Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

du kwa hiyo hata wakati wa kumkamata jambazi mwenye silaha askari lazima ajitambulishe? du sheria tamu kwa bongo

sheria inasema kutokana na hali halisi polisi atatakiwa kujitambulisha au kumtaarfu mtuhumiwa anakamatwa kwa sabab gani na hii ina exception kwamba kuna makosa mengine sio lazma polisi akwambie unakamatwa kwa sababu gani
 
[IThanx much kwani at least nimepata kuelewa haki yangu ingawa najua in reality sitaipata katika mazingira haya ya utendaji kazi wa polisi wetu na mahakama zetu[/I]
 

penal code ni kanuni ya adhabu ,na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inaitwa criminal procedure act
 
UTII WA SHERIA BILA SHURUTI unavunja haki zote hizo maana utakapoanza kumwambia askari ajitambulishe tu ....utakula kichapo maana utakuwa hujatii.....
 
Nisaidieni Haki za raia akiwa amepakia basi la abiria ambalo limevunja sheria...maana mara kadhaa nimeshuhudia polisi wakikamata basi labda dereva alifanya kosa wanaambia abiria wote washuke basi liende kituoni....

2. Naomba mniambie sheria za dereva ukiendesha gari lako trafiki akakukamata labda umepita service road! faini yake, hauna fire extinguisher faini yake, hauna stika ya insurance fain yake etc
 
Ninapokamatwa na polisi na haki zote zikawa zimevunjwa na polisi ktk hizo nilizojifunza kupitia jamii forum je nini itakuwa haki yangu baada ya kuwa nimeshapigwa, nimeumizwa kisheria?
 
Ahsante sana mkuu kwa kutufumbua akili na fahamu zetu juu ya sheria katika nchi yetu ya tanzania.
 
Sheria inasemaje juu ya watoto chini ya umri wa miaka 8 kulazwa rumande kwa kosa la kushutumiwa kuvunja kioo cha gari wakicheza na mwenye gari akasisitiza watoto walazwe rumande?

Tukio hili limetokea siku ya jumapili 22 Sep. 2013 hapa jiji la Arusha na watoto hao wawili wa kiume miaka 8 na miaka 7 wamelazwa rumande pale Central Police Arusha!
 
Kuna hii nyingine.

Wengi wetu hatujui.

Nini kifanyike unapofikishwa kituoni?

UNA HAKI HIZI

  1. Una haki ya kufahamishwa, KWA MAANDISHI, si kwa mdomo, kosa au makosa unayotuhumiwa kuyafanya. Wao wanasema UNASHTAKIWA, yaani, "accused". sio kutuhumiwa, yaani "suspected". Mshtakiwa ni yule ambaye anaonekana kuwa na kosa la kujibu, kwa hiyo, pale mahakamani ndipo anakuwa "mshtakiwa", si kabla. Muhimu muelewe hili, kwamba ukiwa Police Post, wewe ni MTUHUMIWA na wala SI MSHTAKIWA. Kwani wanakuwa wamekamilisha upelelezi wao kwa kesi inayokuhusu? Wala usiogope. DAI haki yako. Ni ya KIKATIBA, kwa hiyo Jeshi la Polisi linapaswa kukupa kwa maandishi makosa unayotuhumiwa kuyafanya.
  2. Unapaswa pia, kabla ya kufika wakati wa kutoa/kuandika maelezo yako, muhimu sana, uwe umepewa ruhusa ya kuwasiliana na ndugu yako wa karibu au wakili wako, ili uweze kupata msaada wa kisheria. MUHIMU SANA. Wengi wetu tunajikuta tukifanya mambo na kukosea, halafu wao wanajitetea, MSHTAKIWA HAKUOMBA KUPEWA MSAADA WA KUWASILIANA NA NDUGU au WAKILI WAKE. Hawatakupa nafasi hiyo BILA KUIDAI!
  3. Wakati wa kuandika maelezo yako, LAZIMA kuwepo na Shahidi, ambaye ataweka sahihi yake kwenye hati ya maelezo. Vinginevyo, hati hiyo huenda isikubalike mahakamani, kwani maelezo yanakuwa ya upande mmoja tu. Askari Polisi anayeyachukua maelezo yako, bila ya kuwa na shahidi (ndugu au wakili) hawezi kuaminika, lazima kuwe na mtu au watu wengine, watakaothibitisha kwamba maelezo hayo ndiyo sahihi, wakati yatakapotolewa mahakamani. Watu wengi wamejikuta wakiwa hatiani kwa kuwa tu maelezo yao yaliandikwa upya na sahihi yao kughushiwa, ikaonekana kwamba kile kilichoandikwa humo ni kile walichoandika wao.
  4. Jeshi la Polisi HALIRUHUSIWI kumweka mtu yeyote kwenye ulinzi kwa zaidi ya saa 24. Kama wakizidisha basi hilo ni kosa kwani linaenda kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai!

