jamaa anacheza vizuri Sana, kuanzia utoto , mwanamke, babu , mpaka mlala Hoi au mchungaji...jamaa pote anapita Tu fresh.

Ana uwezo mkubwa Sana hakuna WA kumfikia hapa bongo na itachukua muda kumpata mwamba kama huyu tena, nimeamua nimpe sifa zake akiwa bado hai ..... Joti asifananishwe na mchekeshaji yoyote ni kumkosea heshima Sana

Nimalizie Kwa kusema kama Una stress, huna amani, unahitaji kuburudika na hata kufurah basi angalia clip za joti nafikiri zipo YouTube .....angalizo tu huyu jamaa usipokuwa makini utamaliza hela kununua bando Kwa ajili yake.

images (49).jpeg
 
Idris Sultan!!! Huyu huyu Idris anakuchekesha kweli kuna watu bandama zenu mwazitumia vibaya.
😂😂😅😅 mkuu mimi sio miongoni mwa binadamu wanaocheka kwa vichekesho vyenye Rabsha nyingi

Eti mpaka mtu avae kidem dem au avae manywele, mara avae misuruali mikubwa au mishati mikubwa au wapigane pigane kama wale wapuuzi wa futuhi

Idriss anatumia akili nyingi sana kumchemesha mtu for me he is the best jamaa kauli mali tu utakuta umecheka ,the same to nalimi
 
Joti ni Legend ila kwa kusema anachekesha kuliko wote si kweli maana anatumia nguvu nyingi sana kukuchekesha. Kuna pure talents kuna yule SUMAKU wa Mizengwe ile ni talent, au Victaza mzee Electronic Kitambo Veta. Au the late Mzee Majuto hizo ndio pure talents hata hawatumii nguvu sikiliza maneno yao tu.
 
Mkongwe tu halafu tuseme anafit kwenye character mbalimbali ,

Hilo la kuwa mchekeshaji namba moja kuna Nalimi Joseph halafu kuna fundi anaitwa Idriss hapana Chezea mkuu
Hao wote uliowataja ni one sided na wabakuchekesha kwenye comment only , Ila huyu jamaa Joti aisee kile ni kipaji bhana , kuanzia muonekano, anavyoongea, na hata mazingira full kucheka
 
Joti ni Legend ila kwa kusema anachekesha kuliko wote si kweli maana anatumia nguvu nyingi sana kukuchekesha. Kuna pure talents kuna yule SUMAKU wa Mizengwe ile ni talent, au Victaza mzee Electronic Kitambo Veta. Au the late Mzee Majuto hizo ndio pure talents hata hawatumii nguvu sikiliza maneno yao tu.
Mzee Majuto jina lilimbeba alikuwa anafurahisha lakini sio comedian mzuri Mungu amrehemu ni kama watu wakisema Kanumba Mungu amrehemu, mimi sikuona kikubwa kwake uhalisia ulikuwa hakuna unaona kabisa huyu ana act lakini kuna watu walikuwa na wanampenda hayo ni maoni yao na naheshimu ila bado hatujapata watu waka act katika kuvaa uhusika bado, Joti yuko vizuri short video zake script zake mara nyingi wako vizuri.
 
Back
Top Bottom