Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Mkuu, hata mimi nina utata na taratibu za hawa jamaa wa barabarani, naongezea swali, je ni haki yangu kutompa traffic police anapoiomba/ ihitaji, je nikimuonyesha tu bila kumpa aishike nitakuwa nimetenda kosa?

Natamani kweli kupata majibu ya haya maswali yote , ksb polisi wa barabarani ni kero mno.
Nikipata maswali ya majibu haya ntahakikisha nayaprint na kuyaweka kwenye wallet yangu. Nikikamatwa tu nayapitia ili niende sawa na hawa polisi.
 
Mkuu naamini wanazifahamu sana ila unajua kule hufanya kazi kwa order wakiamini wako ya sheria sitaki kusema sana ila kumbuka yule mwandishi wa habari aliemiminiwa risasi akageuzwa butcher...Unadhani ni bahati mbaya tu ilitokea ile?
Mkuu bado point yangu iko pale pale kwamba huenda hawana uelewa unaotakiwa ukizingatia uzoefu na uelewa wa kazi unazidiana na kutofautiana kutoka polisi mmoja hadi mwingine kutokana na uzoefu wa kazi na muda waliodumu kazini. Ni sawa na kumpa dereva mpya mwenye leseni ya daraja D aendeshe lori kubwa lililobeba mzigo mzito na kumwambia asafirishe mzigo kwenda mbali, matokeo yake unayajua. Kijana yule wa polisi alikuwa na umri wa miaka 23, na kwa vyovyote utakuwa umejua uzoefu wake kwenye field za kipolisi ukoje.
 
Mkuu, hata mimi nina utata na taratibu za hawa jamaa wa barabarani, naongezea swali, je ni haki yangu kutompa traffic police anapoiomba/ ihitaji leseni yangu, je nikimuonyesha tu bila kumpa aishike nitakuwa nimetenda kosa?
Polisi Wa Usalama Barabarani Anaruhusiwa Kisheria Kukagua Gari Yako Kama Inamakosa Kadha Wa Kadha. Kama Sehemu Alokusimamishia Ni Porini Na Unatia Shaka Na Maeneo Hayo Usisimame Bali Nenda Katoe Taarifa Kituo Cha Polisi Kilichopo Mbele Yako.

Kuhusu Leseni Ni Haki Yake Kisheria Kukuuliza Maana Leseni Si Mali Yake Na Wala Si Mali Ya Dereva Bali Ni Mali Ya Serikali Ambapo Muhusika Amepewa Na Anaweza Kunyang'anywa Kisheria Pale Avunjapo Sheria.

Anapokuuliza Na Kuihitaji Leseni Yako Unapaswa Kumpa Na Kama Atafanya Kinyume Basi Fuata Utaratibu Wa Kisheria Ili Hatua Za Kinidhamu Zichukuliwe.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Mtoa Uzi Umegusa Na Kueleza Mambo Mazuri Sana Japo Wengi Wetu Pengine Tumejua Nini Askari Anatakiwa Afanye Na Si Nini Nasi Raia Tunatakiwa Tufanye.

Kwanza Kabisa Lazima Tutambue Kwmb, Askari Hawa Wameajiriwa Na Hawajajiajiri So Wanapaswa Kufanya Kazi Kwa Mujibu Wa Sheria.

Yote Alozungumza Mtoa Uzi Yamegusa Sheria Ya Mwenendo Wa Makosa Ya Jinai (Criminal Procedure Act), Lakn Ambacho Ningependa Kuwasihi Wasomaji Wote Ni Kwmb, Utendaji Wa Polisi Unaendana Na Uhalisia Wa Matukio Japo Makaratasi (Sheria) Inaweza Kusema Hivi

STORI FUPI.
Mzee Mmoja Alimkuta Kijana Alomaliza Elimu Ya Juu Anakunywa Maji Yasochemshwa, Maongezi Yakawa Hivi.

Mzee, We Kijana Unakunywa Maji Yasochemshwa Inamaana Tangu Pri School Mpaka University Hujajifunza Madhara Ya Kunywa Maji Hayo?.

KIJANA Akajibu, Ni Kweli Mzee Nilijifunza Lakn Kwa Kujibia Mtihani.

NINI MAANA YANGU.
Wakat Mwingine Sheria Inaweza Kusema Hivi Lakn Uhalisia Wa Tukio Kwa Muda Muafaka Upo Very Tofauti.

MTOA UZI KASEMA (SHERIA INASEMA)
Msachi Mtu Day Na Si Night.

MIFANO KADHAA.
MFANO No.1
Matharani> Tukio Limefanyika Day Maeneo Ya Kinondoni Lakn Taarifa Za Kiintelijensia Zinasema Silaha Imefichwa Mbezi Kwa Mzee Fataki.

Unataka Unambie Polisi Watasubiri Mpaka Kesho Ifike Ndio Wasachi Ili Kuepuka Kuvunja Sheria?.

