JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

Mimi binafsi sitashiriki hiyo kesho kupiga kura. Ila ninaunga mkono mabadiliko. Watanzania Wazalendo wajitokeze kwa wingi kumchagua Mh. Tundu Antipas Lissu.

Ifikie wakati tuwe na utaratibu wa kupokezana madaraka. Haiwezekani tangu Uhuru tutawaliwe na watu wale wale, vyama vile vile na mtazamo ule ule. Mabadiliko hayakwepeki nchini mwetu.

Chagua Lissu ili kuondokana na Udikteta wa CCM na Viongozi wake.
 
Natamani hawa wachambuzi waniambie, huu uhakika wa CCM kushinda unatoka wapi, na kama wana uhakika kweli hizi faulo za nini......rejea uonevu wa wazi wanaofanyiwa wapinzani, tuangalie yanayotokea Zanzibar wakati huu......Mkuu Pasco, msaada tafadhali........au nyie haya hamuyaoni?
 
Natamani hawa wachambuzi waniambie, huu uhakika wa CCM kushinda unatoka wapi, na kama wana uhakika kweli hizi faulo za nini......rejea uonevu wa wazi wanaofanyiwa wapinzani, tuangalie yanayotokea Zanzibar wakati huu......Mkuu Pasco, msaada tafadhali........au nyie haya hamuyaoni?

Ushauri mzuri sana umetolewa. TL aache kuwa mwanaharakati ili aaminiwe. Kumbuka dola haipewi kwa kila mtu kienyeji tu.
 
Mbona anazunguka zunguka hajahoji credibility ya hii tume tiifu kwa jiwe !

Jiwe kakosea mara ngapi na tume imefyata mkia?

Sababu kuu ya kuslow down traffic ya internet kuelekea uchaguzi nini maana yake?

Kwanini CCM wanaishi katika comfort zone kuwa matokeo ya urais yatolewayo na tume anayoteua rais hayapaswi kuhojiwa mahakamani?
 
Heeeeee!! Huyu lisu anaogopewa kwanini??? Hajajenga flyover,hajajenga SGR,hajatoa elimu bure nchi nzima,hajanunua ndege za nchi nk.Lakini akisimama tu kwenye kampeni kuna watu hawana amani wakati wanajinasibu wamefanya vitu vikubwa!

Halafu hapohapo ukiwambia maendeleo ya watu ndio muhimu kuliko maendeleo ya vitu wanabisha.wekezeni kwenye watu kusaidia waboreshe maisha yao wekeni mazingira mazur ya biashara kwa kuweka Kodi zisizo umiza,wapeni watu uhuru wakujieleza nakutoa maoni kwenye nchi yao muone kama na nyinyi hamta pendwa na raia.ila mkiendelea kuwekeza kwenye vitu badala ya watu mtasubili Sana kushangiliwa labda ndege na flyover ndio ziwashangilie[emoji1787]
 
Magu hashindi uchaguzi huu, tunaenda second round ndio atashindwa kabisa
Kwa NEC hii hii ya Dr. Mahera?

Kushinda uchaguzi kwa kura nyingi ni jambo moja ila kutangazwa na NEC ni jambo tofauti kabisa.

Harafu NEC yetu ina kiburi cha juu sana maana inajua maamuzi yake hayapingwi kokote Duniani

Kutakuwa hakuna haja ya kufanya chaguzi tena kwa muundo wa sasa wa NEC na Katiba yetu baada ya uchaguzi huu
 
Pascal Mayalla, wewe hadhi yako ni kutoa ushauri kwa wagombea udiwani au wenyeviti serikali za mitaa na sio rais na pia sio kwa mbunge. Umeshindwa kutumia ushauri huo wewe mwenyewe kwenye chama chako kwenye ubunge ukaruka na kura moja sasa unapata wapi nguvu za kutoa ushauri kwa mgombea urais Pascal?

Unatumia theory gani kushauri Pascal?
 
Hata kama wananchi hawaitaki hiyo dola?

"The Pareto principle states that for many outcomes roughly 80% of consequences come from 20% of the causes (the “vital few”).[1] Other names for this principle are the 80/20 rule, the law of the vital few, or the principle of factor sparsity"

Maana yake ni kuwa kuna mambo mengi duniani sio lazima wengi wapate. Ndio Dunia ilivyo
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
 
Back
Top Bottom