USINYANYASWE WE NDUGU FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI
IMEANDALIWA NA MAWAKILI WETU
( 1 )Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
( 2 )Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
( 3 )Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
( 4 )Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
( 5 ) Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
( 6 )Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
( 7 )Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
( 8 ) Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
( 9 )Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
( 10 )Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
( 11 )Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
( 12 )Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
( 13 )Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
( 14 )Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
( 15 ) Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
( 16 )Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
( 17 )Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
( 18 )Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
( 19 ) Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
( 20 )Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
( 21 )Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
( 22 )Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.
Kutoka: Sheria Yakub Blog: USINYANYASWE NDUGU