Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inawezekana kifungu hakina makosa, labda aliyeandika hapa kwenye jukwaa ndiye aliyekosea transcription...yale yale ya "kafa Manzese mazishi Sinza, mchicha mbichi mpishi mbishi!", unapoyatamka, ni rahisi kuchanganya ulimi kama hauko well composed.Hivi muandishi wa hiki kifungu amedhamiria kuandika kilichoandikwa ama la?
Kimsingi amesema mtu asikamatwe au kupekuliwa na polisi baada ya saa 12.30 jioni na kabla ya saa 12.30 alfajiri ila tu pale kutakapokuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua au kumkamata baada ya saa 12.30 jioni na kabla ya saa 12.30 alfajiri kunaweza kuleta madhara.
Kwa hiyo asipekuliwe wala kukamatwa katika muda huo mpaka pale kutakapokuwa na ushahidi kwamba kutakuwa na madhara, tunatafuta madhara kwa nguvu, nani kaandika utumbo huu?
When we are talking about rights simply means the basic and necessary criterion that should be provided or considered during undertaking any legal activities. So it have to be obeyed and being obligatory the problem is, majority of Tanzania are feel inferior when aimed to proceeds for their rights .......Hao polisi wa marekani siyo tanzania kwanza kabla ya swali kofi
yaani wakikudandia bora uwe mpole tu, hawaoni hasara kukuwekea vipisi vya bangi ukijifanya kufuata sheriaembu kwanza kamatwa na askari wetu hawa alafu ufanye hivyo unavyodai wewe uone kama utakuwa salama???
fanya hibyo alafu uone kama utaweza kushika hiyo keybody yako ulwte mrejesho hapa..!!!
Shukurani nyingi kwa wote mlioandaa hii elimu,
Elimu yenu imekuwa faida kwa jamii nzima. Mungu awabariki zaidi.
Ni elimu nzuri, lakini kwa wenzetu si hapa, jeshi linaendeshwa kwa mihemko ya kisiasa, husuda ,na visasi kati ya raia na askari.
Hakuna nidhamu ya kazi.
Mkuu hata polisi wenyewe sidhani kama wanazifahamu hizi taratibu.Kama waliweza kuzuia msafara wa viongozi wakuu wa upinzani kwenda kumzika Mzee Kisumo...Na hakuna sheria inayosema hivyo na kwenye huo msafara palikuwa na Manguli kama Lowasa, Ndesa pesa na wengine na wote wakakubali yaishe...Sembuse wewe raia wa kawaida hakika watakuua tu na hakuna kesi....Askari wengi hufanya kazi bila weledi ama kwa kufuata order..Wacha uonekane muoga uwe salama .
Mkuu naamini wanazifahamu sana ila unajua kule hufanya kazi kwa order wakiamini wako ya sheria sitaki kusema sana ila kumbuka yule mwandishi wa habari aliemiminiwa risasi akageuzwa butcher...Unadhani ni bahati mbaya tu ilitokea ile?Mkuu hata polisi wenyewe sidhani kama wanazifahamu hizi taratibu.
Mkuu, hata mimi nina utata na taratibu za hawa jamaa wa barabarani, naongezea swali, je ni haki yangu kutompa traffic police anapoiomba/ ihitaji leseni yangu, je nikimuonyesha tu bila kumpa aishike nitakuwa nimetenda kosa?Naombeni msaada wataalam wa sheria,
Je natakiwa nifanye nini ninapokamatwa na trafiki polisi,
au yeye polisi anatakiwa afuate utaratibu gani pindi anapotaka kukagua gari / anapokuta kosa lolote kwenye gari? au chombo chochote cha moto kitumikacho barabarani.
Nami kama raia wajibu wangu ni upi pindi ninapokutwa na kosa lolote lile.
Ntashukuru kama ntaelekezwa hatua kwa hatua kama mlivyoelezea hapo kwenye kukamatwa na kukaguliwa na polisi nyumbani.