JTC yatembelea alama ya mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Zambia

JTC yatembelea alama ya mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Zambia

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
IMG-20250508-WA0047.jpg

TUNDUMA

Kamati ya Pamoja ya Wataalamu wa Tanzania na Zambia (JTC) inayokutana katika mji wa Tunduma mkoa wa Songwe kujadili Mpango Kazi wa Uimarishaji Mpaka wa Kimataifa imetembelea na kukagua alama za mpaka wa nchi hizo mbili kwa lengo la kuona uharibifu uliofanyika.

Mpaka wa Tanzania na Zambia una urefu wa takriban km 345 ambapo km 100 ni nchi kavu, km 189 ni mto Kalambo na km 56 ziwa Tanganyika.

Mpaka huo unaanzia alama Na. B588 (Mlima Nankugulu, wilaya ya Ileje) alama inayotengamisha Tanzania, Zambia na Malawi.

Zoezi la uimarishaji mipaka ya kimataifa ni utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Afrika kuwa, ifikapo mwaka 2027 mipaka baina ya nchi za Afrika iwe imeimarishwa.

Tanzania imepakana na nchi 10 ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, DRC, Zambia, Malawi, Msumbiji, Comoro na Shelisheli huku mipaka baina ya nchi hizo ikiwa imegawanyika katika sehemu mbili za nchi kavu na majini.
 
Ni habari njema,kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom