Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Polisi aje kijinga bila kufata sheria zao, aje kutak kunipekua kwangu bila kibari au utaratib maalum…? Anikamate bila warant wakati sipo kwenye kosa nitajihami aisee,, akiomba back up ya wajinga wenzie waje tu, watakuta kun back up yang somewhere pia...kama law enforcers wanavunja sheria unawachap mtakutan mahakamani.
Mambo hayo kwenye taarifa ya habari huishia....askari wetu walilipiga risasi jambazi hilo lilipoanza kuwashambulia kwa silaha (haitajwi hapo hata kama ulijitetea kwa kijiko)
 
Labda sio askari wabongo ukijifanya unajua sheria watakuua siumeona kwa lipumba mtuambae anaheshimika katika taifa alicho fanyiwa sembuse mlalahoi haki iko mahakamani pekee ili police wana sheria zao

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Na kweli mwenye hy jeuri ni tajiri tuu maskini ataambulia virungu tajiri wataanzia wp?wanajua wanaweza kupotezwa

Tajiri anaweza kusema twende panda kwenye gari yangu huku ana drive hana shaka
 
hapa bongo askari wetu hawa walochangwanywa na joto la kwenye kota za mabati,watakuvunja kiuno.
 
Kama unataka uvunjwe ugoko na kupotezewa korodani just apply them and see.

Policemen aren't people,they're just creatures of their own specie.
 
Kati ya vitengo ambavyo vyatakiwa kuvunjwa vunjwa na kuundwa upya basi ni jeshi la polisi. Ni watu hovyo sana
 
Sexer

we sio mwanasheria ni kanjanja, utasababisha wenzio waumizwe bure! taja hivyo vifunga vya cpa na uongelee pia police force and auxiliary act, Acha ubabaishaji.
 
Last edited by a moderator:
Kama kina kitu ambacho kinanisgangaza kuliko kitu chochote katika jeshi hili LA polisi ni vituo vyao!yani hua nashindwa kuelewa kwanini serikali yetu inashindwa kujenga vituo vyenye hadhi!
 
USINYANYASWE WE NDUGU FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.
 
Thanks mkuu,raia wengi hupata shida na kunyanyaswa na hawa jamaa,kwa kutojua hako yao
 
Ha ha.haaaaa. Police hawajui wajibu wa kazi yao. Wao ni kupiga raia tu. Hasa maandamano. Lkn ambush za majambazi waoga . Wanasingizia mafuta ya gari hayatoshi. Ha haaaa.
 
hawa maaskari wanaovuta bangi na kula miraa huku mitaani hayo walaaa hawayatambui, vichwa vinakuwa bangi oriented na walishapewa go ahead ya kupiga tu!!! teh teh Tanzania zaidi ya uijuavyo. atakayekamatwa akadai hayo ni tajiri tu, masikini sie utapigwa tu na kashtaki uone cha moto.

Hapo umenena namtoa mada kwanza angalie hao polisi wanvyo vunja haki kwenye mandamano Kwanza wenyewe ndo wavunja sheria
 
Tatizo ni pale hata huyo askari mwenyewe hazijui hizo sheria na haki. Zipo lakini hawazisomi. Ukimueleza vizuri, utashangaa yeye anakuliza wewe sasa tena kwa mikwara... arooo hizo sheria za wapi, unanifundisha kazi. Ki ukweli hajui.
 
hizi sheria za marekani unaleta bongo mkuu?

sitatake tuuliwe

nakumbuka kuna matapeli walienda police central mwanza wakachukua maasikari kwenda kukagua simu za sumsung maduka ya mwanza eti wametoka sumsung makao makuu watu wakachukulia masimu zao na hela wakatoa za kutosha
jamaa walikusanya si chini ya m 30 eti za faini kuuza simu feki

wanakuja kushituka ni matapeli watu walishahama mwanza
 
Back
Top Bottom