JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Miongoni mwa vitu vinavyotukwamisha sisi Watanzania kupata maendeleo ya kweli, ni kutokusikiliza ushauri,
Leo Mwana JF, mwenzetu, mashuhuri na maarufu karibu kuliko wana jf wote all times, Mkuu Mzee Mwanakijiji, ametoa ushauri huu kwa Chadema, naomba msikilize



Kwa faida ya watumiaji wa bundle kwa budget hivyo hawezi kufungua video links na wale wenzangu na mimi wa kiwango cha uelewa wa chini kiasi cha kutoweza kumuelewa GT wa level ya Mkuu Mzee Mwanakijiji,
nawawekea paraphrased version, naomba kunukuu

"Nije kwa ndugu yangu Lissu...,
Lissu ni mtu ambaye anayeweza kuja kuwa rais wa Tanzania, hili sina shaka, sina shaka kabisa, na ana qualifications zote,
Jambo pekee ambalo amelikosa, na hii ninayo waambia, ndio sio sababu kubwa kwanini Lissu, sio tuu kwamba atashindwa, bali inampasa ashindwe, unisikilize vizuri.

Lisu atashinda, lakini pia inampasa ashindwe, nitakuambia kwa nini, kwasababu ndio utaamua upinzani wa Tanzania unaelekea wapi. Hili linalotokea leo hii, lilitakiwa litokee 2015, leo hii kuna mstari umechorwa mweupe kabisaa, kati ya CCM na Chadema, ile separation is very clear, watu wanaomuunga Lissu wapo na wanajua kwanini, na wanaomuunga Magufuli wapo na wanajua kwanini, Lissu atakaposhindwa, itaamua Chadema iende vipi 2025, ina ajenda gani?.

Na jambo la kwanza ambalo napenda kulisikia kabla ya mwisho wa wiki hii, baada ya Magufuli tuu kutangazwa kuwa rais,
(atashinda nimewaambia), (kwa msisitizo)
Freeman Aikaeli Mbowe, ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu chama, Lissu aijenge Chadema kwa image yake, na anataka chama cha upinzani kiende vipi.

Na nnajua (Lissu) ni mwanaharakati, na hii labda ndio weakness yake, lakini sasa ni lazima aanze kuonekana kama ni statesmanship, kuonyesha statesmanship, lazima Lissu aanze kuonekana kama kiongozi kweli wa upinzani, na hivyo aone, ni kwamba atakipokea chama hiki kabla ya mwisho wa wiki hii, na akae chini na...
mimi of course, mimi I'm always open, wakisema Bwana Ben, tunaomba uje uzungumze nasi, unatushauri vipi sasa hivi, mimi I'm very frank, mimi kwangu Tanzania ni kubwa zaidi kuliko hawa wagombea, kuliko hivi vyama vya kisiasa...


Lakini Lissu, atatakiwa aijenge Chadema, hastahili kupewe kura za pole, shukrani, hongera au asante, anatakiwa apewe kura za kuonyesha kama amekuwa kuongozi wa upinzani, na ameujenga upinzani wa Tanzania, na ana miaka 5 kuamua Chadema inakuwaje"-Mzee Mwanakijiji

Mwisho wa kunuku
My Take
Kufuatia exposure ya Mkuu Mzee Mwanakijiji, mimi naukubali ushauri huu ni ushauri wa busara sana, hivyo nawashauri wale wote wanaomkubali Mzee Mwanakijiji, na walipanga kesho wampigie kura Lissu, sasa kura hizo, waziweke akiba hadi 2025, kwa kesho, badala ya kuzipoteza kwa kumpigia mtu ambaye hata shinda, bora wampe Magufuli ambaye ndiye atamkabidhi Lissu ikule ile 2025.
Paskali
 
..mbona hizi kampeni tayari zimeonyesha kwamba Lissu is a statesman?

..kwa upande mwingine Jpm ameshindwa kuwa statesman ktk miaka mitano aliyoongoza.

..mimi nadhani tunatakiwa kufikiria mbele zaidi / beyond flyover, na midege, anayotuletea Magufuli.

..hakuna Raisi ambaye hatajenga flyovers, miradi ya umeme, etc, lakini lazima tujiulize tunajenga taifa la namna gani.

..kwa maoni yangu, ktk kampeni hizi, kwa kauli mbiu ya Uhuru, Haki, na Maendeleo ya Watu, Lissu ameonyesha statesmanship kwa ku-define Tanzania ya miaka 50 mbele.
 
Andiko lako hili Lina lengo la kuwaanda watu kisaikologia kwamba Jiwe atashinda. Pili, andiko lako hili linalenga kuwatoa watu kwenye mstari. ..Kama ilivyopangwa mechi ya Simba na Yanga stretigically kuwatoa watu kwenye main talking point.

Acha Mara moja upumbavu wako ndg Pasco. Bila HARAKATI utawezaje kuendesha siasa za upinzani ukaleta impact? Shenzi kabisa Mayala. Harakati NI LAZIMA. Statesmanship zitakuja baada ya ku capture power. Ndivyo ilivyo.
 
Back
Top Bottom