Joyce Kiria: Darasa la saba tu lakini mambo makubwa

Joyce Kiria: Darasa la saba tu lakini mambo makubwa

View attachment 48787
Mtangazaji Mashuhuri wa Kipindi cha Wanawake Live Bi Joyce Kiria leo 0603012 ameweka bayana kiwango chake cha elimu na kusema kwamba licha ya kwamba ameishia darasa la saba tu lakini ni mwanamke anayeweza kujivunia kwa mafanikio aliyonayo hadi sasa kwa kuweza kumiliki kampuni mbili ikiwemo ya Local Media Entertainment, ameyazungumza hayo na kuishia kububujikwa machozi wakati wa maadhimisho ya kuelekea siku ya mwanamke duniani aliyoandaliwa na WiLDAF katika ukumbi wa Karimjee (mtoa makala alikua shuhuda) na kusema kwamba mfumo wa elimu uliopo sasa unamkwamisha kuendeleza kipaji chake......

I am impressed and she is a living proof that higher 'formal' education is not the be-all and end-all of human existence.
 
Talk show yake ipo ki-local local, hamna u-professionalism hata chembe

Mkuu unaweza kunitajia show mbili tatu za kibongo hosted na wanawake zenye u-professionalism unaouzungumzia?!
 
Mkuu unaweza kunitajia show mbili tatu za kibongo hosted na wanawake zenye u-professionalism unaouzungumzia?!

Kwa vile ndo tu ameanza mimi sioni huo u-professionalism kuwa kama ni ishu kubwa kihivyo. Hata talk show queen Oprah wakati anaanza ile miaka ya 80 show zake hazikuwa kama zike za miaka ya 2000!

She will improve as time goes on, hopefully.
 
Mkuu unaweza kunitajia show mbili tatu za kibongo hosted na wanawake zenye u-professionalism unaouzungumzia?!

Kwa hiyo kama wote wanaboronga ndio tumpambe?

Salama Jabir ni afadhali
 
Kwa vile ndo tu ameanza mimi sioni huo u-professionalism kuwa kama ni ishu kubwa kihivyo. Hata talk show queen Oprah wakati anaanza ile miaka ya 80 show zake hazikuwa kama zike za miaka ya 2000!

She will improve as time goes on, hopefully.

Tatizo letu Watanzania tupo mbele mno kurudishana nyuma, badala tumpe mtu moyo mtu aliyethubutu kufanya kitu ili ajitahidi kufanya vizuri tunaishia kuponda bila kutoa solution.
Kwa hiyo kama wote wanaboronga
ndio tumpambe?
Salama Jabir ni afadhali
Mkuu hata kwenye vibovu kuna vyenye afadhali, Joyce kaanza kutangaza lini kulinganisha na Salam J ambaye yupo kitambo sana..Kama alivyosema NN ni swala la kumpa muda tu.
 
Tatizo letu Watanzania tupo mbele mno kurudishana nyuma, badala tumpe mtu moyo mtu aliyethubutu kufanya kitu ili ajitahidi kufanya vizuri tunaishia kuponda bila kutoa solution.

Mpaka hapo kwangu Joyce is a winner!
 
Namkubali Joyce Kiria nimemuona kwenye porogrammes za African Magic. Kuhusu kusoma asijali kwani hata kina Bill Gates,Winston Churchill, Steve Jobs hawakuwa na vyeti vya University. Cha muhimu ni upeo upeo ulionao na jinsi jamii inavyopokea mchango wako. Ila ukitaka kusoma bado una chance kwani waweza kujiandikisha QT ukapata "O" level credits then una sit private candidate exam ya Form VI. Therefter ukipata eligibility ya university waweza kuwa graduate by 2017. Na nakuhakikishia ukifika hapo utakuwa juu sana. Hata Tyra Banks amegraduate mwaka 2012 na degree ya Havard baada ya kufanya talk shows na modelling kwa miaka zaidi ya 15. Wake up Joyce and do it!! Kumbuka kuwa "What a woman has done, a woman can do"

Hio qoute zako zijakupata hapo? Mie maimuna
 
Ajitahidi zaidi asijione kafika...

Ni kweli aongeze na kashule pia kwani anayo nafasi anaweza kupiga ka QT akavutavuta itamwongezea kaconfidence. Kwani hatusomi kwa ajili ya kupata pesa pekee bali pia tunatafuta freedom kwenye maeneo mengi tu.

Halafu hili la darasa 7 mm ningekuwa yeye I'm sure nisingelisema, simaanishi kupretend la hasha, ningekaa tu kimya kwani nina uhakika kuna watu atawapoteza kwenye show yake kwa wao tu kujua kwamba yy ni std 7. I know guys ambao wako tayari kuangalia upuuzi kutoka kwa msomi lakini hawajipi nafasi kuangalia mambo ya maana kutoka kwa mjinga (kama kutosoma ni ujinga) kwani hawana huo muda wa kusikiliza na kupembua, watampotezea tu. Though pia kwa kufunguka kwake imewapa moyo wengine wasiobahatika elimu kwamba you can also make it bila higher formal education kama alivyosema NN.
 
amejitahidi kwa hayua aliyofikia.....
Ila talk show yake ipo very unprofessional.......
Hana upeo mkubwa wa kuchambua mambo....
Akiweza kurekebisha hayo atafika mbali.....
 
Ilimu muhimu sana! Kuwa na kampuni hata mia haikufanyi uwe na upeo. UPEO unaletwa na ELIMU. Tusitanie ndo maana ana inferiority. Shule kwanza na pesa baadaye.
 
Ilimu muhimu sana! Kuwa na kampuni hata mia haikufanyi uwe na upeo. UPEO unaletwa na ELIMU. Tusitanie ndo maana ana inferiority. Shule kwanza na pesa baadaye.

Unazungumzia elimu gani wewe?
 
Back
Top Bottom