MFANO no.2
Ktk Kugombana Na Mkewangu Nikamuuwa Kwa Bastola, Majirani Wametoa Taarifa Polisi Kisha Polisi Wakamkamata Mtuhumiwa.
Baada Ya Mtuhumiwa Kuulizwa Silaha Ikowapi? Anagoma Kutaja Ilipo.

Kumbuka Hiyo Nyumba Mtuhumiwa Anaishi Na Watoto Wake Ama Ndugu Pengine.
Je, Polisi Watasubiri Mpaka Pakuche Ndio Wakasachi Hiyo Nyumba Kuipata Silaha?.

Sipingani Na Mtoa Uzi Hata Kidogo Balia Najaribu Kueleza Mazingira Ambayo Kimsingi Yanaleta Uhalisia Wa Sheria Kutofuatwa Kwa Nia Njema Tu.

CRIMINAL PROCEDURE ACT
(MODES OF ARREST)
Topic Hii Inazungumzia Jinsi Askari Anavyotakiwa Kumkamata Raia.
1. Ajitambulishe.
2. Amueleze Kosa Lake.
3. Amshike Bega Kwendanae Kituoni.

Tuchukulie Wewe Ni Askari, Umeenda Na Wenzako Kukamata, Mnafika Mnajitambulisha Au Kabla Hamjajitambulisha Mnakutana Na Mawe Au Visu Au Hata Silaha Za Moto. Je Wewe Kama Askari Utajitambulisha Kumkamata Muhusika?.

Wanasheria Wanafanya Kazi Nzuri Sana Ya Kutufundisha Sisi Haki Zetu Lakn Wanachoshindwa Kueleza Ukwel Ni Tukio Na Mazingira Yake.

HITIMISHO.
Shuleni Nilijifunza Kwmb Nikinywa Maji Yasochemshwa Nitapata Kipindupindu, Amoeba etc, Lakn Yote Yale Yalikuwa Ya Kujibia Mtihani (Nadharia)
Leo Nakunywa Maji Yasochemshwa Coz,
1. Sina Pesa Ya Kununua Mineral Water.

2. Nyumban Zipo Kuni/Mkaa Wa Kupikia Na Si Wa Kuchemsha Maji.

3. Maisha Ya Shulen Yalikuwa Makaratas Lakn Leo Naishi Uhalisia.

4. Nipo Ktk Mazingira Magumu, Wakat Mgumu, Nitakunywa Maji Yap?

MASWALI
Nani Alitegemea Kuwa Atakuwa Bar Maid?.

Nani Alipenda Kuishi Maisha Ya Taabu Leo?.

Nani Alienda Chuo Cha Uhalifu Akapewa Na Cheti?.

Uhalisia Ni Bora Kuliko Makaratasi Ndio Maana Hata Sheria Ina Criminal Liabilities Kwa Dhumuni La Kutambua Mazingira Halisi Ya Tukio Ili Kumlinda Mshiakiwa Kama Hakuwa Na Nia Ovu.

Aksante
 
Japo amepangilia vizuri lakini ameshindwa kujua askari anapokuwa kwenye uniform anaweza kukumata bila hata kitambulisho ili mradi kosa limefanyika
Halafu pia sioni kama kuna uwezekano wa kumshtaki polisi aliyekudhalilisha, maana ndio yale ya kesi ya ngeredere anapelekewa nyani.
 
  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
Asante sana, ingependeza kuandika kwenye magazine ili watu walio wengi zaidi wapate kitu.
 
Safi sana, tusaidie kuandika kwenye magazeti ili watu walio wengi wapate fursa ya kusoma na kujua haki zao
 
Askari wetu hawafuati hizi sheria sio kwa kosa lao, hapa ntailaumu serikali, maaskari wanapata mafunzo ya ovyo, wanarush~rush tu then wanaingia kazini, wangekua wanafundishwa vizuri hizi sheria na kuzikazia ili umuhimu wake uonekane wangezifata, tena walitakiwa wachukuliwe hatua za kisheria kama wataenda kinyume, maaskari wangezifata hizi kirahisi tu. Watu nao inabidi watangaziwe hata kwenye tv mara kwa mara wajue, na iwepo institution ya kuwatetea wananchi ambao wamekua victims wa askari wasiofuata sheria.

Serikali yetu kama sasa hivi inakaribia kua ka ya kidikteta hili haliwezekani, kauli za "kamata kwanza tutafix baadaye" hizi sheria zitabaki kwenye karatasi tu.
 
USINYANYASWE WE NDUGU FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI
liftarn_Police_brutality.png


IMEANDALIWA NA MAWAKILI WETU
( 1 )Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
( 2 )Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
( 3 )Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
( 4 )Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
( 5 ) Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
( 6 )Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
( 7 )Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
( 8 ) Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
( 9 )Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
( 10 )Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
( 11 )Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
( 12 )Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
( 13 )Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
( 14 )Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
( 15 ) Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
( 16 )Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
( 17 )Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
( 18 )Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
( 19 ) Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
( 20 )Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
( 21 )Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
( 22 )Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.

