Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

USINYANYASWE WE NDUGU FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.

Kwa mfano Traffic akinikamata akaniomba Leseni na sina kwa muda huo najua unaweza kuipeleka within 24hrs. Je sheria inasema uache gari mpaka utapopeleka Leseni?
 
Kama kuna nay Statute inayoonyesha naomba muiweke hapa tuweze download na kujisomea.
 
Hao polisi wa marekani siyo tanzania kwanza kabla ya swali kofi
 
Ukidakwa na polisi cha kwanza ni kujipiga Tanganyika jek mengine ndiyo yanafuata
 
Mmh! Bac sawa kwa kutujuza tatizo mamwera wa kibongo hawanaga izo kwanza ukikamatwa tanganyika jek inahuc utaanzia wap kuuliza maswali hayo
 
Polisi Wenyewe Haki Za Raia Hawazijui!! Wao Wanachokijua Ni Vipigo Tu!! Na Upelelezi Wao UMEEGEMEA Kupiga Watuhumiwa Na Kuwalazimisha Kukiri Tuhuma Wanazotuhumiwa Kwa MATESO!!!! Wakifikishwa Mahakamani Ushaidi UNAKOSEKANA!!!! Ila Ndio Hivyo Tena Mtuhumiwa Anakuwa Kilema!!
 
My Take ,

Police wetu watii sheria bila shuruti kwanza ndipo nasi tutatii kwa uzuri zaidi ila wao hawatii sheria ana hawazijui sheria Police wamejisahau as if wao ndio wako juu ya sheria wakati wao ndio wanapaswa kukupa mwongozo uitambue haki yako ukiwa Police.
 
Back
Top Bottom