Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Lakini polisi wetu hawajui huio utaratibu wao wakifika ni "kaa chini" na kufuatiwa na virungu kisha wanakwambia utajibu mbele
Polisi akikuambia Kaa chini kwann tu usikae, kwani ukikaa unakufa?
 
Police force(force=nguvu), jiandae kukumbana na nguvu pale inapobidi... Hakuna namna
 
Polisi akikuambia Kaa chini kwann tu usikae, kwani ukikaa unakufa?
Sasa virungu na vya nini? Lazima ajitambulishe na asema kwanini anataka kunikama na kwa kosa gani. Mambo mbengine haya hitaji nguvu ni kumwambia tu mtu aende mwenyewe kituoni anahitajika lakini wao ni nguvu tu!
 
Police force(force=nguvu), jiandae kukumbana na nguvu pale inapobidi... Hakuna namna

Hii ideology ndio maana hatuendelei, nguvu pale inapobidi sijakataa, ila situations za kutumia nguvu ni kama mtu ana silaha, ila kukamata watu ovyo na kuanza kuwapiga huku bado hawajahukumiwa its stupid na mtu mwenye akili mbovu ndio ataona ni sawa.
 
Weka na option zake kuna watu wanakalili hivyo hivyo ulivyoandika kwa mfana issue ya masaa ishirini na nne kama upelelezi haujakamilika inakuaje na kama ukikamatwa ijumaa kuu inakuaje maana kuna siku nne za mapumziko na watu wanakalilo tu 24!!!!&
 
Hii ideology ndio maana hatuendelei, nguvu pale inapobidi sijakataa, ila situations za kutumia nguvu ni kama mtu ana silaha, ila kukamata watu ovyo na kuanza kuwapiga huku bado hawajahukumiwa its stupid na mtu mwenye akili mbovu ndio ataona ni sawa.
Msiwafanganye Raia wema na Ideology zenu za kale nipe maana ya kituo cha USALAMA ungekuwa dereva aliyeleta ajali au uliyesingiziwa uhalifu km mgoni au mwizi kumbe unasingiziwa ndipo ungeona Kituoni POLISI ni peponi
Bila Traffic gari ndogo na pikipiki zisingekuwepo
Bila Fraud Officer huko makazini usingebaki kitu
Hakuna watu wabaya km wanasheria Advocate maana wanaomba / wanadai hela kuliko POLISI

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 

Mkuu we polisi nini? Kama hujawahi experience kitu tulia, sio kila unayeongea naye JF ni hooligan, naona una shida na wanasheria, hapa tunaongelea kitu tofauti usigeuze mada
 

Mimi naombeni tu mnisaidie zinapatikana wapi kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mkuu we polisi nini? Kama hujawahi experience kitu tulia, sio kila unayeongea naye JF ni hooligan, naona una shida na wanasheria, hapa tunaongelea kitu tofauti usigeuze mada
Kwani ww ni Moderator
Mnawadanganya raia kujifanya maBushlawyer
Msidhani kila muelewa atauendekeza uongo wenu kituoni ni pahali pa USALAMA WA RAIA Duniani pote hakuna sehemu salama palipochagululiwa km hapo kabla ya kufika Mahakamani

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
mkuu asante sana kwa thread nzuri kama hii. naomba pia nifahamu ni hatua gani ambazo mtuhumiwa anaweza kuzichukua endapo askari polisi atakiuka moja kati ya taratibu hizo..........mtuhumiwa anapaswa kumchukulia polisi hatua gani???????
 
**NJE YA MADA KIDOGO**
Kutokana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya wagonjwa walio katika hali mbaya kwenye hospitali mbalimbali hapa nchini kutokana na kuugua magonjwa yasiyokuwa na tiba na wao kuendelea kuteseka vitandani huku watu wasijue la kufanya, je, muda umefika kwa tanzania kuwa na utaratibu wa "kuua kwa huruma" kama ambavyo nchi za wazungu zinafanya? naomba maoni yako kwenye mjadala huu:

click here: Should "Mercy killing" be practiced in Tanzania?
 
Issue hapa Je,Askari Polisi wanajua mpaka yao ya kazi?Je wanajua haki za RAIA na haki za Mtuhumiwa? Kama wanajua basi kuna mahali panatatizo ni wakati wa RAIA kulishtaki jeshi la polisi kwa kutofuata taratibu na mpaka ya kazi yake.Kama.hawajui basi ni wakati wa serikali kukielimisha jeshi kuanzia wa ngazi ya chini hadi juu.
Pia je wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanajua mipaka yao na mpaka ya jeshi la polisi kwenye utendaji wa Polisi?Kama wanajua basi wanafanya makusudi kutumia nafasi zao kuumiza RAIA bila sababu.Kama hawajui basi ni Lazima Serikali ichukue hukumu la kuwaelimisha wasitie orders zinazopelekea kupiga au kujeruhi RAIA bila sababu zozote kwani mwenye hati ya Kuhukumu ni Mahakama tu
 
ZIFAHAM SHERIA ZAKO ZA MSINGI UKIKUTANA POLISI USINYANYASWE FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI
IMEANDALIWA NA MAWAKILI.
1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAM HAKI ZAO
.
 
Reactions: SIM
Kwa Tanzania bado ndugu, labda hadi hapo ccm itakapoondoka madarakani.
 
Kaka umeongea ukweli ila wachache tunaujua big up.
 
tumshukuru bwana Mpinga kwa kuweka misingi ya upolisi hasa wa barabarani. maana akikuonea kama una uhakika komaa hata mwende kituoni na dmand kuonana na responsible officer. sema sisi raia huwa hatuna muda ni quick fix ya 5,000 ama 10,000 au 30,000 ya receipt!!
 
WanaJF, kuna jambo huwa linaniumiza kichwa tena kwa nchi hii ya Tanzania.

Polisi unapomueleza kisheria au kujua wajibu wako kisheria hapo ndipo adui yako.

Ukimtajia wajibu wake au kapindisha basi jibu lake "unijifanya unajua sheria".
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] tuwazoee tu mkuu ndio walinzi wetu
 
Nini kifanyike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…