Kutoka: Sheria Yakub Blog: USINYANYASWE NDUGU
Great
 
Hizi taratibu zipo lakini sijui hawa polisi wa kwetu huwa hawafundishwi wakiwa chuoni!!! au sijui inakuwaje?
 
Askari wetu hawafuati hizi sheria sio kwa kosa lao, hapa ntailaumu serikali, maaskari wanapata mafunzo ya ovyo,
Serikali yetu kama sasa hivi inakaribia kua ka ya kidikteta hili haliwezekani, kauli za "kamata kwanza tutafix baadaye" hizi sheria zitabaki kwenye karatasi tu.
Naona watu wengi mna mihemuko na hamfahama maana ya USALAMA
pale Kituoni na mahali salama kwa kujielezea na kuomba hifadhi km umeharibu URAIANI
Kuna siku rafiki yangu alipata pesa nyingi ghafla akanipeleka Grocery akaniambia niagize chakula na kunywa nitakavyo yeye yupo.
Kwa vile ana pesa nilifanya hivyo deni likafika zaidi ya 30,000/=
jamaa akasepa nyuma ya banda akiagiza nitajilipia
wahudumu kweli walidavua nikavumilia hadi nilipoona askari POLISI ambaye nilimuomba msaada anipeleke Dukani kwangu nikawalipe hao wahudumu, kufika Dukani nikakuta jamaa kafika na kukomba hela eti kuja nikomboa kumbe kalala mbele tena.
nilikopa jirani lakini ilibidi niende POLISI kufungua faili wakagoma kupata ushauri kwanza nako mm nikagoma bora nilalae hapo maana NITAUA
POLISI walinisaidia tukafanikiwa kumkamata tapeli wangu lakini aligoma kila kitu kulipa.

tutafikatu ahsante kwa hii. Ukituletea na ya traffic itakuwa umetusaidia kutii sheria bila shuruti
Mfano hai wa 2
Taffik ni wasaidizi wazuri kwa Maderevana wanaokoa mm sioni mnawalaimu labda hamjapata matatizo baranarani
si gari zote zina breki, taa au kioo kuwa na crack
si gari zote zina Bima, Road Licence
nalifika kwenye Traffic Light za TAZARA naelekea kulia Nyerere rd malori ya azam yanatoka nikafuata sheria km mwenzangu alivyosimama mara wa nyuma kanigonga na nikaserereka kumgonga mwenzangu wa nyuma kaindika taa zilipowaka mimi na niliyemgonga tutnatakiwa tuandikiwe nimlipe kwani nimemgonga kwa nyuma, Traffic walikuwepo wakasuluhisha twende Kituoni km hatutaelewana, Busara zikatumika jamaa akanisamehe akasepa mm nazubaa hapo Tazara mara Majembe wakaniambia Wrong Parking twende TAMESA km huna 50,000/
kweli niliwarudia Traffic watoe msaada zikanitoka tena na DAR sirudi tena
lkn bila Traffic wenye gari ndogo hatutaendesha
Hizi Sheria zikifuatwa bila uBINADAMU tutamalizwa msidanganywe na wanasheria ni WALAJI kuliko POLISI
 
Naona watu wengi mna mihemuko na hamfahama maana ya USALAMA
pale Kituoni na mahali salama kwa kujielezea na kuomba hifadhi km umeharibu URAIANI
Kuna siku rafiki yangu alipata pesa nyingi ghafla akanipeleka Grocery akaniambia niagize chakula na kunywa nitakavyo yeye yupo.
Kwa vile ana pesa nilifanya hivyo deni likafika zaidi ya 30,000/=
jamaa akasepa nyuma ya banda akiagiza nitajilipia
wahudumu kweli walidavua nikavumilia hadi nilipoona askari POLISI ambaye nilimuomba msaada anipeleke Dukani kwangu nikawalipe hao wahudumu, kufika Dukani nikakuta jamaa kafika na kukomba hela eti kuja nikomboa kumbe kalala mbele tena.
nilikopa jirani lakini ilibidi niende POLISI kufungua faili wakagoma kupata ushauri kwanza nako mm nikagoma bora nilalae hapo maana NITAUA
POLISI walinisaidia tukafanikiwa kumkamata tapeli wangu lakini aligoma kila kitu kulipa.

Mkuu unatetea polisi kwa kua wamekusaidia kesi moja, kwa hiyo kesi yako moja, wapo walioumizwa kumi kwa hiyo kama kitu hakijakutokea wewe usigeneralize, ukweli ni kwamba hawa polisi wengi wao wana piga kwanza alafu story baadaye, hawafati hizi sheria zilizoandikwa hapo juu.

Wapo mapolisi wanaojielewa, ila sio wengi kama unavyotaka tuamini. Ni vitu tunaona wazi tu kwa macho hata sio story za kijiweni.
 
Back
Top Bottom