mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Ule msisimko wa kampeni nzima za uchaguzi kwa kinyang'anyiro cha nafasi nyeti ya ofisi ya Rais leo haukuwepo kabisa, si tu katika mitandao maarufu ya kijamii, bali pia kutoka katika vyombo makini vya habari hapa nchini. Hii yote ni kwa sababu yule Rais Mtarajiwa, "the game changer" hakuwa na ratiba ya kufanya kampeni.
Tumeona makada wote maarufu wa chama chakavu, wakijigawanya kimkakati nchi nzima ili kuweza kujaribu kupambana na hoja kinzani. Tunawashuhudia Jakaya, Pinda, Samia, Majaliwa na makada wengine wakihangaika na kuishiwa pumzi mapema huku hawajui nini kitakuwa hatima ya maisha yao ya kisiasa.
Wakati Tundu mwana wa Lissu, yupo bado "very compromised" katika hatua za awali za siasa za kimkakati za kanda. Amefanya tathimini ya yale yaliyojili huku akiwa anaongoza kwa 65% huku akimwacha kwa mbali mgombea wa CCM akiwa na 30%, huku vyama vingine vikiambulia 5% tu.
Kwa upande wa Zanzibar, upepo umetokea wa ghafla na nyeti za mtetea CCM zipo hadharani. Siri za JMT zimewekwa hadharani na koti la Tanganyika waliovishwa Wazanzibari limeoneka si lolote bali ni ukoloni kama ulivyo mwingine wowote ule.
Sasa, sasa (kwa mnukuu Rais Mtarajiwa), uchaguzi huu wa mwaka 2020 ni tofauti kabisa kuliko chaguzi nyingine zote zilizotangulia. CCM imebananishwa kote Tanzania Bara na Visiwani. Wapigakura wawachague viongozi wao kwa njia ya kidemokrasia, ukishindikana haki itatafutwa kwa nguvu za umma, kwa kujitokeza kupinga dhuluma barabarani.