Kwa leo naishia hapo.

Tutaonana tena, Mungu akipenda.
 
Kuna tukio limetokea la msimamizi wa kituo cha ukaguzi wa mazao pamoja na mazao ya misitu kilwa kuwekwa ndani kwa masaa zaidi ya nane na baadae kuachiwa kwa dhamana. Na kwamba kaambiwa kwa sasa yupo chini ya dhamana kwa muda usiojulikana. nijuavyo mtuhumiwa anapaswa apelewe mahakamani ndani ya masaa 24 bali huyu afisa kapewa dhamana na polisi wakati upelelezi ukiendelea.

Naomba ufafanuzi iwapo alichotendewa ni haki
Naelezo ya ziada nimeyaweka hapo chini

Tukio lenyewe lilikuwa hivi, msimamizi wa kituo alipewa taarifa kutoka kwa mlinzi wa kituo cha ukaguzi kuwa mlinzi wa kituo amekamata mtu akiwa na silaha na hizo nyara wa serikali. Baada ya kupata taarifa hizo msimamizi huyo alitimiza wajibu wake kwa kumpigia askari mhifadhi wa wanyama pori tukio hilo na haikuchukua muda askari huyo wa wanyama pori alifika na kukabidhiwa mtuhumiwa pamoja na mali zilizokamatwa. Na inasemekana jangili huyo alitaifishwa mali alizokutwa nazo pamoja nakulipishwa faini na ofisi za wanyama pori. Hii ilitokea miezi miwili iliyopita.

Wiki hii mkuu wa wilaya ya kilwa ametoa agizo kukamatwa Yule msimamizi wa kituo pamoja na yule askari wa wanyama pori. Sababu za kukamatwa kwake inasemekana mkuu wa wilaya kapata taarifa kutoka kwa yule jangili kuwa katika mzigo uliokamatwa kulikuwa na risasi 20 ambazo waliokamata mzigo ule hawakuzikabidhi. Cha kushangaza ni kuwa yule mlinzi wa kituo aliyemkamata jangili na ndiye aliyetoa ushahidi wa vitu vilivyokamatwa hakusema kuwa aliziona risasi, bali pia huyo mlinzi yuko huru wala hajatuhumiwa kwa kosa lolote. Aliyekamatwa ni yule aliyepeleka taarifa za tukio la kukamatwa jangili akiwa na silaha pamoja na nyama pori kwa askari husika wa wanyama pori kuwa ana kesi ya kujibu.

Kwa ufupi inaonyesha mkuu eidha kapewa taarifa potofu zitakazosababisha mtu aishi kwa mashaka bila ya sabubu za msingi au anashiriki kuwalinda majangili, kwani sisi wananchi tayari tuna mashaka na utendaji wa aina hii kama tunavyoamini ukiwa ndani ya serikali ya KIFISADI lazima ule na mafisadi. Bali ukitaka kujifanya wewe ni MUADILIFU mfumo utakuumiza kwani utaonekana wewe ni adui wa mfumo. Kwani yule jangili na wale watumishi waliohusika moja kwa moja na sakata hili wako huru. Bali yule aliyekamatwa na kupewa dhamana ambayo haijulikana atashitakiwa lini au atakuwa huru lini kwa sasa yupo mashakani. Na inasemekana anafanyiwa mizengwe ya kusimamishwa kazi.
 
juzi nilienda kumdhamini mtu polisi wakati nakuta mtuhumiwa anahojiwa na Askari zaidi ya watano tena kwa ukali sana kiasi ambacho mtuhumiwa kapaniki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…